Na Ahmed Mahmoud Watanzania wametakiwa kuzalisha bidhaa za Kilimo zinazoendana
na masoko ya kimataifa ili kuweza kujingezea kipato na kukamata masoko hayo ya
kimataifa Aidha Waziri wa Kilimo Husein Bashe anatarajiwa kuwa mgeni Rasmi
katika maonesho ya kimataifa ya kilimo TanzFood Expro 2022 yenye kibwagiz mbiu
Ladha ya Tanzania. Akizungumza na waandishi wa habari katika makao makuu ya EAC
Jijini Arusha Mkurugenzi wa sekta ya uzalishaji ndani ya Jumuiya ya Afrika
masharika Jean Baptiste amesema maonyesho hayo yatafanyika kwa siku tatu kuanzia
tarehe 11 hadi 13. Amesema kwa siku tatu watatumia kujenga mtandao wa kibiashara
katika mazingira ya kitaalamu na kwamba sekta hii ya kilimo sio kwa ajili ya
Tanzania Pekee ndio maana kama Eac na KiliFair Promotion tumeungana ili nchi
wanachama wa jumuiya ya Afrika mashariki tutoke na bidhaa zilizo bora. "Bidhaa
bora zinahitajika sana ili kuweza kutangaza katika maonyesho haya kutoka kote
katika jumuiya itasaidia kuongeza tija ya kuzalisha bidhaa zenye ubora wa
kimataifa". Awali Mkrugenzi wa Kilifair Dominic Shoo Alisema kuwa maonesho ya
kilimo TanzFood pia yatazinduliwa na Balozi wa Ujerumani nchini Regine Hess na
Waziri wa Kilimo Husein Bashe na kuyaleta pamoja makampuni 120 ya hapa nchini na
nchi za Eac. Alisema kuwa wanayofuraha kuona waonyeshaji wa ndani na nje ya nchi
kutoka masoko mengine kuja kuangalia bidhaa zetu huku akiyataka makampuni ya
mbegu na Mashine za kilimo kuleta bidhaa zao katika maonyesho. Kwa Upande wake
Mkurugenzi Mwenza wa Kilifair Tom Kunkler alisema kuwa maonesho hayo washiriki
watapata fursa ya kupata mafunzo ya kilimo na uzalishaji wa bidhaa ili waweze
kushindana katika soko la kimataifa. Alisema kuwa mafunzo hayo kwa wakulima
yatawasaidia kuongeza ubora na maendeleo katika sekta ya kilimo ambapo kauli
mbiu yake ni Ladha ya Tanzania.
Jisajili kwenye:
Machapisho (Atom)