Na Ahmed Mahmoud Arusha
SERIKALI imeridhishwa na utekekezaji wa miradi miwili ya maendeleo ya
ujenzi wa Jengo la ghorofa kumi la nyumba za kuishii watumushi wa
serikali lililopo mkabala na jengo la Uhamiaji mkoa pamoja na
uboreshaji wa uwanja wa ndege wa Arusha..
Naibu waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Mwita Waitara, ameyasema hayo
ilipohitimisha ziara yake ya siku moja ya kutembelea miradi
hiyo,iliyotanguliwa na Waziri huyo kufanya kikao na watumishi wa
serikali kwenye ukumbi wa benki kuu.
Kwenye mradi wa ujenzi wa Jengo la ghorofa kumi linalomilikiwa na
linalijengwa na wakala wa majengo nchini TBA,Waitara,ameipongeza
wakala huyo na kuagiza kuwa kipaumbele cha watu watakao ishi ndani ya
jengo hilo iwe ni watumishi wa serikali.
Alisema kukamilika kwa ujenzi wa Jengo hilo kutaongeza mapato ya
serikali na uhitaji wa majengo ya kuishi watumushi ni mkubwa mno hivyo
Jengo hilo litaiwezesha TBA,kujiendesha kibiashara .
Alisema wizara imeshaagiza wastaafu ikiwemo wabunge waliomaliza muda
wao kuondoka kwenye nyumbaza serikali zilizopo Dodoma ili kuwezesha
watumishi wengine kupata nyumba za kuishi.
Akiwa kwenye uwanja wa ndege wa Arusha,Waziri Waitara,ameridhishwa na
hatua za uboreshaji wa uwanja huo uliofanywa na mamlaka ya viwanja vya
ndege nchini,na kusema kuwa serikali Imetoa fedha nyingi kwa ajilj ya
miradi hiyo.
Alisema kukamilika kwa ukarabati huo unahusisha kuongeza Urefu wa
uwanja eneo la kurukia ndege kutaongeza ndege nyingi kutua uwanjani
hapo na mapato nayo yataongezeka.kwani uwanja huo ni rafiki kwa
watalii na wananchi wa mkoa wa Arusha
Alisema jumla ya viwanja kumi na moja nchini vitafanyiwa marekebisho
na uboreshaji katika bajeti ya mwaka huu na serikali sasa inafungua
njia za uchumi kwa kuimarisha miundo mbinu ya barabara,reli,ndege na
Mali kwa wizara hiyo ni wezeshi kufikia malengo ya kiuchumi.
Kwa upande wake meneja wa uwanja wa ndege wa Arusha,Mhandisi Eliud
Tesha,alisema mradi wa ukarabati na maboresho ya uwanja huo
yanahusisha eneo la maegesho ya ndege na kuruka ,maegesho ya
magari,eneo la kurukia ndege na miradi hiyo iliyotekelezwa ambayo
imekamilika mwaka jana.
Ameongeza kwamba mamlaka ya viwanja vya ndege nchini ina mpango wa
kujenga jengo lingine la kisasa uwanjani hapo.la kufikia wageni kwa
lengo la kuendelea kuongeza wigo mpana kwa abiria wanaofika kusafiri
ndani ya uwanja huo.