![]()  | 
| Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Abbas Kandoro (PICHA MAKTABA) | 
Na Kahema Emanuel,Mbeya
WITO
 umetolewa kwa Waratibu  wa uchaguzi wa mikoa ,wasimamizi  wa uchaguzi 
na wasimamizi wasaidizi pamoja na maafisa uchaguzi wa halmashauri mikoa 
ya kanda za juu kusini  kuhakikisha wanafanya kazi zao kwa waledi na kwa
 uadilifu bila kuwa na upendeleo wa chama chochote cha siasa ua mgombea.
Kauli
 hiyo imetolewa na Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Ndugu Abbas Kandoro wakati 
akifungua mafunzo ya wasimamizi wa uchaguzi na wasimamizi wasaidizi 
pamoja na maafisa uchaguzi halmashauri ambao ni wakurugenzi wa 
halmashauri na maafisa uchaguzi katika mikoa  ya Iringa na Mbeya.
Amesema
 ili zoezi hilo la uchaguzi liende vizuri na lisighubikwe na vurugu 
nivema wasimamizi hao wakatumia waledi wao na udilifu bila kuwa na 
upendeleo wa chama chochote cha siasa au mgombea yoyote ili kuepuka hali
 hiyo. 
Amesema
 mara baada ya kupatiwa mafunzo hayo nivema wakaendelea kutumia muda wao
 wa ziada kusoma na kupitia  vitabu vya maelekezo waliyopatiwa kwa 
kutumia kanuni na maadili ya uchaguzi ili kuimarisha uelewa zaidi kuhusu
 wajibu na majukumu yao katika zoezi hili la uchaguzi mkuu mwezi Oktoba.
Amesema
 pamoja na majukumu mengine waliyonayo pia wametakiwa kutoa kipaumbele 
katika kutekeleza zoezi hili la kitaifa kwa ufanisi zaidi na kwa muda 
uliopangwa kwani uchaguzi huu utafanyika kwa siku moja tu kwa kila baada
 ya miaka mitano.
Aidha
 amesema kuwa Tume ya Taifa ya Uchaguzi imetekeleza jukumu lake katika 
hatua ya mafunzo na maandalizi ya vifaa na rasilimali nyingine hivyo wao
 kama wasimamizi wanatakiwa kutekeleza wajibu wao katika ngazi zote kwa 
mujibu wa taratibu zilizopangwa na Tume.
Katika
 semina hiyo wasimamizi hao watajifunza wajibu wa wasimamizi wa vituo 
vya kupigia kura  ,uwendeshaji wa zoezi la upigaji kura vituoni  sanjali
 na uendeshaji wa zoezi la kuhesabu kura,kujumlisha kura na kutanganza 
matokeo ya uchaguzi.
| Afisa Uchaguzi Kanda ya Nyanda za juu kusini -Tume Ndugu Jane Tungu akizungumza katika semina hiyo. | 

Hakuna maoni:
Chapisha Maoni