Mratibu Mkazi wa Mashirika ya
Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP) nchini,
Alvaro Rodriguez akizungumza wakati akizindua Malengo Endelevu 17 ya Maendeleo nchini
(SDG’s) Tanzania katika shule ya Uhuru mchanganyiko, katika hafla
ambayo pia benki ya Standard Chartered Tanzania ilishiriki na kugawa
vitu mbalimbali kwa ajili ya wanafunzi wa shule hiyo. (Picha na Zainul
Mzige wa Modewjiblog)
Na Mwandishi wetu
Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja
wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP) nchini, Alvaro
Rodriguez, amesema uondoaji umaskini nchini unawezekana kwa ushirikiano
kati ya wadau mbalimbali wa maendeleo.
Kauli hiyo ameitoa mwishoni mwa wiki wakati akizindua Malengo Endelevu 17 ya Maendeleo nchini
(SDG’s) Tanzania katika shule ya Uhuru mchanganyiko, katika hafla
ambayo pia benki ya Standard Chartered ilishiriki na kugawa vitu
mbalimbali kwa ajili ya wanafunzi wa shule hiyo.
Katika hafla hiyo ambayo
ilitengenezwa mahususi kuanzisha utekelezaji wa Malengo Endelevu (SDG’s)
yakiwemo ya elimu, afya na mazingira Standard walipeleka miti 150 ya
kupanda, kompyuta na pia kutumia muda kuangalia afya za wanafunzi.
Alisema katika kukabiliana na
umaskini kwa kuangalia Maendeleo Endelevu hakuna kitu kigumu
ukilinganisha na ugumu wa mwanafunzi asiyeona kujifunza kwa kupitia
vitabu vya nukta nundu na asiyesikia kuwasiliana na mtu mwingine lakini
pamoja na ugumu huo watoto hao wanaweza.
Alisema kwa ushirikiano wa wadau
kama walivyofanya wao na benki ya Standard Chartered Tanzania anaamini
kwamba maendeleo yatafikiwa na Tanzania itafanikiwa kuzika umaskini
ifikapo mwaka 2030.
Alisema kutiwa saini kwa Malengo
Endelevu na viongozi wa nchi 190 kumeonesha wazi nia ya seriakli
mbalimbali duniani kushughulikia umaskini na kuuzika kwa kutekeleza
malengo hayo endelevu.
Mwakilishi wa Mkurugenzi wa Benki
ya Standard Chartered Tanzania, Charles Katongole akitoa salamu za
Mkurugenzi wake ambapo benki hiyo imeahidi kushiriki kikamilifu katika
kuhakikisha utekelezaji wa malengo mapya ya Maendeleo Endelevu (SDG's)
yanafanikiwa nchini Tanzania. Kushoto ni Mratibu Mkazi wa Mashirika ya
Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP) nchini,
Alvaro Rodriguez, Mtaalam wa Mahusiano na Mawasiliano wa Umoja wa
Mataifa (UN) Tanzania Hoyce Temu (kulia) pamoja na Mkuu wa Mahusiano wa
benki ya Standard Chartered Tanzania, Juanita Mramba (wa pili kulia).
Naye Mwakilishi wa Mkurugenzi wa
Benki ya Standard Chartered Tanzania, Charles Katongole, alisema kwamba
ni lengo la benki hiyo ni kurejesha faida kwa jamii kupitia miradi yake
mbalimbali na kwamba kusaidia shule hiyo ya Uhuru mchanganyiko
iliyoanzishwa 01-01-1921 awali ikiitwa Government African secondary
school kabla ya kuhamishiwa Mzumbe Morogoro 01-01-1953 na kubadilishwa
jina kuwa Kichwele African boys middle school ikiwa na madarasa ya
V-VII, ni sehemu ya kurejesha faida kwa jamii.
Alisema ni lengo la benki hiyo kwa
mwaka huu kuwezesha kupatikana kwa dola za Marekani milioni 5 kusaidia
mambo mbalimbali ya watoto kwa mwaka huu kwa nchi za Afrika mashariki
huku Tanzania pekee watoto milioni 10 wakifikiwa.
Benki hiyo yenye matawi Dar es
salaam, Mwanza na Arusha katika miradi yake ya afya, vijana na elimu
wamekusudia kushirikiana na Umoja wa Mataifa kutekeleza malengo
mbalimbali endelevu ikiamini kwamba jamii ikiboreshwa itakuwa katika
mfumo mzuri wa maendeleo na kupiga vita umaskini.
Malengo ya SDG’s yamepangwa kutekelezwa katika kipindi cha miaka 15.
Mwalimu Mkuu wa Shule ya msingi
Uhuru mchangayiko, Anna Mshana akitoa risala fupi ya shule yake sambamba
na changamoto zinazoikabili shule yake kwa ugeni huo kutoka Umoja wa
Mataifa na Benki ya Standard Chartered Tanzania.
Mwalimu Mkuu wa shule hiyo Anna
Mshana alisema shule hiyo ambayo ilianzisha kitengo cha wanafunzi
wasioona 1962 na kubadilishwa kuwa Shule ya msingi Uhuru mchanganyiko
mwaka 1964, inakabiliwa na changamoto mbalimbali.
Miongoni mwa matatizo ni miundombinu
ya shule hiyo isiyokidhi mahitaji halisi, ukosefu wa ukuta, mashine za
kufundishia watoto wasioona, upungufu wa mabweni, magodoro, vitanda na
gari la kuwakimbiza hospitalini inapotokea dharura.
Alisema ingawa kuna taasisi hutoa
msaada wa gari na matibabu kwa watoto mchana, lakini nyakati za usiku
kukitokea dhararu inabidi shule igharamie ingawaje wakati mwingine
hatuna fedha inakuwa ni changamoto kwetu.
Alisema Shule ya msingi Uhuru
mchanganyiko yenye kutoa elimu jumuishi ina vitengo vya ufundi seremala
(1975) wanafunzi wenye mahitaji maalumu ulemavu wa akili (1984) na
viziwi na wasioona (Deafblidn) kilichoanzishwa mwaka 1994.
Wanafunzi ambao ni viziwi nao walipata fursa ya kuja kila kinachoendelea kutoka kwa mkalimani wao.
Mkuu wa Mahusiano wa benki ya
Standard Chartered Tanzania, Juanita Mramba akitangaza wanafunzi 17
ambao walishiriki shindano la kuhifadhi malengo mapya ya Maendeleo
Endelevu (SDG's) wakati wa kukabidhi zawadi kwa wanafunzi hao wa shule
ya Uhuru mchanganyiko.
Mratibu Mkazi wa Mashirika ya
Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP) nchini,
Alvaro Rodriguez akikabidhi zawadi zilizotolewa na Benki ya Standard
Chartered Tanzania kwa wanafunzi hao, sambamba na Mwakilishi wa
Mkurugenzi wa Benki ya Standard Chartered Tanzania, Charles Katongole.
Mwakilishi wa Mkurugenzi wa Benki
ya Standard Chartered Tanzania, Charles Katongole akimkabidhi Mwalimu
Mkuu wa Shule ya msingi Uhuru Mchanganyiko, Anna Mshana (wa pili
kushoto) moja kati ya kompyuta tano zilizolotolewa na Benki hiyo ikiwa
ni kama ishara ya utekelezaji wa lengo namba nne “Quality Education”
wakati wa uzinduzi wa Malengo mapya ya Maendeleo Endelevu (SDG’s)
uliofanywa na Benki ya Standard Chartered Tanzania kwa kushirikiana na
Umoja wa Mataifa katika shule ya msingi Uhuru mchanganyiko jijini Dar
mwishoni mwa wiki. Kulia ni Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa
Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP) nchini, Alvaro
Rodriguez na kushoto ni Mjumbe wa Bodi ya Shule ya msingi Uhuru
Mchanganyiko, Bw. Abubakar Mwambungu wakishuhudia tukio hilo.
Kompyuta tano zilizotolewa na Benki ya Standard Chartered Tanzania kwa shule ya Uhuru mchanganyiko.
Mwakilishi wa Mkurugenzi wa Benki
ya Standard Chartered Tanzania, Charles Katongole (wa tatu kushoto),
Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika
la Maendeleo (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez (katikati), Mwalimu Mkuu wa
Shule ya msingi Uhuru Mchangayiko, Anna Mshana (wa pili kushoto),
Mjumbe wa bodi ya kamati ya Shule ya msingi Uhuru Mchanganyiko,
Abubakari Mwambungu (kushoto) pamoja na baadhi ya wafanyakazi wa Benki
ya Standard Chartered Tanzania katika picha ya pamoja huku wakiwa
wameshikilia miche ya miti mbalimbali ikiwemo ya matunda ambapo zaidi
ya miche 150 ya miti ilipandwa kuzunguka mazingira ya shule hiyo kulinda
mazingira ikiwa ni ishara kwa vitendo ya utekelezaji wa lengo namba 13
"Climate Action" kati ya Malengo 17 mapya ya Maendeleo Endelevu (SDG’s)
nchini Tanzania.
Pichani juu na chini baadhi ya wanafunzi na walimu wa shule ya msingi Uhuru mchanganyiko waliohudhuria uzinduzi huo.
Mwakilishi wa Mkurugenzi wa Benki
ya Standard Chartered Tanzania, Charles Katongole sambamba na Mratibu
Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la
Maendeleo (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez wakishiriki zoezi la upandaji
miti kuzunguka maeneo ya shule ya Uhuru mchanganyiko jijini Dar mwishoni
mwa wiki.
Mratibu Mkazi wa Mashirika ya
Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP) nchini,
Alvaro Rodriguez akishiriki zoezi la upandaji miti sambamba na baadhi ya
wanafunzi wa shule Uhuru mchanganyiko.
Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi
Uhuru Mchangayiko, Anna Mshana akitoa maelezo kwa Mratibu Mkazi wa
Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo
(UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez (aliyeinama) na Mkuu wa Mahusiano wa
benki ya Standard Chartered Tanzania, Juanita Mramba (kulia)
walipotembelea darasa la awali la watoto wenye ulemavu wa macho (upofu)
katika shule hiyo. Nyuma ya Mwalimu Mkuu ni Mjumbe wa Kamati ya Shule ya
Msingi Uhuru Mchangayiko, Abubakar Mwambungu.
Mratibu Mkazi wa Mashirika ya
Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP) nchini,
Alvaro Rodriguez akicheza na mtoto Fatuma Haji wa darasa la awali katika
shule hiyo ambaye ni mlemavu wa macho alipotembelea darasa hilo kabla
ya kuzindua wa Malengo mapya ya Maendeleo Endelevu (SDG’s) hafla
iliyoandaliwa na Benki ya Standard Chartered Tanzania kwa kushirikiana
na Umoja wa Mataifa katika shule ya msingi Uhuru Mchanganyiko jijini Dar
mwishoni mwa wiki.
Mwakilishi wa Mkurugenzi wa Benki
ya Standard Chartered Tanzania, Charles Katongole, Mratibu Mkazi wa
Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo
(UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez, Mkuu wa Mahusiano wa benki ya Standard
Chartered Tanzania, Juanita Mramba pamoja na ujumbe wao katika nyuso za
masikitiko walipotembelea darasa la watoto wenye ulamavu wa macho
(vipofu) na matatizo ya kutosikia (viziwi) katika shule ya msingi Uhuru
mchanganyiko.
Mwakilishi wa Mkurugenzi wa Benki
ya Standard Chartered Tanzania, Charles Katongole, Mratibu Mkazi wa
Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo
(UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez, Mkuu wa Mahusiano wa benki ya Standard
Chartered Tanzania, Juanita Mramba na ujumbe wao katika picha ya pamoja
na wanafunzi ambao ni walemavu wa macho ambao pia ni viziwi katika shule
ya msingi Uhuru mchanganyiko.
Walimu wa darasa la watoto wenye ulemavu wa macho ambao ni viziwi wakicheza ngoma na wanafunzi wao.
Maana ya ulemavu wa macho na kuwa kiziwi.
Mkutubi wa maktaba ya shule ya
Uhuru mchanganyiko, Masanja akitoa maelezo ya namna mashine za kukuzia
maandishi kwa wale wanafunzi wenye uono hafifu katika shule hiyo kwa
Mwakilishi wa Mkurugenzi wa Benki ya Standard Chartered Tanzania,
Charles Katongole (kushoto) na Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa
Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP) nchini, Alvaro
Rodriguez walipotembelea maktaba hiyo.
Mratibu Mkazi wa Mashirika ya
Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP) nchini,
Alvaro Rodriguez akipitia Katiba maalum kwa watu wenye ulemavu wa macho
iliyopo kwenye maktaba ya shule hiyo. Kushoto kwake ni Mwakilishi wa
Mkurugenzi wa Benki ya Standard Chartered Tanzania, Charles Katongole.
Mratibu Mkazi wa Mashirika ya
Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP) nchini,
Alvaro Rodriguez na Ujumbe wa Benki ya Standard Chartered Tanzania
ulioongozwa na Mwakilishi wa Mkurugenzi wa Benki ya Standard Chartered
Tanzania, Charles Katongole wakitembelea mambweni ya wanafunzi katika
shule ya msingi Uhuru Mchanganyiko.
Mwakilishi wa Mkurugenzi wa Benki
ya Standard Chartered Tanzania, Charles Katongole, Mratibu Mkazi wa
Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo
(UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez pamoja na baadhi ya wafanyakazi wa Benki
ya Standard Chartered Tanzania katika picha ya pamoja na baadhi ya
wanafunzi wa shule ya Msingi Uhuru Mchanganyiko.
Mwakilishi wa Mkurugenzi wa Benki
ya Standard Chartered Tanzania, Charles Katongole (kulia) na Mratibu
Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la
Maendeleo (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez katika picha ya pamoja na
wanafunzi wa shule ya msingi Uhuru mchanganyiko Issa Abasi Wenge w
darasa la pili (wa pili kushoto) mlemavu wa ngozi na Fatuma Haji (wa
pili kulia) wa shule ya awali mwenye ulemavu wa macho.
Mwakilishi wa Mkurugenzi wa Benki
ya Standard Chartered Tanzania, Charles Katongole (kulia) na Mratibu
Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la
Maendeleo (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez na Mwanafunzi Mariana Alex
(Mariana the voice of the SDGs in TZ) wa darasa la tano katika shule ya
msingi Uhuru mchanganyiko jijini Dar. #TELLEVERYONE about the #GlobalGoals
Mtaalam wa Mahusiano na
Mawasiliano wa Umoja wa Mataifa (UN) Tanzania Hoyce Temu akiserebuka na
baadhi ya wanafunzi wa shule ya Uhuru mchangayiko.
Bango lililoorodhesha Malengo 17 mapya ya Maendeleo Endelevu (SDG’s).
Siku ilimazika kwa mechi ya
kirafiki baina ya Shule ya msingi Uhuru mchanganyiko na wafanyakazi wa
Benki ya Standard Chartered Tanzania katika viwanja vya shule ya
sekondari Benjamin Mkapa ambayo ilizinduliwa na Mwakilishi wa Mkurugenzi
wa Benki ya Standard Chartered Tanzania, Charles Katongole (kulia) na
Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika
la Maendeleo (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni