TFDA YAZINDUA MAABARA YA KISASA YA UCHUGUZI WA MADAWA

Mkuu wa Maabara  ya Mikrobilojia wa Mamlaka ya Chakula na Dawa Nchini  (TFDA)Dk. Adelard Mtenga akitoa maelekezo juu ya kifaa  maalum cha uchunguzi wa Vifaa tiba ikiwemo nyuzi za ushonaji pamoja na dawa za sindano  ambapo ni kifaa cha kwanza Katika  Nchi za Kusini ,Mashariki na Kati  Barani Afrika. leo Jiji Dar es Salaam.
 Mkurugenzi Mkuu  wa Mamlaka ya Chakula na Dawa Hiiti  Sillo akikata utepe kufungua mtambo huo leo Jiji Dar es Salaam. Katiti ni mwakilishi mkazi wa Wizara ya Afya na Usitawi wa Jamii Dk. Mohammed Ally Mohammed kuli ni Mwakilishi wa Shirika la Msaada kutoka Marekani,Ms. Kelly Hamblin.
 Mkurugenzi Mkuu  wa Mamlaka ya Chakula na Dawa Hiiti  akifafanua jambo mbele ya wanahabari (hawapo pichani).
 Mwakilishi wa Shirika la Msaada kutoka Marekani,Ms. Kelly Hamblin akifafanua jambokwa waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo.
 Mkurugenzi Mkuu  wa Mamlaka ya Chakula na Dawa Hiiti  Sillo na Mwakilishi wa Shirika la Msaada kutoka Marekani,Ms. Kelly Hamblin  wakisani makabidhiano ya nyaraka za mradi huo.
 Mkurugenzi Mkuu  wa Mamlaka ya Chakula na Dawa Hiiti  Sillo na Mwakilishi wa Shirika la Msaada kutoka Marekani,Ms. Kelly Hamblin  wakisani makabidhiano ya nyaraka za mradi huo.
Wanahabari wakichukua matukio kwenye hafla hiyo.
Viongozi hao wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya hafla hiyo.Picha na Emmanuel Massaka.
MAMLAKA ya Chakula na Dawa Nchini(TFDA) imezindua jengo la maabara ambalo litatumika  kufanya uchunguzi wa madawa vyakula na vipodozi ili kubaini baadhi ya vijidudu hatarishi kwa afya ya binadamu.

Hayo yamesemwa leo jijini Dar es salaam na Mkurugenzi wa Mamlaka ya Chakula na Dawa Nchini(TFDA) Bw. Hiiti Sillo wakati akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya uzinduzi na makabidhiano ya Maabara hiyo.

Alisema kuwa Dawa zinazofanyiwa uchunguzi ni zile zinazoingia moja kwa moja kwenye mwili wa binadamu,ili kuhakiki kuwa ziko salama na hazina chembechembe yoyote ya wadudu wenye  kudhuru  afya za binadamu.

“Kifaa hiki kitasaidia kufanya uchunguzi kwa kiwango cha kimataifa na pia hakitaruhusu chembechembe yoyote kupita kwenye dawa na kuathiri afya ya binadamu”alisema.

Naye Mkurugenzi wa uhakiki wa Ubora wa huduma ya afya kutoka Wizara ya afya na Ustawi wa Jamii Daktari Mohamed Mohamed amesema kuwa maabara hiyo inahitaji uangalizi wa kutosha ili kutunza vifaa katika maabara pamoja na kutoa elimu kwa wataalamu wa maabara hiyo.

Ukarabati wa jengo hilo umegharimu jumla ya fedha za kitanzania kiasi cha shilingi milioni 489,ambapo serikali ya Tanzania imechangia kiasi cha shilingi milioni 91 huku shirika la misaada la marekani(USAID) limegharamia shilingi milioni 398.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni