Prisca Libaga Maelezo ArushaI
Imeelezwa kwamba changamoto za ushirikiano kati ya taasisi za kifedha na serikali zinawafanya wabunifu kutofikia malengo ya kuongeza uzalishaji na kutofikiwa kwa Masoko.
Akiongea na Wanahabari watafiti na wabunifu wa kanda ya kaskazini waliopatiwa mafunzo na Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH)Mkurugenzi wa Imara Tecknoloji Alfed Changula ambao wamebuni mashine ya kupukuchulia mazao ya nafaka.
Anasema kwamba Imara Tecknoloji inajishughulisha na utengenezaji wa mashine za kilimo wamebuni kutengeneza kwaajili ya kuwauzia wakulima ambapo Imara Tech ilianza Mwaka 2019 na uzalishaji rasmi ulianza Mwaka 2020.
Taasisi hiyo imeweza kuzalisha Ajira 37,Saba za moja kwa moja na 30 vibarua hadi Sasa na mawakala 15 ambao wanauza mashine hizo maeneo mbalimbali kanda ya kaskazini Lengo likiwa ni kufikia kanda zote nchini kwa Uzalishaji wa mashine mbalimbali ikiwemo ya kupukuchulia mazao ya nafaka na mashine nyingine.
Anaeleza kwamba Imara Tech,imekuwa na mafanikio kwa kuuza mashine 400 na kuwafikia wakulima 400 katika maeneo mbalimbali ambapo wanazalisha Ajira kadhaa kwa maeneo waliouza bidhaa hizo
Anabainisha kwamba hadi Sasa bado wanakumbana na changamoto kadha wa kadha ikiwemo ya ugumu wa kuwafikia viongozi wa serikali kuweza kujitangaza kusogeza Maarifa na uelewa sanjari na kutatua baadhi ya changamoto wanazokutana nazo.
Changula Anabainisha baadhi ya changamoto hizo ni ushirikiano mdogo kutoka serikalini na taasisi za kifedha,ruzuku kwa wakulima itakayosaidia kununua mashine ,ongezeko la mara kwa mara kwa bei za bati ambazo zinazalishia mashine hizo.
Aidha anasema kwamba wamekuwa wakikumbana na changamoto kadhaa ikiwemo ushirikiano na taasisi za kifedha kushindwa kuwasaidia wakulima mikopo pindi wanapohitaji mashine hizo.ilhali wao hawakopeshi kutokana na gharama kubwa kwa za vifaa na bidhaa ikiwemo upandaji wa bei za bati mara kwa mara.
"Utakuta wateja wanahitaji mashine hizo ambazo zimewasaidia vijana kuzalisha ajira kwa kujiajiri kwa kufunga kwenye bodaboda Sasa sisi tunaposhindwa kuwakopesha inakuwa changamoto ambapo tunapoongea na taasisi za kifedha bado hawapo teyari kuwadhamini"
Kwa mujibu wa Chengula Wanufaika wa ufadhili wa fedha za Utafiti na Ubunifu katika Sayansi na Teknolojia wameeleza kunufaika na ufadhili huo kutoka Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH) Ilizowasaidia kuongeza ufanisi katika maeneo hayo ila wameomba ruzuku hizo kuongezwa ili kusaidia kuongeza uzalishaji.
Anasema kwamba katika fedha ya ruzuku kutoka COSTECH waneweza kununua mashine ya kukatia mabati na fedha nyingine kufanya Utafiti wa Masoko na kufanikiwa kuongeza uhitaji wa wakulima wanaotaka kununua mashine hizo.
Wanaiomba Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH) kuwasaidia kuongeza wigo mpana wa ruzuku sanjari na serikali kuwashika mkono kuweza kuzifikia ndoto zao na kuzishirikisha taasisi za kifedha kuwezesha wakulima kununua mashine hizo ambazo zimekuwa mkombozi kwa wakulima nchini.
"Teknolojia inaposambaa kwa haraka inabadilisha kilimo na kuongeza tija kwa wakulima mashine hizo zinaokoa upotevu wa mazao baada ya mavuno na kuyafanya yawe bora"
Hatahivyo Kituo cha kuhamilisha teknolojia ya zana za kilimo Vijijini, Camartec,kimekuwa ni nguzo ya kutengeneza zana za kilimo na kuziuza kwa wakulima ndani na nje ya nchi ili kurahisisha shughuli za kilimo.
Camartec,Imetoa teknolojia ya uzalishaji zana za kilimo na mashine mbalimbali kwa taasisi ya Imara tec,iliyowezesha kutengeza mashine mbalimbali na zana za kisasa ambazo zinatumika katika kilimo na kurahisisha uvunaji,kuongeza thamani ya mazao
Kutokana na kuwa ni kisima cha teknolojia Camartec,imeiwezesha kiufundi tasisi ya Imara Tech, kubuni, kusanifu na kutengeneza mashine hizo za kisasa ambazo zinarahisisha shughuli za kilimo na kuongezaji thamani ya mazao
Kupitia uwezeshaji huo kutoka Camartec,taasisi ya Imara Tec,imeweza kubuni ,kusanifu na kutengeneza mashine na zana zingine za kilimo na kupata masoko makubwa ya kuuza zana hizo katika nchi za Kenya, Uganda,Rwanda na Burundi