Mshereheshaji wa mkutano huo Prof. Venant Nantulya akiwa katika hatua ya uendeshaji wa mkutano wa Viongozi wa ngazi ya juu wa dini katika kupambana na kuweka mikakati ya
kuharakisha kumalizama ambukizi mapya ya VVU/UKIMWI.Picha na Geofrey Adroph
Mufti
mkuu wa Zambia, Sheikh Assadullah Mwale akifungua kwa dua katika mkutano
wa viongozi wa dini wa nchi za mashariki na kusini mwa Afrika
uliofanyika leo jijini Dar.
Bi.
Vanessa Anyoti kutoka YWCA Tanzania(kushoto) akizungumza kuhusiana
masuala ya kijinsia pamoja na maendeleo ambayo yanaweza kupunguza
maabukuzi ya virusi vya UKIMWI. Kulia ni
Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi naUtamaduni (UNESCO), Bi. Zulmira Rodrigues
Mwenyekiti
wa Mtandao wa Kimataifa wa viongozi wa dini waishio na VVU/UKIMWI na
waliyoathiriwa na UKIMWI (INERELA+) Mch. Mpumzile Mabizela akizungumza
na Viongozi wa ngazi ya juu wa dini na
wawakirishi wa dini kutoka nchi 17 za Mashariki na Kusini mwa
Afrikawakati wa mkutano ulioanza leo jijini Dar.
Mkurugenzi
Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi naUtamaduni
(UNESCO), Bi. Zulmira Rodrigues akisoma hotuba kwa Viongozi wa ngazi ya juu wa dini na wawakirishi wa dini waliofika kwenye mkutano uliofanyika jijini Dar es Salaam, Tanzania kujadili na kuweka mikakati ya kuharakisha kumalizama ambukizi mapya ya VVU/UKIMWI
Dk.Warren
Namara kutoka shirika la (UNAIDS) akielezea ni kwa njia gani viongozi
wa kidini wanaweza kuelimisha jamii inayowazunguka jinsi ya kupanbana na
kuepuka maambukizi mapya ya virusi vya UKIMWI.
Mwenyekitiwa Tume ya kudhibiti UKIMWI Tanzania (TACAIDS) Dk.
Fatma Mrisho akitoa wito kwa mashirika mbalimbali kujikita katika
utoaji wa elimu kuhusu maambukizi ya virusi vya UKIMWI huku
wakishirikiana na Viongozi wa ngazi ya juu wa dini.
Baadhi ya Viongozi
wa ngazi ya juu wa dini na wawakirishi wa dini kutoka nchi 17 za
Mashariki na Kusini mwa Afrika wakiwa kwenye mkutano huo utakaodumu kwa
takribani siku tatu.
Picha ya Pamoja Kwa washiriki walio hudhuria mkutano huo.
Na Mwandishi wetu
Viongozi wa ngazi ya juu wa dini na wawakirishi wa dini kutoka nchi
17 za Mashariki na Kusini mwa Afrika wakutana Dar es Salaam, Tanzania
kujadili na kuweka mikakati ya kuharakisha kumalizama ambukizi mapya ya VVU/UKIMWI
Shirika la Umoja wa Mataifa laElimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) kwa kushirikiana
na Mtandao wa kimataifa waViongozi wa dini
wanaoishi ua waliyoathiriwa na virusi
vya UKIMWI (INERELA+) pamoja na shirika la umoja wa mataifa linaloshughulikia masuala
ya UKIMWI (UNAIDS) waandaa mkutano wa siku tatu wa kimataifa kujadili ushiriki wa taasisi na viongozi wa dini katika kukabiliana na maambukizi
mapya ya VVU/UKIMWI.
Mkutano huo
ulioanza leo tarehe 02/09/2015 unafanyika katika hotel yaKunduchi, Dar es
Salaam, Tanzania na unaohudhuliwa na zaidi ya viongozi 50 wangazi ya juu wa dini
na wawakirishi wamtandao wa INERELA kutoka nchi 17 za Mashariki naKusini mwa
Afrika ikiwemo Tanzania. Wengine wanaohudhuria mkutano huo ni wawakirishi wa makundi
ya vijana; wawakilishi wa mashirika ya umoja wa mataifa na wawakilishi wataasisi
za serikali ikiwemoTume ya Taifa ya Kudhibiti UKIMWI Tanzania na UNESCO
Tanzania).
Katika mkutano
huo Mwenyekiti wa Mtandao wa Kimataifa wa viongozi wa dini waishio na VVU/UKIMWI
na waliyoathiriwa na UKIMWI (INERELA+) Mch. Mpumzile Mabizela ameeleza umuhimu wakiongozi
wa dini na namna kiongozi wa dini anavyoweza kushiri kikatika kutoa elimu kuhusu
maambukizi ya ukimwi, matumizi sahihi ya dawa zakupunguza makali ya VVU,
Unyanyapaa na namna watu wanavyoweza kujikinga na maambukizi kupitia semina mbalimbali
zinazokuwa zikiendelea katika miskiti na madhehebu mbalimbali
Kwa upande
wake Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi naUtamaduni
(UNESCO), Bi. Zulmira Rodrigues amewataka viongozi wa dini kujikita katika jamii
kwa ajiri ya kutoa elimu inayohusu virusi vya UKIMWI hususani kwa vijana na jamii
iliyopo vijijini. Aliongeza kuwa kutokana na sababu za kiutamaduni na mira wazazi
wengi wanashindwa kuongea na watoto juu ya masuala ya jinsia, barehe na mahusiano
hii inachangia vijana wengi kukosa elimu sahihi juu ya miili yao hususani afya ya
uzazi na kujikuta wanapatamatatizo ikiwemo mimba za utotoni na maambukizi ya
VVU. Akisistiza umuhimu wa viongozi wa dini katika mapambano dhidi ya UKIMWI
naMimba za utotoni, Bi Zulmira aliwataka viongozi hao kushirikiki kamirifu katika
kutoa elimu sahihi na kujiepusha na ushauri utakao wasaidia waamini na vijana “wakati
dunia inategemea mchango wenu katika kuhakikisha watu wanazingatia matumizi sahihi
ya dawa, baadhi yenu mmekuwa mkitoa elimu zinazochangia watukuacha matumizi ya dawa
na hatimaye kuathiri kinga zao za mwili”alisema. Ms. Zulmira aligusia suala la
unyanyapaa na namna viongozi wa dini wanavyoweza kusaidia kupunguza“msiwatenge na
kuwanyanyapaa watu wanaoishi na virusi vya ukimwi kwani wanahitaji elimu zaidi ili
waweze kuwa katika hali ya kawaida nasi ya kiunyonge”alisema.
Naye Mwenyekitiwa Tume ya kudhibiti UKIMWI Tanzania(TACAIDS) Dk. Fatma Mrisho alitoawito
kwa mashirika mbalimbali kusaidiana na viongozi wa kidini katika kuhakikisha watu
wana hamasikana kupima afya zao kila wakati na kusambaza elimu inayohusu maambukizi
ya virusi vya UKIMWI kwa maeneo mbalimbali na pia awaasa vijana ambao bado ni wadogo
kutokujiingiza katika ulimwengu wa ndoa kwani vitendo hivyo vinachangia kwa kasi
maambukizi mapya ya VVU.
Kwa
upande
wake Dk.Warren Namara kutoka shirika la (UNAIDS) aliongeza kuwa
viongozi wa dini ni viongozi waaminifu waadilifu na ni waelimishaji.
Kulingana na huduma yao ya kukutana na waumini kila wiki wana nafasi
nzuri na pia
ni rahisi sana kuweza kuwafikishia ujumbe na kuwaamasisha wananchi
katika maeneo
yao kwa kutoa elimu ya virusi vya UKIMWI. Dk Warren alisisitiza haki ya
kila mtu
kupata elimu sahihi na kuwataka viongozi wa dini kutowatenga watu hasa
waliyokwenye
hatari zaidi ya kupata maambukizi mfano watu wanaotumia madawa ya
kulevya na watu
wanaofanya biashara ya kuuza miili yao.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni