Kufuatia safari ya vijana watano wa
U15 Asaad Ali Juma, Maziku Aman, Issa Abdi, Kelvin Deogratias,
Athumani Maulid waliokwenda kufanya mazoezi kwenye klabu ya Orlando
Pirates kufuatia mwaliko uliotolewa na TFF na klabu hiyo, safari hiyo
ilikamilika na vijana wamerejea nyumbani.
Vijana hawa waliongozana na
Mkurugenzi wa Ufundi wa TFF, Salum Madadi wakiwa Afrika Kusini
walifanya mazoezi ya wiki moja kuanzia Septemba Mosi mpaka tarehe 7
Septemba, 2015 chini ya uangalizi wa Augusto Placious ambaye ni
Mkurugenzi wa Ufundi wa Orlando Pirates.
Idara ya ufundi ya Orlando Pirates
imejiridhisha na kiwango kilichoonyeshwa na vijana hao.
Hatua inayofuata ni mawasiliano kati
ya shule wanazosoma hao vijana hapa Tanzania na klabu ya Orlando
Pirates ili kutafutiwa nafasi za masomo kwenye shule za Afrika
Kusini.
Jambo hili likikamilika vijana hao
watakwenda nchini Afrika Kusini kwa ajili ya masomo na kufundishwa
mpira.
TFF inamshukuru Dr. Irvin Khoza Rais
na mmiliki wa klabu ya Orlando Pirates kwa ushirkiano na kutoa nafasi
kwa vijana wa U15 Tanzania kwenda kufanya mazoezi kwenye klabu hiyo
kongwe nchini Afrik Kusini na kuendelezea
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni