Michuano ya Ligi ya Uropa imeanza
rasmi kwa msimu wa 2015-2016 huku ikishudia timu za Tottenham,
Schalke na Borussia Dortmund wakianza kwa ushindi.
Tottenham wakiwa nyumbani kwenye
dimba la White Hart Lane waliibuka na ushindi wa mabao 3 -1 dhidi ya
FK Qarabag, ambapo Heung-min Son alicheka na nyavu mara mbili.
Heung-min Son akishangilia moja ya bao lake
Apoel Nicosia wakiwa wenyeji wa
Schalke walikubali kichapo cha mabao 3-0, huku Borussia Dortmund
wakishinda kwa mabao 2-1 dhidi ya FK Krasnodar.
Matokeo mengine ya michuano hiyo ni
Ajax 2-2 Celtic, Bordeaux 1-1 Liverpool
Fenerbahçe 1-3 Molde na Anderlecht
1-1 Monaco.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni