WANAFUNZI WATAKIWA KUWEKEZA KWENYE ELIMU

Na Woinde Shizza,Arusha
Wanafunzi wametakiwa kuwekeza katika elimu, kwani elimu ndio ufunguo wa maisha ya sasa na ya baadaye ikiwemo kufanya kazi kwa vitendo ,na mashiko vitavyowasaidia kwenye maisha yao ya sasa na baadae sanjari na kulijenga taifa lao.

Hayo yamesemwa na Mkuu wa utawala na uongozi wa chuo cha Habari maalum,Mr Ernest Karata wakati wa mahafali ya kwanza ya chuo cha Full Bright college kilichopo Ngaramtoni,wilaya ya Arumeru mkoani Arusha. 


Katika mahafali hayo wanafunzi  wanane walihitimu mafunzo ya ukatibu muhtasi ualimu wa shule za awali (chekechea) ambapo wote watapata ajira katika shule na vyuo mbalimbali vilivyopo ndani na nje ya nchi.


Awali akimkaribisha mgeni rasmi mkurugenzi mtendaji  wa chuo cha Full Bright College  Mr.Julius Matiko amewaasa wahitimu wajiongeze na wazidisshe bidii katika elimukwani chuo hicho kina vifaa vya kutosha vikiwemo vifaa vya kompyuta,uhazini ambavyo vipo na hotel management
.Chuo hicho kimesajiliwa na VETA ambapo pia wanatoa mafunzo ya NABE(National
Business Examination)

Mku wa chuo hicho Rose Mapunda  amewasihi na kuwashauri wazazi wawalete wanafunzi chuoni hapo wajipatie elimu na maarifa ya kutosha  zikiwemo stadi za kazi mbalimbali iliwatakapotoka chuoni hapo waweze kupata ajira na kujiajiri.

.
Mkurugenzi wa chuo hicho cha Full Bright Mr .Julius Matiko ameiomba serikali itoe ruzuku kwa vyuo binafsi ikiwezekana itoe usafiri pamoja na kutoa vifafa mbalimbali vya kujifunzia  na kujisomea katika chuo hicho.


Akitaja Changamoto zinazokabili chuo hicho ni uhaba wa ardhi ,wa kujenga nyumba za walimu nyumba za kulala wanafunzi, maktaba za kujifunzia  na viwanja vya michezo kwa wanafunzi  na wahitimu wa chuo hicho cha Full Bright College

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni