Zitto Kabwe, CHADEMA Watofautiana Tena

Ikiwa ni takribani miaka mitano tangu Mbunge wa Kigoma Mjini, Zitto Kabwe, avurugane na Chadema ambacho kilikuwa chama chake, sasa hali hiyo inaonekana kurudi tena kupitia uchaguzi wa ubunge wa Afrika Mashariki (EALA).

Tofauti na awali ambapo alikosana na Chadema na kufukuzwa uanachama kutokana na kile kilichodaiwa ni kuandaa waraka wa mabadiliko ya 2013, sasa hivi ubunge wa EALA unaonekana kumvuruga tena mwanasiasa huyo na Chadema, baada ya kuandika barua kwa Spika wa Bunge akitaka utaratibu uliotangazwa wa namna ya kupata wabunge ubadilishwe.

Utaratibu huo mpya uliotangazwa, unatoa nafasi kwa wabunge wa EALA kwa mwaka 2017 kulingana na idadi ya wabunge wa kila chama kwenye Bunge la Jamhuri ya Muungano.

Kwa mujibu wa Mwongozo huo, kutokana na idadi ya wabunge wa vyama kwa kila chama, CCM imepata nafasi za wabunge sita kwenda EALA, Chadema mbili, CUF moja, huku ACT Wazalendo  pamoja na NCCR Mageuzi, vikiwa havina nafasi hata moja kwenye Bunge hilo la Afrika Mashariki, kutokana na kuwa na mbunge mmoja kila kimoja, hivyo kutokidhi vigezo.

Kutokana na hali hiyo, Zitto ameliandikia Bunge barua kutaka Kamati ya Kanuni za Bunge ikutane kujadili uchaguzi wa wajumbe wa Tanzania kwenye Bunge la Afrika Mashariki.

Barua hiyo, ambayo baadhi ya wachambuzi wa siasa wanadai inalenga kutaka utaratibu wa awali ubadilishwe ili chama cha Zitto (ACT Wazalendo), kimwingize mwanachama wake, Profesa Kitila Mkumbo kugombea ubunge huo, inasema mwongozo uliotolewa na Bunge umekwenda kinyume cha Mkataba wa Jumuiya ya Afrika Mashariki.

Wanasema endapo hoja ya Zitto ikikubaliwa, ni rahisi zaidi wagombea wa Chadema wakakosa nafasi hizo na badala yake nafasi za upinzani kuiwakilisha Tanzania kwenye Bunge la Afrika Mashariki zikachukuliwa na wagombea wa ACT na wale wa CUF.

Hali hiyo inaelezwa kuchangiwa na wabunge wengi kwenye Bunge la Jamhuri wa Muungano wa Tanzania kuwa ni wa CCM, hivyo ni rahisi kuweka msimamo wa kuwapigia kura wale wagombea wa ACT Wazalendo na wale wa CUF, badala ya wale wa Chadema kutokana na hali ya kisiasa iliyopo nchini kwa sasa.

Barua ya Zitto ya Machi 28 iliyoandikwa kutokana na Tangazo la Bunge kwenye gazeti namba 11 la Machi 17, lililotangaza uchaguzi huo na masharti yake, ilisema mwongozo wa uchaguzi huo unavunja kanuni mbalimbali na kwamba kitakachofanyika sasa kitakuwa ni uteuzi na siyo uchaguzi.

Alisema pia mwongozo huo, mbali na kuvunja Mkataba wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, unataka suala la jinsi lizingatiwe kwenye wabunge wanaokwenda kuiwakilisha nchi katika Bunge hilo.

Baada ya Zitto kuandika malalamiko hayo, Mwanasheria wa Chadema, John Malya, naye aliyajibu akirejea hukumu mbili za kesi ya Anthon Komu (kwenye Divisheni ya Mwanzo na Divisheni ya Rufani).

Malya aliandika kwamba, mwongozo wa Ofisi ya Spika wa Bunge wa kugawa idadi ya viti kwa vyama ni sahihi, kwa sababu Divisheni zote mbili za Mahakama ya Haki ya Afrika Mashariki ziliamua.

Katika sehemu ya barua yake, alisema: “Mwenye kupaswa kubeba mzigo wa makundi ya Zanzibar, Bara na Wanawake (ukiachilia mbali kundi la vyama vya upinzani) ni chama chenye wabunge wengi (CCM)”.

Hoja hiyo ya Malya inachambuliwa na Ado Shaibu, ambaye aliandika ujumbe unaogusa hoja za kisheria ambazo alitumia Malya kukosoa malalamiko ya Zitto.

Shaibu alisema ni kosa kutumia kesi ya Antony Komu ambayo iliamuliwa na Divisheni ya Mwanzo ya Mahakama ya Afrika Mashariki, lakini baadaye Divisheni ya Rufani ya Mahakama ya Haki ya Afrika Mashariki ikatengua hukumu hiyo kwa hoja ya kwamba Divisheni ya Mwanzo ya Mahakama haikuwa na mamlaka ya kuamua suala husika.

MAHAKAMA KUU YAMWAMURU MSAJILI WA VYAMA VYA SIASA KUTOTOA RUZUKU KWA PROF. LIPUMBA NA KUNDI LAKE MPAKA SHAURI LITAKAPOAMULIWA

Mahakama Kuu imemuamuru Msajili wa Vyama vya Siasa nchini kutotoa ruzuku kwa Prof. Ibrahim Lipumba wa Chama cha Wananchi, CUF, na kundi lake.

Zuio hilo ni mpaka shauri dhidi ya Msajili na Mwanasheria Mkuu wa Serikali kuhusu kutoa fedha za ruzuku shilingi milioni 369 kwa njia za wizi na udanganyifu litakaposikilizwa na kutolewa maamuzi.

Uamuzi huo umefikiwa na Jaji Dyansobela baada ya kukubaliana na hoja zilizowasilishwa kwa hati ya dharura.

Jopo la Mawakili wa CUF, liliiomba Mahakama Kuu kutoa amri hiyo kwa kuwa fedha zilizotolewa awali shilingi milioni 369 hazijulikani zimetumika vipi, na hazikuwa katika mikono salama wala hakuna udhibiti wowote wa chama kuhusu fedha hizo ikizingatiwa kwamba, Prof. Lipumba alishavuliwa uanachama.

Mawakili hao akiwemo Juma Nassor , wamesisitiza kwamba, mazingira yaliyopo ni vyema na busara kwa fedha za umma zilizopaswa kutolewa kama ruzuku kwa chama cha CUF kwa sasa ziendelee kubakia serikalini.

Aidha, wameiomba Mahakama Kuu kwamba amri hiyo pia ifungamane na kesi ya msingi namba 23/2016 ya kuhoji maamuzi ya msajili kumtambua Prof Lipumba kwa nafasi ya uenyekiti iliyopo mbele ya Jaji Kihijo ambayo kwa sasa imekatiwa rufani ya kufanyiwa marejeo mbele ya Mahakama ya Rufani Tanzania.

Afikishwa Mahakamani Kwa Kusambaza Picha za Uchi

Mkazi wa Tazara Magorofani, Shaban Biro (47), amefikishwa katika Mahakama ya Wilaya ya Ilala , kujibu shtaka la kusambaza na kuonyesha picha za utupu katika mitandao ya kijamii.
 
Biro (47), alifikishwa mahakamani hapo leo na kusomewa shtaka hilo mbele ya Hakimu Mkazi Flora Mjaya.
 
Akisoma hati ya mashtaka, Wakili wa Serikali Glory Mwenda, alidai kuwa mshitakiwa alitenda kosa Machi, 2016 mtaa wa Kilosa uliopo wilaya ya Ilala.
 
Inadaiwa mshitakiwa alisambaza picha hizo kwenye mitandao ya kijamii kwa kutumia simu ya mkononi aina ya Huawei ambazo zilikuwa zinamwonyesha Nuru Awadhi akifanya mapenzi.
 
Mshitakiwa alikana shtaka na hakimu Mjaya alihirisha kesi hiyo hadi April 17,2017 itakapotajwa.

Waziri wa Elimu Prof.Ndalichako amezindua mpango wa African Capacity katika Chuo cha Nelson Mandela Arusha

Waziri wa Elimu na Sayansi Prof. Joyce Ndalichako mapema leo asubuhi amewasili kwenye Chuo cha Sayansi na Tekinolojia Nelson Mandela Arusha kwa ajili ya Uzinduzi wa mpango wa African Capacity unaofadhiliwa na Benki ya ADB.
Akizungumza na wanafunzi wa Chuoni hapo Profesa Ndalichako amesema Atawachukulia hatua kali waajiri katika sekta ya Elimu watakaowakataza baadhi  ya wafanyakazi waliopata ufadhili wa kwenda masomoni kujiendeleza .

Pia akiwa kwenye uzinduzi huo waziri alifanikiwa kutembelea maabara mbalimbali za idara tofauti za Chuo hicho zinazotumika na wanafunzi kwa ajili ya majaribio na pia alipata wasaaa wakutembelea shamba la migomba lililopo nje kidogo ya chuo hicho.

Waziri wa Elimu akisalimia na watumishi ya Chuo cha Nelson Mandela leo Asubuhi baada ya kuwasili chuoni hapao .



Waziri wa Elimu profesa Joyce Ndalichako ( katikati ) Akimsikiliza Mkuu wa Maabara ya Taasisi ya Chuo Kikuu cha Nelson Mandela jijini Arusha .

Pichani ni wanafunzi wa PHD in material science and Energy lub,Agatha Wagotu na Joyce Elisadiki wakiwa ndani ya Maabara wakifanya majaribio.

SEMINA YA VIONGOZI NA WAANDISHI WA VYOMBO VYA HABARI .



Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akisalimiana na Katibu Mkuu Kiongozi Dkt.Abdulhamid Yahya Mzee na Viongozi wengine alipowasili katika viwanja vya Ukumbi wa Zamani wa Baraza la Wawakilishi Mnazi mmoja Mjini Unguja katika Semina ya Viongozi na Waandishi wa habari wa Vyombo vya Serikali iliyofanyika leo. 


Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akisalimiana na Waziri wa Habari,Utalii,Utamaduni na Michezo Mhe,Rashid Ali Juma na Viongozi wengine alipowasili katika viwanja vya Ukumbi wa Zamani wa Baraza la Wawakilishi Mnazi mmoja Mjini Unguja katika Semina ya Viongozi na Waandishi wa habari wa Vyombo vya Serikali iliyofanyika leo. 

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akifuatana na Mkuu wa Mkoa Mjini Magharibi Mhe,Ayoub Mohamed Mahmoud mara alipowasili katika viwanja vya Ukumbi wa Zamani wa Baraza la Wawakilishi Mnazi mmoja Mjini Unguja katika Semina ya Viongozi na Waandishi wa habari wa Vyombo vya Serikali iliyofanyika leo.

Waziri wa Habari,Utalii,Utamaduni na Michezo Mhe,Rashid Ali Juma alipokuwa akimkaribisha Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein kuzungumza na Viongozi na Waandishi wa habari wa Vyombo vya Serikali katika wengine alipowasili katika Semina ya siku moja iliyofanyika leo katika Ukumbi wa Zamani wa Baraza la Wawakilishi Mnazi mmoja Mjini Unguja.


Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein alipokuwa akizungumza na Viongozi na Waandishi wa habari wa Vyombo vya Serikali katika Semina ya siku moja iliyofanyika leo katika Ukumbi wa Zamani wa Baraza la Wawakilishi Mnazi mmoja Mjini Unguja.

Baadhi ya Wahariri wa Habari na waandishi wa habari wa Vyombo vya Serikali wakimsikiliza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein alipokuwa akizungumza na wanahabari hao katika Semina ya siku moja iliyofanyika leo katika Ukumbi wa Zamani wa Baraza la Wawakilishi Mnazi mmoja Mjini Unguja.

Wakuu wa Wilaya za Zanzibar na Waandishi wa habari wakiwa katika Semina ya siku moja ya Viongozi na Waandishi wa Habari wa Vyombo vya Serikali iliyofanyika leo katika Ukumbi wa Zamani wa Baraza la Wawakilishi Mnazi mmoja Mjini Unguja chini ya Mwenyekiti wake Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (hayupo pichani).

Washauri wa Rais wa Zanzibar ni mongoni mwa Viongozi waliohudhuria katika Semina ya siku moja ya Viongozi na Waandishi wa Habari wa Vyombo vya Serikali iliyofanyika leo katika Ukumbi wa Zamani wa Baraza la Wawakilishi Mnazi mmoja Mjini Unguja chini ya Mwenyekiti wake Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (hayupo pichani).

Baadhi ya Wanahabari wa Vyombo vya Serikali wakimsikiliza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein alipokuwa akizungumza na wanahabari hao katika Semina ya siku moja iliyofanyika leo katika Ukumbi wa Zamani wa Baraza la Wawakilishi Mnazi mmoja Mjini Unguja.

Baadhi ya Wanahabari wa Vyombo vya Serikali wakimsikiliza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein alipokuwa akizungumza na wanahabari hao katika Semina ya siku moja iliyofanyika leo katika Ukumbi wa Zamani wa Baraza la Wawakilishi Mnazi mmoja Mjini Unguja,[Picha na Ikulu.] 01/04/2017.

RC PWANI AAGIZWA APIGE KAMBI MIONO BAGAMOYO


*Waziri Mkuu amtaka amalize migogoro ya wakulima, wafugaji

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amemuagiza Mkuu wa Mkoa wa Pwani. Eng. Evarist Ndikilo apige kambi katika kata ya Miono wilayani Bagamoyo na kuwasaka wafugaji wanaopiga wakulima.

Waziri Mkuu alitoa agizo hilo wakati akizungumza na wakazi wa kata hiyo ambao walisimamisha msafara wake wakati akienda kukagua miundombinu ya Hifadhi ya Taifa ya Saadani iliyoko wilayani Bagamoyo, mkoani Pwani.

Akitoa kero za eneo hilo, Diwani wa Kata ya Miono, Bw. Juma Mpwimbwi alisema kata hiyo inakabiliwa na tatizo la wakulima kupigwa na wafugaji na wakipelekwa kituo cha polisi hawachukuliwi hatua yoyote.

“Wafugaji wanatupiga lakini wenzetu hawachukuliwi hatua na hata ukienda kushtaki polisi, hawakai kwa sababu wanadai wao wana fedha,” alisema diwani huyo.

Pia alisema mbali ya kero sugu ya maji, waliahidiwa barabara ya lami tangu miaka saba iliyopita lakini hadi sasa hawana hata kipande kidogo tu cha barabara hiyo.

Naye Bw. Shabani Mkwimbi ambaye alipewa nafasi ya kuzungumza kwa niaba ya wananchi wenzake, alisema kata hiyo ina kituo cha polisi na mahakama lakini utendaji kazi wa viongozi waliopo hapo unatia shaka.

“Waziri Mkuu tunataka ukimaliza kuongea na sisi, uondoke na Mkuu wa Kituo cha Polisi cha Miono, Bw. Maro na msaidizi wake Bw. Rashidi pamoja na Hakimu wa hapa, kwa sababu hawa watu habari yao ni nyingine. Mkulima akienda polisi au mahakamani hashindi kesi hata siku moja, lakini mfugaji akienda anashinda,” alisema huku akishangiliwa.

“Hawa watu wanadai wana hela na wanafanya chochote wanachotaka, na ndiyo maana hawalali polisi hata kama wameua mtu,” aliongeza.

Akijibu kero zao, Waziri Mkuu aliwahakikshia wakazi hao kwamba Serikali iliyopo madarakani ni yao na hakuna hata mtu mmoja ambaye yuko juu ya sheria.

Alisema suala la polisi wa kituo cha Miono litashughulikiwa na Kamanda wa Polisi wa Mkoa huo, ambaye alikuwepo katika msafara wake. “Tena Mkuu wa Mkoa yuko hapa na yeye ndiye Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa huu, atasimamia hilo.”

Akifafanua kuhusu suala la wafugaji kuwapiga wakulima, Waziri Mkuu alisema msimamo wa Serikali ni kuwaona wakulima wanafanya kazi zao kwa uhuru na wafugaji nao wanafanya kazi zao kwa uhuru. “Hakuna mfugaji anayeruhusiwa kupeleka ng’ombe wake kwenye mashamba yenye chakula. Hili haliruhusiwa hata kidogo,” alisisitiza.

“Mkuu wa Mkoa hili ni agizo. Njoo upige kambi hapa na watu wako, na usake  wahusika hadi wabainike. Ni lazima tuwajue ni akina nani wamehusika na hili,” alisema.

Aliwataka maafisa mifugo wa mkoa huo waende kwa wafugaji na kutambua mifugo waliyonayo na kama kuna maeneo wahakikishe wanapatiwa maeneo rasmi ili waweze kupatiwa matibabu kwa ajili ya mifugo yao.

Aliwataka wafugaji wanaokata mabomba ya maji ya mradi wa maji wa Chalinze (CHALIWASA) ili kupata maji ya kunywesha mifugo yao, waache tabia hiyo mara moja na akaonya kuwa watakaokamatwa, wachukuliwe hatua za kisheria mara moja. Katika ziara hiyo fupi, Waziri Mkuu alikuwa amefuatana na Mkuu wa Mkoa wa Mkoa pwani, Eng. Evarist Ndikilo, viongozi wa wilaya ya Bagamoyo na Mbunge wa jimbo hilo, Ridhiwani Kikwete.
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa (pichani kulia) akiwa ameongozana na Mkuu wa Mkoa wa Pwani. Eng. Evarist Ndikilo alipofanya ziara ya kikazi mkoani humo.

ENEO LA LEBANON SOKO LA SAMAKI LA FERRY JIJINI DAR ES SALAAM KINARA KWA UKATILI WA KIJINSIA


 Mwenyekiti wa Soko la Kimataifa la Samaki la Ferry, Ali Bunda akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani), Dar es Salaam juzi wakati akitoa taarifa ya kupungua kwa vitendo vya ukatili wa kijinsia katika soko hilo, baada ya kupata mafunzo kutoka Shirika la Equality for Growth (EfG). Bunda alilitaja eneo la Lebanon katika soko hilo kuwa ni hatari kwa ukatili wa kijinsia hasa kwa watoto.