Mahmoud Ahmad Arusha
SERIKALI imefuta hati miliki ya mashamba saba katika mikoa ya Arusha na Manyara,ambayo hayajaendelezwa kwa kipindi kirefu na kuwagawia wananchi wenye uhitaji.
Waziri wa ardhi, nyumba na maendeleo ya makazi, William Lukuvi, ameyasema hayo Sep 10 jijini Arusha,alipokuwa akitoa tathimini ya utekelezaji wa maagizo ya rais Jakaya Kikwete, kuhusu utatuzi wa migogoro kabla hajaondoka madarakani.
Ameyataja mashamba hayo kuwa ni Tanzania Plantition ambayo ni mawili, Ufyomi Gallapo Estate,lenye ekari 1220,Kiru Palantation ekari 1536, Hamir Estate ekari 2400, Kiru Valley ekari 2930.
Aidha serikali inakamilisha mchakato wa kufuta hati miliki ya mashamba 48 yaliyopo wilayani Monduli, ambayo hayajaendelezwa kwa kipindi kirefu.
Amesema kwa kipindi kirefu mashamba hayo yamesababisha migogoro ambayo imesababisha wananchi wenye uhitaji kuvamia mashamba na kuzuka mapigano.
Amesema shamba la Tanzania Plantation limited,ya wilayani Arumeru, ambayo hayajaendelezwa kwa muda mrefu katika mgao huo halmashauri ya Meru imepata ekari 925 na Arusha, DC,ambayo imepata ekari 6176.5
Amesema katika mwendelezo huo wa kufuta hati miliki za mashamba serikali imetoa viwanja 100 katika shamba la Noor lililopo Oljoro kulipa fidia kwa wananchi wa jiji la Arusha,ambao walilipa gharama za kupatiwa viwanja kwa kipindi cha miaka 6 iliyopita na walikuwa hawajapata.
Waziri, Lukuvi, amevitaja vijiji vitakavyonufaika na mgao huo kuwa ni Msitu wa mbogo,Shambarai, Burka , Kikuletwa, Bwawani na Themi ya Simba, ambavyo vinayazunguka mashamba hayo ya Tanzania plantation.Amesema wananchi wanaohitaji ardh kwa ajili ya makazi na mashamba halmashauri ya wilaya ya Arusha DC ni 2000 na halmashauri ya Meru ni 400
Pia wanakijiji cha Oldonyo sambu , halmashauri ya Arusha DC, ambao shamba lao lilichukuliwa na jeshi la wananchi wa Tanzania, wamepewa viwanja katika eneo la Bwawani .
Amesema serikali inakamilisha mchakato wa kuyafutia hati miliki mashamba yote yaliyopo mkoani Morogoro,ambayo yametelekezwa na hayajaendelezwa.
Ameongeza kuwa tayari serikali imeshafuta mashamba mengine makubwa yaliyopo mkoani Pwani na kuyatoa kwa wananchi.
Ameongeza kuwa Septemba 12 mwaka huu atazindua mastare plani ya mji wa Kigamboni, na Septemba 13 ataenda mkoani Mwanza kuendelea na zoezi hilo la kufuta hati miliki za mashamba yote ambayo hajaendelezwa.
Amesema ni marufuku kwa viongozi wa vijiji katika maeneo hayo kujigawia mashamba hayo na atakae patikana atashughulikiwa kwa kuwa lengo ni kusaidia wananchi wenye uhitaji na kamwe sio viongozi.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni