PAPA FRANCIS AKUSANYA WATU BAADA YA KUTOKA KWENDA KUNUNUA MIWANI

Kiongozi wa Kanisa Katoliki Dunian Papa Francis amejikuta akikusanya kundi la watu baada ya kutoka kiana Vatican kwenda kumuona daktari wa macho anayepima miwani.

Kwa kawaida daktari huyo hupeleka miwani Vatican, lakini Papa Francis alisisitiza kwenda mwenye kwenye duka la miwani kati kati ya Jiji la Roma.

Papa Francis amekuwa akilalamika mara kwa mara kukosa uhuru wa kutembea bila ya walinzi katika mitaa ya Roma.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni