Mgodi wa dhahabu wa Acacia Buzwagi umezindua maktaba iliyogharimu shilingi milioni 22.4 kwenye shule ya sekondari Bugisha iliyopo katika kata ya Mondo wilayani Kahama mkoani Shinyanga kwa lengo la kusaidia wanafunzi na walimu kuchangia katika kuboresha ubora wa elimu inayotolewa.
Maktaba hiyo imezinduliwa leo Alhamis Februari 8,2018 na Mkurugenzi wa halmashauri ya Mji wa Kahama,Underson Msumba na kuhudhuriwa pia na Meneja Mkuu wa Migodi ya Buzwagi na Bulyanhulu,Benedict Busunzu.
Hii ni maktaba ya pili katika wilaya ya Kahama kuzinduliwa na mgodi huo ambapo mwaka 2017 mgodi wa Buzwagi ulianzisha maktaba ya jamii katika kata ya Kagongwa ili kutoa rasilimali za elimu ya aina mbalimbali kwa wanafunzi na jamii kwa ujumla.
Akizungumza wakati uzinduzi huo, Meneja Mkuu wa Migodi ya Buzwagi na Bulyanhulu,Benedict Busunzu maktaba hiyo itasaidia kuboresha upatikanaji wa elimu kwa wanafunzi kutoka jamii inayouzunguka mgodi wa Buzwagi.
Alisema kupitia mpango wa Acacia wa maendeleo ya jamii wameamua kushirikiana na shirika la kimataifa la Read International kuboresha jengo moja la shule hiyo na kuliwekea samani kwa ajili ya matumizi ya maktaba.
“Read International ni wadau wetu wakubwa hasa katika masuala ya elimu na wamekuwa chachu ya kuleta maendeleo,kwa kutambua umuhimu wao tuliamua kukaa chini na kuamua kukarabati jengo moja na kulifanya maktaba ili vijana wetu wapate mahali pa kupatia maarifa zaidi”,alieleza.
Busunzu alisema Acacia itaendelea kuunga mkono sekta ya elimu nchini kwa njia ya kujenga miundombinu ya shule kama vile vyumba vya madarasa,nyumba za walimu,vyoo na maabara na kutoa misaada kwa wanafunzi kupitia vifaa vya elimu mfano vitabu,sare na ada kupitia programu ya CanEducate.
“Misaada inayotolewa na Acacia katika sekta ya elimu ni sehemu ya sera ya wajibikaji kwa jamii ya kampuni inayojikita katika kuhakikisha jamii inakuwa endelevu kupitia sekta ya elimu na sera hiyo inachangia moja kwa moja maono ya taifa hadi kufikia mwaka 2025 na malengo ya nchi ya kuleta maendeleo endelevu kwa kuhakikisha jamii inapata elimu iliyo bora”,alieleza.
Naye Mwakilishi wa shirika la Read International linalojihusisha na masuala ya elimu,Esther Kalwinzi mgodi wa Buzwagi ndiyo uliotoa shilingi milioni 22.4 kwa ajili kukarabati darasa kuwa maktaba.“Jumla ya vitabu 1,278 vimehifadhiwa katika maktaba hii ambayo itahudumia wanafunzi wapatao 290 na walimu 23 na jumla ya gharama za marekebisho ya jengo hili,vitabu na samani za maktaba ni shilingi 22,442,953”,alifafanua Kalwinzi.
Kwa upande wake,mgeni rasmi katika hafla hiyo,Mkurugenzi wa Mji wa Kahama,Underson Msumba aliushukuru mgodi huo kwa kuendelea kuwa karibu na jamii inayowazunguka na kushirikiana katika shughuli za maendeleo.
“Wakati mwingine huwa nafikiria bila mgodi Kahama ingekuwaje,kwa kweli mgodi umefanya juhudi nyingi katika kuboresha sekta ya elimu katika wilaya yetu,ninaamini uwepo wa maktaba hii utawafanya wanafunzi kufanya vizuri zaidi katika masomo yao”,alisema Msumba.
Aidha aliwataka wanafunzi kuzingatia masomo yao huku akisisitiza kuwa elimu ndiyo urithi pekee wa kudumu na wenye kubadilisha maisha yao.
Muonekano wa jengo la maktaba katika shule ya sekondari Bugisha lililoboreshwa na mgodi wa Buzwagi kwa kushirikiana na Read International - Picha zote na Kadama Malunde - Malunde1 blog
Mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya Kahama Mji Underson Msumba,meneja mkuu wa migodi ya Buzwagi na Bulyanhulu Benedict Busunzu ,viongozi mbalimbali wa kata ya Mondo,walimu na wanafunzi wakiwa nje ya jengo hilo la maktaba kabla ya kuzinduliwa rasmi
Mkurugenzi wa halmashauri ya Mji wa Kahama,Underson Msumba akikata utepe kuzindua rasmi jengo la maktaba katika shule ya sekondari Bugisha. Katikati ni Meneja mkuu wa migodi ya Buzwagi na Bulyanhulu Benedict Busunzu.Wa kwanza kushoto ni Mwakilishi wa shirika la Read International ,Esther Kalwinzi akifuatiwa na diwani wa kata ya Mondo Kija Peja
Mwakilishi wa shirika la Read International ,Esther Kalwinzi akionesha sehemu ya kuangalia orodha/aina ya vitabu vilivyopo katika maktaba hiyo
Mkurugenzi wa halmashauri ya Mji wa Kahama,Underson Msumba akiangalia vitabu katika maktaba ya shule ya sekondari Bugisha
Mkurugenzi wa halmashauri ya Mji wa Kahama,Underson Msumba na Meneja mkuu wa migodi ya Buzwagi na Bulyanhulu Benedict Busunzu wakisoma vitabu ndani ya maktaba ya shule ya sekondari Bugisha
Mkurugenzi wa halmashauri ya Mji wa Kahama,Underson Msumba akiangalia mandhari ya maktaba hiyo
Mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya Kahama Mji Underson Msumba,meneja mkuu wa migodi ya Buzwagi na Bulyanhulu Benedict Busunzu ,viongozi mbalimbali wa kata ya Mondo,walimu na wanafunzi wakiwa nje ya jengo la maktaba baada ya uzinduzi
Mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya Kahama Mji Underson Msumba akiwasisitiza wanafunzi kuzingatia masomo yao
Meneja mkuu wa migodi ya Buzwagi na Bulyanhulu Benedict Busunzu akielezea namna walivyoshirikiana na shirika la Read International katika kufanikisha ukarabati wa jengo hilo la maktaba
Mwakilishi wa shirika la Read International ,Esther Kalwinzi akizungumza wakati wa hafla fupi ya uzinduzi wa jengo la maktaba katika shule ya sekondari Bugisha
Mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya Kahama Mji Underson Msumba
Mkuu wa shule ya sekondari Bugisha Limbuzizi Magumba akiushuru mgodi wa Buzwagi kwa kutoa shilingi milioni 22.4 kwa ajili ya ukarabati wa maktaba katika shule yake
Wanafunzi wa shule ya sekondari Bugisha wakiimba shairi wakati wa hafla ya kuzindua maktaba katika shule hiyo
Mwanafunzi Tedy Martine akisoma risala akisoma risala kwa mgeni rasmi.Alizitaja miongoni mwa changamoto zilizopo katika shule hiyo kuwa ni upungu wa viti na meza hali inayowafanya wakae wawili wawili lakini pia upungufu wa walimu wa masomo ya sayansi.
Diwani wa kata ya Mondo Kija Peja akiushukuru mgodi wa Buzwagi kwa kuendelea kusaidia jamii na kuomba ushirikiano uendelee kuwepo.
Picha zote na Kadama Malunde - Malunde1 blog
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni