Mkurugenzi wa kampuni ya BIMO Media , Bertha Ismail akisoma risala katika ufunguzi wa maadhimisho ya ufunguzi wa michuano ya Nyerere Cup 2015 yaliyokuwa yakitimua vumbi katika uwanja wa Stedium jijini Arushaambapo pia yataambatana na mashindano ya kila mwaka  ya kielimu  ya uandishi wa insha,makala pamoja na uchoraji  picha juu ya masuala ya utalii  kwa wanafunzi wa shule za msingi 25 zilizopo Arusha yaliyoandaliwa na kampuni ya BIMO Media
Mgeni
 rasmi Afisa Elimu jiji la Arusha kwa shule za sekondari Josephat 
m.Ntabindi akiongea na vyombo vya habari pamoja na wanamichezo chini ya 
umri wa miaka 13,alisema kuwa mashindano hayo ni kwa ajili ya kumuenzi 
hayati baba wa taifa Mwl Julias Nyerere ambaye pia alikuwa mstari wa 
mbele katika kuhamasisha michezo.
Mgeni
 rasmi ambaye Afisa Elimu jiji la Arusha kwa shule za sekondari Josephat
 M.Ntabindi akisalimiana na wachezaji kabla ya mechi ya TIMU ya Maafande wa JKT Oljoro ya jijini Arusha na  timu ya AFC Arusha katikaufunguzi wa michuano ya Nyerere Cup 2015. 
Watoto wenye chini ya umri wa miaka 13 wakifanyiwa mahojiano ,aliyeshika maiki ni mmiliki wa jamiiblog Bi.Pamela Mollel
TIMU
 ya Maafande wa JKT Oljoro ya jijini Arusha inayoshiriki ligi daraja 
lakwanza imeshindwa kuonyesha makali mbele ya wadogo zao  timu
 ya AFC Arusha inayoshiriki ligi daraja la pili baada ya kutoka suluhu 
ya bao 1-1 katika ufunguzi wa michuano ya Nyerere Cup 2015.
Mchezo
 huo uliofanyika katika uwanja wa Sheikh AmrI Abeid ,uliiwashuhudia 
maafande hao wa Oljoro wakianza kucheka na nyavu za AFC baada ya 
kujipatitia bao lake kupitia kwa mchezaji Swalehe Idd alilofunga kwa 
njia ya Penalti mnamo dakika ya 58, iliyosababishwa na mabeki wa timu 
pinzani kunawa mpira katika eneo la hatari.
Vijana
 wa AFC walionyesha juhudi zao kwa kulishambulia lango la Oljoro ambapo 
walifanikiwa kusawazisha bao mnamo dakika ya 88 kupitia kwa mshambuliaji
 wao Wandima Malechela baada ya kuachia  shuti kali lililokwenda moja kwa moja vyavuni.
Mashindano hayo yameandaliwa na kampuni ya BIMO Media yakiwa na kauli mbiu ‘Uchaguzi wa Amani  2015,ndio
 taifa moja kwa maendeleo ya utalii nchini’ yatazishirikisha pia timu za
 watoto chini ya miaka 13 ambao watachuana vikali ili kuweza kumpata 
mshindi ambaye atatangazwa siku ya kilele tarehe 19 mwezi huu.
Akifungua
 mashindano hayo Afisa Elimu jiji la Arusha kwa shule za sekondari 
Josephat m.Ntabindi alieleza kuwa mashindano hayo ni kwa ajili ya 
kumuenzi hayati baba wa taifa Mwl Julias Nyerere ambaye pia alikuwa 
mstari wa mbele katika kuhamasisha michezo.
“Michezo hii inawakutanisha vijana hawa  wakiwa na uwezo wao tofati  ambapo pia yatawajengea urafiki  na uhusiano mzuri baina yao  vile vile   yatawasidia kuweza kuimarisha vipaji vyao  vitakavyotumika
 katika kuandaa taifa lililo na vijana wenye uwezo mzuri na pia 
yatahamasisha utalii kwani mkoa huu una vivutio vingi.”alieleza 
Ntabindi.
Naye mkurugenzi wa kampuni ya BIMO Media , Bertha Ismail alisema  maadhimisho hayo yataambatana na mashindano ya kila mwaka  ya ki- elimu  ya uandishi wa insha,makala pamoja na uchoraji  picha juu ya masuala ya utalii  kwa wanafunzi wa shule za msingi 25 zilizopo Arusha.
“ Lengo ni  kuhamasisha uchaguzi wa mwaka huu kufanyika kwa amani vile vile kuhamasiha watu  kuhudhuria hifadhi za utalii zilizoasisiwa na Mwl Nyerere na tunategemea Zaidi ya wanafunzi 700 watashiriki  katika shindano hilo la isha.”ismail alifafanua.
Timu
 za nyota academy,Future Stars,Kijenge Youth,Rolling Stone,Young Life na
 palloti zitachuana na washindi watakabidiwa zawadi mbalimbali ikiwemo 
vikombe na fedha.




Hakuna maoni:
Chapisha Maoni