Na Ahemd Mahmoud
Katika juhudi za serikali za kuimarisha mazingira ya ujifunzaji wanafunzi wa kike hapa nchini,Taasisi ya maendeleo ya jamii Tengeru iliyopo Jijini Arusha kwa mwaka wa fedha 2022/2023 imeipatia shilingi Bilion 2.3 kwa ajili ya ujenzi wa bweni la kike ambalo litasaidia kuondoa changamoto wanazokabiliana nazo ikiwemo vitendo vya ubakaji .
Akizungumza na vyombo vya habari Jijini Dodoma wakati akiwasilisha utekelezaji na mwelekeo kwa mwaka wa fedha 2022/2023 Mkuu wa Taasisi ya maendeleo ya jamii Tengeru Dkt. Bakari George amesema kuwa Bweni hilo lenye uwezo wa kubeba wanafunzi 568 litakuwa mkombozi kwao na taasisi hiyo
Amesema kuwepo kwa bweni hilo itasaidia pia kuwafatilia kwa ukaribu ukizingatia kujua mienendo yao kwani wanapokuwa mtaani wanakumbana na changamoto nyingi ambazo upelekea wengi kushindwa kutimiza ndoto zao na ukizingatia kwa sasa vyuo vingi kwa sasa vinachukua vijana chini ya miaka 17 ambao wamemaliza kidato cha nne ambao wanapaswa kupewa uangalizi.
Pia amesema kuwa taasisi hiyo imeanzisha utaratibu wa kuwachangia fedha wanafunzi wanaoishi mazingira magumu huku akiwataka watanzania watakaowiwa kutoa michango yao ili wanafunzi hao waweze kutimiza malengo yao .
"Kama mnavyojua mtoto wa kike ukimjengea mazingira rafiki ya uzomaji atatimiza ndoto zake kwa hiyo sisi kama taasisi tumejipanga kuboresha miundo mbinu hivyo niwaombe watanzania wenye mapenzi mema na watoto waishio mazingira magumu watume michango yao ili tuweze kuwasaidia"amesema Dkt. Bakari.
Vile vile amesema Kwa mwaka 2022/2023, kituo kinatarajia kushirikiana na wadau kutekeleza utolewaji wa huduma ya msaada wa kisheria kwa kuzingatia falsafa ya maendeleo ya jamii.
Aidha ameongeza kuwa kituo kinaandaa programu ya mafunzo kwa maafisa bajeti wa mamlaka za serikali za mitaa kuwajengea uwezo katika maandalizi ya bajeti zinazozingatia usawa wa kijinsia.
Kwa upande wake Msemaji mkuu wa Serikali Gerlison Msigwa amesema kuwa serikali kwa kutambua umuhimu wa elimu tayari imeajiri maafsa maendeleo ya jamii 3000 huku mahitaji yakiwa ni zaidi ya elfu tano ili jamii iweze kufikiwa na wataalamu.