Mgombea urais wa Tanzania kupitia CCM, Dk John Magufuli akijinadi 
 kwa wananchi huku akishangiliwa aliposimama kusalimia katika Mji wa 
Nyakanazi, wilayani Biharamulo, Mkoa wa Kagera leo. PICHA ZOTE NA 
RICHARD MWAIKENDA;KAMANDA WA MATUKIO BLOG
 Wakazi wa Wilaya ya Kakonko mkoani Kigoma wakati wa mkutano wa kampeni
 Wananchi wakishangilia baada ya kufurahishwa na hotuba za Dk Magufuli wilayani Kakonko, Kigoma
 Dk Magufuli akimkabidhi Ilani ya Uchaguzi Mgombea ubunge jimbo la 
Kakonko, Christopher Chizza wakati wa mkutano wa kampeni wilayani 
Kakonko, Kigoma.
 Vijana wakisikiliza kwa makini wakati huku wakiwa juu ya baiskeli wakati Dk Magufuli akijinadi  wilayani Kakonko
 Dk Magufuli akiwafariji ndugu wa aliyekuwa mwalimu wake wa darasa la
 kwanza marehemu Cornel Pastory alipozuru kaburi la mwalimu huyo 
wilayani Biaharamulo
 Dk Magufuli akiwafariji ndugu wa aliyekuwa mwalimu wake wa darasa la kwanza marehemu, Cornel Pastrory  alipkwenda kuzuru kaburi
 Mwalimu Cornel Pastory enzi za uhai wake
 Dk Magufuli akiweka shada la maua kwenye kaburi la aliyekuwa mwalimu wake wa darasa la kwanza marehemu, Cornel Pastory
 Dk Magufuli akiomba alipozuru kaburi la aliyekuwa mwalimu wake wa 
darasa la kwanza marehemu Pastory wilayani Biharamulo, Kagera.
 Wananchi wakishangilia baada ya kufurahishwa na hotuba ya Dk Magufuli wakati wa mkutano wa  kampeni mjini Biharamulo leo
 Mgombea ubunge Jimbo la Muleba Kusini kupitia CCM, Profesa Anna 
Tibaijuka (kulia) akiwa miongoni mwa walioshiriki katika mkutano wa 
kampeni za CCM mjini Biharamulo
 Wananchi wakishangilia wakati Dk Magufuli akifanya kampeni mjini Biharamulo
 Dk Magufuli akijinadi kwa wananchi mjini ili wampigie kura katika Uchaguzi Mkuu Oktoba 25 Biharamulo
 Ni furaha iliyoje kwa wakazi wa  Bi9aharamulo baada ya kumuona Dk Magufuli wakati wa kampeni mjini humo leo
 Dk Magufuli akimnadi Mgombea ubunge Jimbo la Biharamulo, Oscar Mkassawakati wa kampeni hizo leo
 Dk Magufuli akimnadi mgombea ubunge Jimbo la Chato,Meedard Karemani 
katika Kata ya Igalula  wilayani Chato ambaye ndiye mrithi wake katika 
nafasi hiyo
 Ulinzi ukiwa umeimarishwa nyumbani kwa Dk Magufuli, mjini Chato
 Sura zikionesha matarajio makubwa  baada ya kumuona Dk Magufuli 
alipowasili katika Kata ya Igalula alipozungumza nao na kupata wasaa 
kuwaaga wananchi wa Jimbo la Chato baada ya kufanikiwa kupata nafasi ya 
kugombea urais wa T anzania.
 Sehemu ya wananchi wa Chato wakimlaki Dk Magufuli
 Ulinzi ukiwa umeimarishwa baada ya Dk Magufuli kuwasili nyumbani 
kwake Chato baada ya kufanya kampeni katika Wilaya ya Biaharamulo, 
Kagera.
 Dk Magufuli akiagana na Mkuu wa Mkoa wa Geita, Fatma Mwassa
 Dk Magufuli akisalimiana na ndugu zake akiwemo mamake mzazi 
(katikati) alipowasili nyumbani kwao Chato baada ya safari ndefu ya 
kufanya kampeni katika mikoa 13 nchini.
Dk Magufuli akisalimiana na ndugu nyumbani kwake Chato
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni