Balozi
Tuvako Manongi akizungumza wakati wa Majadiliano ya Baraza Kuu la Umoja
wa Mataifa kuhusu dhana ya kuwalinda raia (R2P) majadiliano
yaliyojielekeza katika kutathimini mafanikio na changamoto za utekelezi
wa dhana hiyo ikiwa ni miaka kumi tangu kuasisiwa kwake.
Katibu
Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki Moon, akizungumza wakati wa Mkutano
wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa kuhusu dhana ya wajibu wa kuwalinda
raia, ambapo alisema licha ya kuasisiwa kwa dhana hiyo dunia bado
imeendelea kushuhudia maisha ya watu wasiokuwa na hatia yakiendelea
kupotea kwa sababu tu Jumuiya ya Kimataifa inashindwa kutumiza wajibu
wake kwa wakati.
Wakimbizi katika kambi moja nchini Tanzania, ambao jana jumanne
akizungumza katika Mkutano wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa,
Mwakilishi wa Kudumu wa Tanzania katika UN Balozi Tuvako Manongi amesema
kutoka na wimbi kubwa linaloendelea la wakimbizi kukimbilia mataifa
mengine kutafuta usalama wao. Jumuiya ya kimataifa haina budi
kushirikiana na bila kubagua katika kuwalinda na utoaji wa huduma na
misaada ya kibinadamu kwa wakimbizi
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni