WAZIRI AWAASA VIJANA KUPAMBANA


Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Airtel Beatrice Singano Mallya akiongea
wakati wa uzinduzi iliyofanyika katika viwanja vya karume jijini Dar
es Saalam.
 Naibu katibu mkuu wa wizara ya habari vijana utamaduni na michezo Prof
Elisante Ole Gabriel akiongea wakati wa uzinduzi wa michuano ya Airtel
 Rising Stars katika ngazi ya taifa
 Mwanamuziki wa Hip Hop Nay Wa Mitego akitumbuiza wakati wa ufunguzi wamashindano ya Airtel Rising Stars ngazi ya Taifa katika Uwanja wa
Karume jijini Dar es Salaam.

WAZIRI wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dr. Fenella Mukangara
amewaasa vijana wanaoshiriki michuano ya Airtel Rising Stars kwa
vijana chini ya miaka 17, kupambana kwa bidii ili kufanikisha malengo
yao.
Dr. Mukangara alisema hayo wakati wa ufunguzi wa michuano hiyo katika
uwanja wa Kumbukumbu ya Karume jijini Dar es Salaam Jumapili
iliyopita.


Akizungumza kwa niaba ya Waziri Mukangara,  Naibu Katibu Mkuu wa
Wizara hiyo, Profesa Elisante Ole Gabriel, alisema kuwa Dr. Mukangara
amemimina pongezi za dhati kwa kampuni ya Airtel hapa nchini kwa
kuendelea kutoa sapoti kwa maendeleo ya soka hapa nchini ili
kuitangaza Tanzania kimataifa.


“Angalieni timu ya taifa ya wasichana- Twiga Stars. Kuna wachezaji
wengi sana ambao wametokana na michuano hii” , alisema huku akilitaka
Shirikisho la Soka nchini (TFF) na wadau wengine kutumia michuano hii
kutafuta vipaji vipya kwa maendeleo ya soka hapa nchini.


Alisema kuwa kwa kuweka msisitizo mkubwa kwenye soka la vijana,
Tanzania itakuja kuwa moja ya nchi zenye nguvu kubwa katika soka.
“Mataifa yote yenye nguvu katika soka duniani, yamefanikiwa kutokana
na programu hizi”, alisema.


“Kiwango chetu cha soka kitakapoimarika, tutakuwa na fursa nzuri sana
ya kujitangaza kimataifa hasa vivutio vyetu kama vile Mlima
Kilimanjaro ambao ndio mrefu kuliko yote duniani na hifadhi zetu za
taifa. Hii itafanya watalii wengi kuja hapa nchini hivyo kuongeza pato
la taifa”, alisema


Pia aliwashauri vijana kuongeza juhudi zaidi kwani mchezo wa soka kwa
sasa umekuwa ni moja ni sekta rasmi ambayo inatoa ajira  kwa kiasi
kikubwa, hivyo juhudi zao ndio msingi wa mafanikio yao na familia zao.


Akizungumza katika hafla hiyo hiyo, Mkurugenzi wa Mawasiliano wa
Airtel nchini, Beatrice Singano Mallya, alisisitiza kampuni yake
kuendelea kudhamini michuano hiyo huku akionesha kuridhishwa na jinsi
Wizara husika, TFF na wadau wengine wanavyotoa sapoti kubwa sana kwa
kampuni hiyo. “Tunajivunia sana mafanikio yaliyopatikana kupitia
michuano hii na tunaahidi kuendelea kutoa sapoti kama ambavyo tumekuwa
tukifanya”.

 alisema
Kwa upande wake, makamu wa rasi wa TFF Wallace Karia aliwashukuru
Airtel na kuyaomba makampuni mengine kuiga mfano huu.
Sherehe za ufunguzi zilitanguliwa na michezo miwili, ambapo
wenyeji-timu ya wasichana ya Temeke iliwatungua bila huruma Arusha kwa
magoli 8-0, kabla ya hapo baadaye Mwanza kuifunga Kinondoni kwa bao
1-0, mchezo ambao ulichezwa katika uwanja huo huo wa Karume.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni