AUWAWA INDIA KWA KUDAIWA KUWA YEYE NA FAMILIA YAKE WANAKULA NYAMA

Mwanaume mmoja kaskazini mwa India ameuwawa na kundi la watu kutokana na uvumi kuwa familia yake imekuwa ikihifadhi nyumbani na kula nyama ya ngome jambo ambalo ni mwiko nchini humo.

Mwanaume huyo Mohammad Akhlaq alipigwa mateke na kutupiwa mawe hadi kufa na na kundi la wanaume katika mji Dadri, katika jimbo Uttar Pradesh, ambapo mtoto wake wa kiume naye amejeruhiwa vibaya.

Uchinjaji ng'ombe ni jambo ambalo halikubaliki sana nchini India ambapo wanyama wanachukuliwa kama viumbe watakatifu na dhehebu la Hindu ambalo ni asilimia 80 ya idadi ya watu bilioni 1.2.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni