DC DAQARRO ATAKA WADAU WA ELIMU KUHAKIKISHA MPANGO WA LANES UNAENEA ARUSHA NA KULETA MATOKEO CHANYA

Mkuu wa wilaya Arusha mjini Gabriel Daqarro akifungua wiki ya usomaji iliyofanyika kwenye maktaba ya mkoa Arusha pembeni ni mkutubi mkuu wa maktaba hiyo Bi Rafiki Mvamba na kushoto ni Afisa elimu Vielelezo Godfrey Augustino wakifuatilia hotuba ya mgeni rasmi mkuu huyo wa wilaya picha zote na mahmoud ahmad arusha 

Afisa elimu Vielelezo Godfrey Augustino akitoa hotuba kwenye ufunguzi wa wiki ya usomaji Lanes kabla ya kumkaribusha mgeni rasmi mkuu wa wilaya ya Arusha Gabriel Daqarro picha na mahmoud ahmad arusha

Meza kuu wakiwa wanajadiliana mkuu wa wilaya na mkutubi mkuu wa maktaba bi Rafiki Mvamba ambapo afisa elimu akiendelea kutoa hotuba yake kabla ya kumkaribisha mgeni rasmi

Pichani juu na chini ni sehemu ya wanafunzi wa shule sita za wilaya ya Arusha walioshiriki mashindano mbali mbali ya kusoma kuandika na kuhesabu wanaoonekana pichani ni wanafunzi wa shule ya msingi Mwangaza na sombetini  wakifuatilia kwa makini matukio mbali mbali yalioendelea kwenye hafla hiyo


MAONYESHO YA VITABU MBALI MBALI NAYO YALIKUWEPO KWENYE WIKI YA USOMAJI KATIKA JIJI LA ARUSHA ILIYOADHIMISHWA KWENYE MAKTABA KUU YA MKOA WA ARUSHA

Mwanafunzi wa shule ya Msingi Uhuru Jaquline Abrogast akisoma kitabu mbele ya mkuu wa wilaya kwenye maadhimisho ya siku ya Usomaji iliyoadhimishwa kimkoa kwenye maktaba ya mkoa jijini Arusha


Picha juu ni igizo la wanafunzi wa shule ya msingi Naura wakionyesha masuala mbali mbali ya safari ya kusoma kwenye maonyesho ya wiki ya usomaji mbele ya mgeni rasmi mkuu wa wilaya ya Arusha

Wanafunzi wa shule ya msingi Arusha School wakiimba wimbo mbele ya mgeni rasmi mkuu wa wilaya ya Arusha

Mkutubi mkuu wa maktaba ya mkoa akiwa na majaji wenzake wakifuatilia mashindano ya kusoma kwa wanafunzi wa shule sita za Naura,Sombetini,Meru,Mwangaza,Uhuru na Arusha School

Baadhi ya wanafunzi wakioshiriki mashindano ya kusoma vitabu wa darasa la kwanza wa shule hizo sita zilizoshiriki maadhimisho hayo ya wiki ya Usomaji
Na Ahmed Mahmoud Arusha
Mkuu wa wilaya ya Arusha Gabriel Daqarro amewataka waalimu na Afisa elimu kuhakikisha mpango wa KKK (LANES) unatiliwa mkazo sanjari na kuhakikisha wanafunzi wanajua kusoma kuandika na kuhesabu ili kuleta matokeo chanya na kufikia malengo ya serikali ya wananchi wote kujua kusoma.
Akiongea wakati akifungua wiki ya kusoma na stadi za kukuza kusoma kuandika na kuhesabu (LANES) iliyofanyika katika Maktaba ya mkoa Dc Daqarro amesema kuwa wajibu huo ni wetu sote kuanzia nyumbani hadi mashuleni kuhakikisha kila moja wetu anatimiza wajibu wake.
Amesema kuwa wiki kama hiyo ni ya kujitathmini tumefika wapi na tunaelekea wapi kama taifa kwa ajili ya kukuza uelewa wa vijana wetu kujua kuhesabu kusoma na kuandika ili kuwa na taifa linalopiga hatua kwa wananchi wake kujua kusoma.
“Taifa limejipanga kuondoa  wananchi wasio jua kusoma na kuandika ndio maana ilikaja na mkakati wa kkk hivyo kila mmoja wetu anawajibu kuhakikisha tunafikia malengo ya mkakati huu”alisema Daqarro
Kwa Upande wake Afisa elimu vielelezo Godfrey Augustino amesema kuwa wajibu wa wazazi ni kufuatilia maendeleo ya watoto wao na wao kama waalimu watahakikisha kila kijana anayepata nafasi anajua kusoma kuandika na kuhesabu lengo ni kuondoa vijana wanaomaliza elimu wakiwa hawajui kusoma na kuandika.
Amesema kuwa hatavumilia kuona wilaya hiyo ikiwa ina vijana ambao hawajui kusoma wala kuandika na amejipanga kuhakikisha wanafikia malengo yalioanza kuonekana kwenye ufaulu kwa wilaya kushika nafasi ya kwanza kitaifa katika ufaulu wa Darasa la saba mwaka huu.
Awali mkutubi mkuu wa maktaba ya mkoa Rafiki Mvamba amesema kuwa analishukuru shirika Kwa kufadhili wiki hiyo na kuwataka watanzania kupenda kujisomea na kufuatilia watoto wao ili kujua kusoma na kuandika itakayopelekea taifa kuwa na wananchi wenye elimu ya kuweza kufikia malengo endelevu
Amesema kuwa mpango huo LANES wa wiki ya kusoma ni kujitathmini na kuwafikia wanafunzi kujua uelewa wao katika kukuza stadi za kusoma kuandika na kuhesabu kuanzia watoto wa awali hadi vyuo vikuu kupenda kujisomea kwani elimu haina mwisho.
“sisi kama maktaba tumejipanga kuhakikisha wanafunzi wote wanaofika hapa wanapata vitabu vyote wanavyohitaji sanjari na kuwapa nafasi na kuwaongoza pale wanapohitaji ili lengo ya kuwa na taifa lenye watu wanaojua kusoma na kuandika linafikiwa”alisema Mvamba
Mwisho………………


TCCIA LONGIDO SACCOS WAITAKA SERIKALI KUSIMAMIA SUALA LA ELIMU KWA VYAMA VYA USHIRIKA NCHINI

Afisa ushirika wilaya ya Longido Japhet Mambo akisisitiza jambo wakati akiongea na wanachama wa TCCIA Longido Saccos Ltd ambapo kushoto ni Mwenyekiti wa TCCIA wilaya hiyo Abduraman Konje akifuatalia mkutano huo na kulia ni Mshauri kutoka Shirika la Trias Julius Mlambo akifuattilia picha zote na mahmoud ahmad wa globu ya jamii Longido

Juu na chini ni sehemu ya wanachama wa saccos ya TCCIA wilayani Longido wakiwa katika mkutano wao wa mwaka wakifuatilia vipengele vya Agenda za mkutano huo picha na mahmoud ahamad longido


Meza kuu wakifuatilia mkutano huo kushoto ni makaumu wa mwenyekiti wa saccos hiyo akifuatiwa na mtendaji wa kata ya Namanga akifuatiwa na mwenyekiti wa Longido Saccos Abdulrahman Konje na Afisa Ushirika na mwisho kabisa ni mshauri wa vikundi kutoka shirika la TRIAS Julius Mambo

Vijana nao walikuwemo kama sehemu ya mkakati wa serikali kuweza kutengeneza uchumi wa kati wa viwanda vijana ndio nguvu kazi ya taifa lolote kufikia malengo kaama walivyokutwa na kamera ya matukio

Wanachama wakisoma taarifa za kikao hicho hatua kwa hatua katika mkutano huo

Mwenyekiti wa mkutano huo David Wiliam na makamu wake Adela Magani wakisikiliza taarifa ya mapato na matumizi ikisomwa

Wanachama hawakuwa nyuma kufuatilia hatua kwa hatua taarifa ya mapato ya chama chao


Wananchama juu na chini wakifuatilia kikao hicho ambapo waliibua mambo mengi ya kuweza kusaidia kukuza chama chao


Na Ahmed Mahmoud Longido
Vyama vya Ushirika nchini vimetakiwa Kutenga muda wa kutoa elimu kwa wananchama wao lengo likiwa kujua faida za vyama hivyo pamoja na kuweka akiba na kukopa ili kuweza kuwafikia wanachama wengi zaidi hapa nchini kukuza vipato vyao sanjari na kujiwekea akiba na hisa.
Akifungua mkutano mkuu wa mwaka na wa pili wa TCCIA Longido Saccos Mwenyekiti wa Tccia wilaya ya Longido Abrahaman Konje ameitaka serikali kutambua suala la elimu ya uwekaji akiba na uwekaji wa amana kwa watanzania suala ambalo wengi wao bado hawana elimu hiyo.
Amesema kuwa Tatizo hilo ndio maana vyama vingi vya ushirika vimekuwa vinaende kwa kusuasua jambo ambalo sio zuri na linaleta ukakasi kwa wanachama katika juhudi zao za kufikia kuwa na vyama vikubwa hapa nchini vitakavyosaidia maendeleo ya nchi na kuongeza vipato.
“Tatizo hapa nchini wanachama wengi hawana uelewa mkubwa wa masuala ya kujiwekea akiba na Amana(HISA) hivyo kujikuta wanashindwa kutofautisha vicoba na saccos kwa kushindwa kujiletea faida na kuendesha familia kwa kujiwekea amana ili kuweza kuweka na kuwasaidia kusomesha watoto wao na kujiendesha maisha”alisisitiza Konje.
Aidha Kwa Upande wake Afisa ushirika wilaya ya Longido Japhet Mambo amewataka wataalamu wenzake kuhakikisha wanatenga muda mwingi kuvifikia vikundi kwa ajili ya kutoa elimu ya vyama vya ushirikia kwani amegundua vyama vingi wanachama vijijini hawana uelewa hivyo sasa ni ndio muafaka sanjari na kuifafanua sheria namba sita ya mwaka 2013 ya vyama vya ushirika.
Amesema kuwa wengi wa wanachama wa vyama vya ushirika wamekuwa wanashindwa kutofautisha vicoba na saccos na faida zake kwa jamii hususani kuweka akiba na amana jambo hilo limechangia kuwepo mapungufu mengi katika vyama vya ushirika hapa nchini.
Awali akisoma taarifa kabla ya kumkaribisha  mgeni rasmi Mwenyekiti wa TCCIA Longido Saccos Ltd Flora Swai amesema kuwa chama hicho kina jumla ya wanachama 147 ambapo kina mtaji wa kiasi cha tsh.14 milion na kuwataka  wanachama wenzake kuhakikisha wanajiwekea hisa ili kuweza kufikia malengo ya chama chao.
Amesema kuwa kuanzia mwakani wataweka utaratibu wa kuwapongeza wanachama watakaofanya vizuri na kuitaka serikali kuwafikia vyama vya ushirika hapa nchini kuweza kutoa elimu ya uwelewa kwa wanachama wa saccos mbali mbali ili ziwe na tija na kuongeza pato la mwananchi na taifa kwa ujumla.
“Nawasihii wanachama wenzangu kujiwekea amana na kupenda kuuliza ili kuweza kujiletea maendeleo ambapo wengi  wamekuwa pindi kunapotolewa wito wavikao wanashindwa kufikia viwe vya serikali ama vya ushirika nawaomba muwe na moyo wa kuitikia wito pindi unaposikia na sio kupuuzia wito”alisisistiza Swai
Mwisho…………………………………………………………..





Mwili Mwingine Waonekana Ukielea Ajali Mv Nyerere tanzia



Mwili mmoja wa mtoto umepatikana saa nne asubuhi hii, wakati wazamiaji wakiweka sehemu ya chini Maputo (boya) yanayojazwa upepo ili kukiinua kivuko cha MV Nyerere, eneo la Bwisya kisiwani Ukara, jijini Mwanza.
Kazi ya kukinyanyua kivuko hicho  kilichozama Alhamisi iliyopita na kusababisha vifo vya watu  225 ilianza jana  Jumamosi Septemba 23.
Kazi hiyo inafanywa na kampuni ya Songoro Marine chini ya usimamizi wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ).
Akizungumza mbele ya Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa katika Kijiji cha Bwisya Kisiwa cha Ukara kilipozama kivuko hicho, mtaalamu kutoka kampuni hiyo, Meja Songoro alisema hatua ya kwanza itakuwa kuingiza hewa ndani ya kivuko ili kuyatawanya maji na kuanza kukivuta.
“Kivuko kinaendelea kuelea kwa sababu kuna hewa ndani yake. Wakati kinageuka (kupinduka) kilichota maji, tutaanza kuingiza hewa kutoa maji na kuanza kukivuta. Tutakapoanza kuyatawanya maji hayo, pia tutapeleka boya na hii itafanya chombo kizidi kuja juu. Baada ya hapo tutakisogeza taratibu hadi kwenye maji mafupi.”
 
Usisahau Kuinstall  Andoid Applicatuion yetu ili kupata habari zetu kwa haraka zaidi. Ingia Playstore, search Manyara leo blog

Breaking: Shaffih Dauda afikishwa mahakamani... Aachiwa kwa Dhamana

Wamilikiwa wa blog ya Dauda.com  wameachiwa kwa dhamana na Mahakama ya Mkazi Kisutu ambao ni pamoja na mtangazaji wa Clouds fm Shaffih Dauda. Wawili hao wanatuhimiwa kwa kosa la kuendesha blogs bila kuwa na kibali.

Licha ya Kesi hiyo imehairishwa mpaka tarehe 8 mwezi wa kumi,washtakiwa hao walikataa tuhuma hizo za kumiliki blog bila kuwa na kibali.
Wakili wa upande wa Jamhuri ameiomba Mahakama kuhairisha shauri hilo mpaka pale upelelezi utakapokamilika, na kwa Wakili wa upande wa utetezi Jebra Kambone ameiomba Mahakama kuwapa dhamana wateja wake kwa kuwa haki ya kupata dhamana ipo na Hakimu wa kesi hiyo amekubali kuwapa dhamana washtakiwa hao.

Shafiih na wenzake ambaye anashikiliwa ni Ben Ali (Ben On Air) ambaye alikuwa muendeshaji wa Dauda TV kupitia mtandao wa (Youtube) walikamatwa wiki iliyopita kwa kosa la kuendesha blog hiyo bila kuwa na kibali kutoka TCRA.

Mawasiliano ya simu kuvifikia Vijiji vyote nchini kwa gharama nafuu


Serikali kwa kushirikiana na Mfuko wa Mawasiliano kwa wote imejipanga kuhakikisha vijiji vyote nchinivinapata huduma ya Mawasiliano ya simu za Mkononi kwa gharama Nafuu ifikapo mwakanin,2019.

Akiongea na waandishi wa habari jijini Arusha  katika mkutano wa siku mbili wa Taasisi za udhibiti waMawasiliano katika nchi za Ukanda wa Afrika Mashariki(EACO),Naibu waziri wa Uchukuzi na MawasilianoMhandisi Atashasta Nditie.

Amesema hadi sasa Tanzania ina asilimia 94 ya wananchi  wanaotumia mawasiliano ya Simu za Mkononina kwamba ifikapo mwaka 2019 watanzania wote watafikiwa na huduma hiyo ya mawasiliano ya uhakika .

''Ndani ya kipindi cha mwaka mmoja watanzania wote watakuwa wamefikiwa na mawasiliano ya uhakika naNinaposema mawasiliano simaanishi Mitandao yote ya Simu iwafikie ila tunamaanisha hata mtandaommoja ukifika tayari watanzania watakuwa wamefikiwa na mfumo wa Mawasiliano "Amesema Naibu waziri

Katika hatua nyingine Mhandisi Nditie Amesema mfuko wa mawasiliano kwa wote utajenga Minara yamawasiliano kwa vijiji 369 kuanzia mwezi ujao wa kumi ,hivyo kuongeza huduma ya mawasiliano,jambolitakalosaidia kuimarisha uchumi kupitia sekta ya mawasiliano.

Awali  katibu Mtendaji wa  taasisi  ya mawasiliano ya Afrika Mashariki (EACO),Ally Simba amesema.nchi zajumuia ya Afrika Mashariki zimepiga hatua kubwa katika mawasiliano ya Simu za Mkononi kwa asilimia 50na Intaneti asilimia75 ikiwemo  Tanzania yenye asilimia 94,Kenya asilimia 90 na Uganda ni asilimia 70.

Lengo la mkutano huo ni kuhakikisha vijiji vyote vilivyoko katika nchi za jumuiya ya Afrika Mashariki visivyona Mawasiliano vinapata huduma hiyo  "Amesema

Naye Mkurugenzi wa Mamlaka ya Mawasiliano NchiniTCRA),Mhandisi James  Kilaba Amesema Mamlakahiyo itaendelea kudhibiti maudhui ya mawasiliano  pamoja na kusimamia  sheria ya mtandaoni

"Tanzania imekuwa nchi ya kwanza kwa nchi za jumuiya ya Afrika mashariki kwa kuanzisha mfuko maalamukwa ajili ya kupeleka huduma ya mawasiliano kwenye vijiji ambavyo kampuni za Simu zinaona havina mvutowa kibiasharaAmesema

Amesema mamlaka ya mawasiliano nchini imelazimika kuuza kwa mnada Masafa ya mwendo kasi ilikuwawezesha wananchi kote nchini kupata huduma ya Mawasiliano ya uhakika.
 
Mkurugenzi wa TCRA James Kilaba