Mwenyekiti wa umoja wa vijana wa UVCCM taifa, Sadifa Juma
Khamisi, amewapongeza vijana mkoani Arusha kwa mshikamano walionao katika
kipindi hiki cha kampeni na mshikamano ambao unatoa imani kubwa kwa chama cha
mapinduzi kupata ushindi kwenye uchaguzi mkuu ujao. 
 
Sadifa,ametoa pongezi hizo leo alipokuwa akizungumza kwenye
kikao cha shirikisho la vyuo vikuu mkoa wa Arusha kwa pamoja na baraza la UVCCM
wilaya ya Arusha kilichofanyika ukumbi wa Chama cha Mapinduzi mkoa.
 
Sadifa,amewataka vijana wasilale bali waimarishe kampeni
katik kipindi hiki ili chama cha mapinduzi kipate ushindi mkubwa kwenye
uchaguzi mkuu ujao..
 
Amwataka makatibu wa UVCCM,mkoa na wilaya zote nchini kufanyia
kazi kwa haraka pindi wanapopata taarifa za kuwepo matukio ya kuwakwamisha
vijana kufanya kazi ikiwemo,kufanyiwa vurugu na  kushambuliwa na wanachama wa upinzani .
 
 
 Amewataka vijana kujipanga
tayari kuwakabiri wanachama wa vyama vya upinzania ambao wanakusudia kuvuruga
uchaguzi na kuwakumbusha kuwa vijana ndio walinzi wa chama cha mapinduzi.
 
Pia
 amewataka kufanya kampeni za kistaarabu ambazo zitawashawishi wapiga 
kura kukipigia chama cha mapinduzi kura na hivyo kuibuka na ushindi wa 
kishindo ila yeyote atakaye mchokoza mmoja wenu uvumilivu sio silaha ya 
vijana bali mjibu mapigo.
"Najua
 wamejipanga kuhakikisha kuwa wanaharibu uchaguzi nyie muwe wastaarabu 
katika kuhakikisha chama chetu kinapata ushindi kuanzia kwa dkta 
Magufuli hadi kwa madiwani wetu ifikapo oktoba 25"alisema Sadifa
Aidha
 mkutano huo wa ndani wa vijana jijini hapa uliofanyika katika ukumbi wa
 ccm mkoa uliibua hisia mbali mbali huku vijana wakitunishiana misuli 
hali iliyopelekea mwenyekiti huyo wa uvccm taifa kuweka sawa hali hiyo 
na mwisho kuondoka ukumbini hapa.
Sadifa
 alisema kuwa hali ya sasa ya kisiasa inavyoonekana wenzetu wamejipanga 
kuhakikisha uchaguzi unakuwa si wa amani lakini msiwafuate hadi pale 
watakapowachokoza ndiyo hapo vijana onyesheni kuwa nanyi ni vijana.
 
 
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni