| Promota Kaike Silaju katikati akiwainuwa mikoni juu mabondia Thomas Mashali kushoto na Fransic Cheka baada ya kusaini mkataba wa kuzipiga desemba 25 katika uwanja wa jamuhuri Morogoro Picha na SUPER D BOXING NEWS | 
| Mabondia Thomas Mashali kushoto na Fransic Cheka wakionesha mikataba yao baada ya kusaini kuzipiga desemba 25 katika uwanja wa jamuhuri Morogoro Picha na SUPER D BOXING NEWS | 
| Bondia Fransic Cheka kushoto na Thomas Mashali wakisoma mkataba kabla ya kutia saini kwa ajili ya kuzipiga desemba 25 katika uwanja wa Jamuhuri Morogoro Picha na SUPER D BOXING NEWS | 
| Wakili Paul Kalomo kutoka Mega Attorneys akiwafafanulia kifungu kwa kifungu mabondia Thomas Mashali wa pili kushoto na Fransic Cheka kulia kabla awajasaini | 
| Promota Kaike Silaju katikati akipitia mkataba kabla ajawasainisha mabondia Thomas Mashali kushoto na Fransic Cheka ambapo wamekubaliana kuzipiga desemba 25 katika uwanja wa jamuhuri Morogoro Picha na SUPER D BOXING NEWS | 
Wakili
 Paul Kalomo akiwaelekeza mabondia Thomas Mashali kushoto na Fransic 
Cheka jinsi ya kusaini mkataba wa pili kushoto ni promota Kaike Silaju  
mabondia hawo watapigana desemba 25 katika uwanja wa jamuhuri morogoro .
Picha na SUPER D BOXING NEWS
 Na Mwandishi Wetu
Mabondia
 Thomasi Mashali na Fransic Chaka Jana wamesaini mkataba wa kuzipiga 
siku ya desemba 25 katika uwanja wa jamuhuri Morogoro
akisimamia utiaji saini huo 
Wakili
 Paul Kalomo kutoka Kampuni ya  Mega Attorneys amesema mkataba huo ni 
rasmi kwa mabondia hawo watapambana siku hiyo kwenye mpambano wa raundi 
kumi kwa dakika tatu kila raundi na kupumzika kwa dakika moja mpambano 
utakuwa wa raundi kumi na mabondia watapimwa afya zao siku moja kabla ya
 mchezo ili kujiridhisha kuwa wako fiti
nae 
promota wa mpambano uho ambaye amekuwa akiandaa mapambano makubwa 
makubwa na yenye msisimko nchini amesema kuwa mpambano uho unasubiliwa 
na mashabiki lukuki na nimeamua kuweka katika uwanja wa Jamuhuri 
Morogoro ili kuwapa fursa nyingine kwa wakazi wa morogoro kumwona Cheka 
ambaye kwa mda mrefu ajacheza
nae 
bondia Fransic Cheka amewaomba wapenzi na mashabiki wajitokezekwa wingi 
ili kuja kujionea kichapo atakachompa Mashali ambapo ndio kitamfanya 
ajutie kabisa kucheza mchezo wa ngumi
kwa 
upande wa Mashali amesema amefurai kupata nafasi nyingine ya kucheza na 
cheka kwani anataka kuonesha kiwango chake kilivyo kikubwa kwa sasa na 
yeye ni nambari wani katika ngumi nchini
katika
 mpambano huo siku hiyo kutakuwa na mapambano ya utangulizi ambapo 
bondia Vicent Mbilinyi atapambana na Deo Njiku wakati Mohamed Matumla 
atakabiliana na Cosmas Cheka
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni