Afisa
vijana kutoka Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Bw.Godfrey Massawe
akizungumza na wawezeshaji wa Kitaifa wa Stadi za Maisha kutoka Mikoa ya Kanda
ya Ziwa kabla ya kufunga mafunzo ya wawezeshaji hao leo Jijini Mwanza.
Kaimu Katibu Tawala Mkoa wa Mwanza Bibi. Susan Ndunguru akizungumza na
Wawezeshaji wa Kitaifa wa Stadi za Maisha (hawapo pichani) kabla ya kufunga
Mafunzo ya siku nane ya Uwezeshaji kwa wawezeshaji hao leo Jijini Mwanza. Kushoto
ni Afisa Vijana Bw. Godfrey Massawe na kulia ni Mwezeshaji Kitaifa Bibi.
Octavina Kiwone
Kaimu Katibu Tawala Mkoa wa Mwanza Bibi. Susan Ndunguru akitoa cheti cha kuhitimu Mafunzo ya
Uwezeshaji wa Stadi za Maisha kwa Bw.
Edwin Gacho (kushoto) wakati wa kufunga Mafunzo hayo leo Jijini Mwanza
Afisa Vijana kutoka Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Bibi. Diana
Kasonga (kushoto) akifuatilia Wawezeshaji wa Kitaifa wa Stadi za Maisha kutoka
Mkoa wa Kagera wakiandaa Mpango kazi watakaotumia wakati wa kufikisha ujuzi walioupata
kwa waelimisha rika wa Mkoa wa Kagera.
Mwezeshaji wa Kitaifa wa Stadi za Maisha Bi. Virginia Chacha (kulia) akifanya
mazoezi ya uwezeshaji kwa wawezeshaji wenzake kama njia mojawapo ya kupima
uwezo wa wawezeshaji hao kabla ya kufunga Mafunzo ya Uwezeshaji leo Jijini
Mwanza
Kaimu Katibu Tawala Mkoa wa Mwanza Bibi. Susan Ndunguru (wapili kushoto waliokaa)
katika picha ya pamoja na Wawezeshaji wa Kitaifa wa Stadi za Maisha baada ya
kufunga mafunzo ya uwezeshaji leo Jijini Mwanza. Wapili kulia ni Mtaalam wa
Stadi za Maisha Bw. Benny Lugoe na wakwanza kulia ni Afisa Vijana Bw. Godfrey
Massawe.
Picha
na:
Genofeva Matemu – Maelezo, Mwanza
Na:
Genofeva Matemu - Maelezo, Mwanza
Vijana wametakiwa
kutumia vizuri mazingira wanayowazunguka kuibua mbinu mbalimbali za
ujasiriamali ili kuweza kuondoka na taifa tegemezi kwa kusubiri kuajiriwa mara
baada ya kuhitimu masomo yao.
Rai hiyo imetolewa na
Kaimu Katibu Tawala Mkoa wa Mwanza Bibi. Susan Ndunguru alipokua akifunga
mafunzo ya Wawezeshaji wa Kitaifa wa Stadi za Maisha leo Jijini Mwanza.
Bibi. Ndunguru
amesema kuwa vijana waliopata mafunzo ya uwezeshaji wa stadi za maisha ni
mabalozi ambao kama watatumia vizuri uwezo walioupata katika mafunzo hayo
watabadili fikra za vijana wengi nchini hivyo kuweza kujenga taifa lenye afya
nzuri, weledi na pamoja na ujuzi.
Kwa upande wake Mtaalamu
wa masuala ya Stadi za Maisha Bw. Benny Lugoe amesema kuwa washiriki wa Mafunzo ya Stadi za Maisha wana
ari na motisha ya kujifunza na kama wataendelea kuwa na ari hiyo watakua
wabunifu na wawezeshaji wazuri kwa vijana ndani ya jamii.
Aidha Bw. Lugoe amewataka wahitimu wa kitaifa wa
Stadi za Maisha kutimiza wajibu wao kwa kuwaandaa waelimisha rika katika mikoa
yao ili kuweza kutimiza malengo yaliyokusudiwa na kuweze kubadili fikra za
vijana katika jamii.
Naye Mwezeshaji wa
Kitaifa wa Stadi za Maisha kutoka Mkoa wa Shinyanga Bw. Ezra Manjerenga amesema
kuwa ukosefu wa elimu ya afya ya uzazi kwa vijana ni tatizo kubwa kwa Mkoa wa
Shinyanga hivyo ugeni wa mafunzo ya stadi za maisha katika Mkoa huo utawavutia
vijana wengi jambo ambalo litapelekea kutimiza lengo la serikali kufikisha
mafunzo hayo kwa vijana wa rika mbalimbali.
Bw. Manjerenga
ameiomba serikali kutoa mafunzo ya mara kwa mara kwa wawezeshaji wa kitaifa wa
Stadi za Maisha haswa pale panapokua na mabadiliko katika mwongozo wa Stadi za
maisha ili kuweza kubadilisha fikra za vijana wote nchini.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni