Rais Barack Obama wa Marekani
amesema kuwa amevunjika moyo baada ya mfanyakazi mmoja mwandamizi wa
Ikulu kufa katika ajali ya baiskeli wakati wa shuguli ya kujitolea.
Mfanyakazi huyo Jake Brewer, 34,
alikufa wakati akishiriki msafara wa baiskeli wa kukabiliana na
Saratani siku ya jumamosi.
Afisa huyo ushauri wa sera katika
ofisi ya mkuu wa teknolojia alishindwa kumudu baiskeli yake na
kugongwa na gari.
Rais Obama amesema marehemu Jake
alijitolea maisha yake katika kuwawezesha watu, na kuifanya serikali
kufanya kazi vyema.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni