Meneja Ufanisi wa Mgodi wa Dhahabu wa
Bulyanhulu, BGML, unaomilikiwa na Kampuni ya Acacia, Elias Kasikila, (kushoto),
akiagana na baadhi ya vijana wanaokwenda kuhudhuria mafunzo ya ufundi chini ya
mpango wa IMTT unafadhiliwa na mgodi huo, wakati wa hafla ya kuwaaga
iliyofanyika mwishoni mwa wiki kwenye eneo la mgodi, huko Msalala mmoani
Shinyanga. Mgodi huo umetuamia kiasi cha zaidi ya nusu bilioni kila mwaka kufadhili mpango huo
Na K-VIS MEDIA
MGODI
wa dhahabu wa Bulyanhulu, BGML, unaomilikiwa na kampuni ya uchimbaji na
utafutaji madini ya Acacia, umetumia kiasi cha zaidi ya shilingi nusu bilioni
kila mwaka, kufadhili mafunzo ya ufundi kwa vijana, chini ya mpango wa IMTT.
Mpango
wa kufadhili mafunzo ya IMTT, (Integrated Mining Technical Training), ulianzishwa
mnamo mwaka 2009, ambapo mgodi huo hutoa fedha kufadhili elimu hiyo kwa vijana
wenye elimu ya kidato cha nne ambao walisoma kwenye shule zilizoko vijiji 14 vinavyozunguka
mgodi huo na kushindwa kuendelea na kidato cha sita kwa sababu mbalimbali lakini
wawe na umri usioozidi miaka 25.
Akizungumza
kwenye hafla ya kuwaaga vijana 20 kutoka vijiji hivyo kwenye mgodi huo, mwishoni
mwa wiki ambao wameenda kuanza mafunzo hayo yanayochukua muda wa miaka kati ya
mitatu na miwili kwenye chuo cha VETA-Moshi, Menenja Ufanisi (OE),wa BGML,
Elias Kasikila, alisema, ufadhili huo ni utekelezaji wa sera ya mgodi
kushirikiana na wenyeji wao, (wananchi wanaoishi maeneo yanayozunguka mgodi),
katika kujenga mahusiano mema.
Akielezea
utaratibu wa kuwapata vijana hao, Kasikila alisema, waombaji hupeleka maombi
yao kwenye ofisi za serikali za vijijina kisha maombi hayo kukabidhiwa kwa
uongozi wa mgodi ambao huyaachuja kwa kuzingatia vigezo vilivyowekwa.
“Sharti
muombaji awe amefaulu masomo ya Kiingereza na Hisabati, lakini kupitia kitengo
chetu cha usalama, vijana hao huchunguzwa tabia zao huko walikotoka, ikiwa ni
pamoja na kufanyiwa vipimo vya kiafya na wanaokidhi vigezo hivyo huchaguliwa.”
Alifafanua
Mafunzo
yanayotolewa ni pamoja na ufundi umeme kwa miaka mitatu, fitting na uchomeleaji
vyuma, kwa miaka miwili, Diesel mechanic and Instrument, kwa miaka mitatu.
Alifafanua Kasikila.
Alifafanua Kasikila.
“Kila
kijana tunamlipia shilingi milioni 7 kwa mwaka ambazo hutumika kama ada,
malazi, ununuzi wa vitabu na vifaa, lakini pia tunawapatia shilingi 100,000 kwa
kila kijana kila mwezi ikiwa ni kitunza mfuko kwa matumizi madogomadogo bila
kusahau usafiri wa kwenda na kurudi kutoka chuoni.”
Alisema Meneja huyo
Alisema Meneja huyo
Kasikila
alisema, vijana 64 waliotokana na mafunzo hayo wamepata ajira ya kudumu, 59
kwenye migodi inayomilikiwa na kampuni ya Acacia, na watano (5), wameajiriwa na
mgodi wa Geita Gold Mine, GGM), huku wengine 89 wanafanya kazi mafunzoni,
(trainees).
“Lengo
kuu la mafunzo haya sio kutoa ajira kwa vijana hawa, bali ni kuwajengea uwezo
wa kujiajiri wengine na wachache huwa
tunawachukua lakini pia huwa tunawaunganisha na taasisi nyingine zinazohitajio
utaalamu wao.” Alifafanua Kasikila.
Akitoa
shukrani kwa niaba ya vijana wenzake, Baraka Nasoro, aliushukuru mgodi huo kwa
kuwawezesha kupata fursa ya kielimu na kuwaasa wenzake kujituma ili hatimaye
kumaliza masomo kwa mafanikio.
Naye mwakilishi wa
wazazi wa vijana hao, Rhoda Aaron, amewataka vijana hao kujiepusha na vitendo
vya anasa na uasherati ili waweze kushiriki vema mafunzo na kuzingatia
kilichowapeleka
Maafisa wa BGML, wanaosimamia mpango wa IMTT
Kasikila akitoa nasaha zake
Baadhi
ya vijana waliofaidika na IMTT mwaka huu wakisiliza kwa makini nasaha
zilizokuwa zikitolewa na uongozi wa BGML, na wazazi wao
Wazazi wa vijana waliofaidika wakisikiliza
Mmoja wa wazazi wa vijana hao, Rhoda Aaron, akitoa shukrani zake na nasaha kwa vijana
Kasikila, (kulia), akipongezwa na Rhoda
Maafisa wa BGML, wanaosimamia mpango wa IMTT
Mwakilishi wa vijana hao, Baraka Nasoro, akitoa shukrani zake kwa niaba ya wenzake
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni