Katika
hali isiyotarajiwa na wengi katika Jimbo la Moshi Mjini, Mgombea
Ubunge kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi Davis Mosha ameanza utekelezaji
wa ahadi zake katika Jimbo hilo, wiki chache baada ya kuzungumza na
wanamuziki na wasanii kuhusu kazi zao na wasanii hao kuomba kupata kituo
cha Redio cha kisasa na Studio ya kisasa ambavyo vitaweza kufanya kazi
zao kwa ubora zaidi na pia kufika mbali.
Katika
kutekeleza hilo Mh. Davis Mosha amekwishaanza ujenzi wa Studio ya
Kisasa ya Kituo cha Redio chini ya Kampuni yake ya Africa Swahili Media
na ujenzi huo unatarajiwa kukamilika mapema na vifaa vya Studio huyo
vinatarajiwa kuwasili muda wowote kutoka Dar es Salaam baada ya kuwasili
Bandarini vikitokea Nchini Italy. Mh. Davis Mosha aliwaahidi wasanii
hao kufungua kituo cha Redio kitakachoweza kusikika Tanzania Nzima na
Duniani kote kwa njia ya Satelite. Pia aliwahakikishia kufungua na kituo
cha televisheni. Kituo hicho cha Redio na Studio ya kisasa
kianatarajiwa kufunguliwa katika jingo la Kilimanjaro Commercial Complex
Maarufu kama jingo jipya la NSSF lililopo Moshi Mjini.
|
Mh. Davis Elisa Mosha |
|
Hati ya Kontena la Vifaa vya Studio lililotoka Italy Baada ya kuingia Bandari ya jiji la Dar es Salaam. |
Mbali
na utekelezaji huo wa Kero ya Wasanii, Mh. Davis Elisa Mosha wiki
iliyopita aliweza kufanya Ziara ya kimya kimya katika Soko la Mitumba la
King George Memorial na kutazama Changamoto za Soko hilo lakini pia
alipata fursa ya kuzungumza na uongozi wa Soko hilo na wafanyabiashara
wa Soko hilo. Kwa pamoja walieleza MAzingira magumu wanayofanyia
Biashara huku ikiwa Miundombinu mibovu ikiwemo vyoo na Soko halina Paa
inapelelea iwapo mvua itanyesha basi kunakua hakuna biashara kabisa
maana Bidhaa hunyeshwa na Mvua na mbali na Mvua pia jua ni lao. Katika
kutatua changamoto hizo Davis Mosha aliwaahidi kulifanyia kazi mapema
tatizo lao na hatosubiri mpaka muda wa uchaguzi ufike maana adha hiyo
wanayoipata ni wananchi wa Moshi wakiwemo mama zake na baba zake waliopo
hapo Sokoni.
|
Mh. Davis Mosha alipotembelea Soko la Mitumba la Memorial na kujionea changamoto mbalimbali. |
|
Mh. Davis Mosha akisalimiana na wafanyabiashara wa soko la Memoria alipotembelea soko hilo. |
Kutokana
na Ahadi hiyo Jana Mh. Mosha aliwasili Sokoni hapo na Mainjinia kutoka
Kampuni ya Group Six ltd ambao ni Raia wa China kwa lengo la kufanya
kufanya vipimo na Michoro ya uboreahwaji wa Soko hilo ili kuweza kuondoa
changamoto zinazowakabili wafanyabiashara wa Soko hilo. Mainjinia hao
walizunguka katika Soko hilo na kutazama eneo la Soko ili kuweka mipango
ya kuanza ujenzi wa Soko hilo ambapo ujenzi huo hautoathiri
wafanyabashara hao kuendelea kufanya biashara zao.
|
Mainjinia
Raia wa China kutoka Kampuni ya Group Six wakiwa soko la Mitumba la
Memorial kwa ajili ya kufanya ukaguzi wa Matengenezo ya soko hilo. |
|
Mh. Mwigulu Nchemba akimkaribisha Mh. Davis Mosha azungumze na Wafanyabiashara wa Soko la Memorial |
|
Mh. Davis Mosha akizungumza na wafanyabiashara wa Soko la Mitumba la Memorial |
Kutokana
na utekelezaji huo wa ahadi wananchi mbalimbali wameonekana
kufurahishwa na aina ya kiongozi waliompata ambaye anaomba Ridhaa ya
kuchaguliwa kuongoza Jimbo la Moshi Mjini. Haata hivyo katika mkutano wa
Hadhara uliofanyika jana katika Soko hili ulihudhuriwa na Viongozi
mbalimbali wakiongozwa na Mh. Mwigulu Nchimbi ambaye alipata fursa ya
kumzungumzia Davis Mosha. Mwigulu alisema kazi ngumu kuliko zote ni
kutomchagua Davis Mosha kuwa Mbunge wa Moshi mjini na kazi Rais sana ni
kumchagua Davis Mosha. Aliwaambia wakazi wa Moshi kuwa wana bahati ya
kipekee kupata Mbunge ambaye ameanza utekelezaji wa ahadi zake kabla ya
kusubiri bajeti ya serikali na viongozi kama hao ndi o Tanzania
inawahitaji, Kwahiyo ikifika 25 mwezi wa Kumi wasifanye kosa wamchague
Davis Elisa Mosha awe Mbunge wa Moshi Mjini pamoja na Madiwani wake wa
ccm na bila kusahau kumpa kura za Kishindo Mgombea Urais wa ccm Ndugu
John Pombe Magufuli.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni