TIMU ya
 panone FC ya mjini Moshi, mkoani Kilimanjaro maarufu kama matajiri wa 
mafuta ,inatarajia kuanza kutupa karata yake ya mchezo wa kwanza wa ligi
 daraja la kwanza(FDL) dhidi ya maafande wa JKT Oljoro ya jijini Arusha.
Mchezo  huo
 utafanyika septemba 19 mwaka huu, katika uwanja wa Ushirika mjini moshi
 mkoani kilimanjaro,ambapo  baada ya mchezo huo pia wataikaribisha timu 
ya Polisi Tabora semptemba  26.
Katibu
 wa timu ya Panone FC  Augstino mwakatumbula alisema kuwa 
msimu  huu  wanaenda kuanza ligi daraja la kwanza  ambapo kila mchezo 
kwao ni fainali na watahakikisha wanatinga kucheza ligi kuu msimu wa 
2016-2017.
“Tulifanya
 usajili mzuri wa wachezaji 7  ambao wameungana na wachezaji wetu 
tuliokuwa nao msimu uliopita na  tunaimani
 wataisaidia timu hii na tuna jumla ya wachezaji 27 wanaounda kikosi cha
 timu pia hatukuweza kuwasajili wote waliokuwepo hapo mwanzo na  ni 
kutokana na matatizo mbalimbali yakiwemo wengine  kutokuwa na 
nidhamu,uwezo wao umeshuka kimchezo.”alisema Mwakatumbula .
Aliwataja
 wachezaji hao saba  ambao wamefanikiwa kusajiliwa na matajiri hao wa 
mafuta kuwa ni pamoja na Ally Mseja ambaye ni mchezaji huru na Abdallah 
Shauri ‘Machopa’ aliyetokea timu ya Lipuli –Iringa wote wakiwa ni 
washambuliaji, Florence  Haure kutoka academy ya Kitayosce ya mkoani 
Kilimanjaro, Frank Kijoti aliyetokea AFC Arusha Rashid Gumbo 
kutoka  Kinondoni Manispaa ambaao wote ni Kiungo,Maulid 
Khalid kutoka  Singida United ambaye ni winga,Mansoul Mansoul  kutoka 
Coastal Union ya Tanga ambaye ni golikipa.
Timu
 hiyo ya Panone FC ipo kambini miezi miwili sasa ikijiweka tayari kwa 
ajili ya michuano hiyo ya ligi Daraja la kwanza ambapo inatarajiwa 
kucheza michezo ya kirafiki mapema wiki hii  na timu za  African sports,Magambo JKT na Coastal Union zote za Tanga .
Matajiri hao wa mafuta wananolewa na kocha Atuga  Manyundo akisaidiwa na msaidizi wake Azizi Nyoni .
Ligi
 daraja la kwanza ina shirikisha jumla ya timu 24 zilizogawanywa katika 
makundi matatu ambapo timu ya Panone ipo katika kundi ‘C’ na timu za JKT
 Olojro- Arusha,Polisi Mara –Mara,Rhino Rangers –Tabora,Mbao fc 
–Mwanza,Polisi Tabora  -Tabora,Geita Gold –
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni