SERIKALI YASIKIA KILIO CHA WADAU WA SEKTA YA UWINDAJI WA KITALII NCHINI, YAONGEZEA MIAKA MIWILI YA UMILIKI WA LESENI ZA VITALU
posted on
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla akizungumza na wadau wa sekta ya uwindaji wa kitalii katika mkutano uliondaliwa na Wizara yake mjini Dodoma jana kwa ajili ya kujadili mikakati mbalimbali ya kuimarisha sekta hiyo ikiwemo utekelezaji wa azma ya Serikali ya kuanzisha utaratibu mpya wa utoaji wa leseni za vitalu vya uwindaji wa kitalii kwa njia ya mnada. Kushoto ni Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Mej. Jen. Gaudence Milanzi na Naibu Katibu Mkuu, Dk. Aloyce Nzuki (kulia).
Na Hamza Temba, Dodoma
...............................................................
Serikali imesikia kilio cha wadau wa sekta ya uwindaji wa kitalii nchini na kuamua kuongeza muda wa miaka miwili ya umiliki wa leseni za vitalu 95 vya uwindaji wa kitalii ambazo zilikuwa ziishe muda wake tarehe 31 Desemba mwaka huu (2017).
Uamuzi huo umefikiwa na Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla wakati wa kikao cha majumuisho na watendaji wa Wizara hiyo muda mfupi baada ya kumalizika kwa mkuano wa wadau wa sekta hiyo ulioandaliwa na Wizara hiyo mjini Dodoma jana.
Akizungumzia uamuzi huo Dk. Kigwangalla alisema, lengo ni kuwapa muda wawekezaji hao ili waweze kujiandaa na mabadiliko ya mfumo mpya wa utowaji wa leseni za vitalu vya uwindaji wa kitalii kwa njia ya mnada ikiwemo kurudisha baadhi ya gharama za uwekezaji walizoweka katika vitalu hivyo.
Awali akizungumza katika mkutano huo wa wadau Mwenyekiti wa Chama cha Wamiliki wa Kampuni za Uwindaji wa Kitalii nchini, Michael Mantheakis alimuomba Waziri Kigwangalla kuwaongezea muda wa umiliki wa leseni zao kuanzia miaka mitano au mitatu na nusu ili waweze kurudisha gharama za uwekezaji walizowekeza katika vitalu hivyo ikiwemo ujenzi wa miundombinu, makambi na vifaa vyake pamoja na maji.
Hata hivyo, Waziri Kigwangalla aliweka wazi msimamo wa Serikali wa kutimiza azma yake ya kuingia kwenye utaratibu mpya wa utoaji wa leseni za vitalu vya uwindaji wa kitalii kwa njia ya mnada na kusema kuwa kamwe haitorudi nyuma na kwamba utekelezaji wa zoezi hilo hauwezi kusubiri muda mrefu kiasi hicho.
Akizungumzia kuhusu hatua ya utekelezaji wa utaratibu huo, Waziri Kigwangalla alisema kwa sasa taratibu za kuandaa Sheria za usimamizi zinaendelea na zinatarajiwa kukamilika mwezi Februari 2018 pamoja na kanuni zake zinazotarajiwa kukamilika mwezi Aprili 2018.
Aidha, alisema mfumo maalumu wa kielektroniki unaandaliwa ambapo maombi yote ya leseni za umiliki wa vitalu vya uwindaji kwa njia ya mnada yatafanyika kwa uwazi kwa njia ya mtandao.
Alisema baada ya kukamilika kwa taratibu zote na mfumo huo mpya wa utoaji wa leseni za vitalu vya uwindaji wa kitalii kwa njia ya mnada na maombi kuwasilishwa, mnada wa kwanza utaanza tarehe 1 Julai, 2018 kwa kuanza kunadi vitalu 61 ambavyo kwa sasa havina wawekezaji.
Mnada wa pili utafanyika mwaka 2020 baada ya kuisha kwa muda huo wa nyongeza wa miaka miwili ukihusisha vitalu 95 vilivyoongezewa muda wa umiliki wa leseni pamoja na vitalu vingine endapo vitabaki katika mnada huo wa kwanza kwa sababu mbalimbali.
Alisema sheria na kanuni zinazoandaliwa hivi sasa zitazingatia mambo muhimu ikiwemo kuwapa nafasi watanzania wenye mitaji midogo kuweza kuingia kwenye biashara hiyo pamoja na kuweka adhabu kali dhidi ya wafanyabiashara watakaohujumu biashara hiyo kwa makusudi.
Mkutano huo wa siku moja ulihudhuriwa pia na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Meja Jenerali Gaudence Milanzi, Naibu Katibu Mkuu, Dk. Aloyce Nzuki, wakurugenzi, wakuu wa vitengo na wakuu wa taasisi zilizopo chini ya wizara hiyo na waandhishi wa habari.
Oktoba 22 mwaka huu (2017) wakati akiongoza kikao cha wadau wa sekta ya Maliasili na Utalii mjini Dodoma, Waziri Kigwangalla alitangaza kufuta leseni za vitalu vya uwindaji wa kitalii zilizokuwa zianze mwezi Januari, 2018 ili kupisha utarartibu mpya wa utoaji wa leseni hizo kwa njia ya mnada ikiwa ni mkakati wa Serikali wa kuimarisha sekta hiyo.
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla akizungumza na wadau wa sekta ya uwindaji wa kitalii katika mkutano uliondaliwa na Wizara yake mjini Dodoma jana kwa ajili ya kujadili mikakati mbalimbali ya kuimarisha sekta hiyo ikiwemo utekelezaji wa azma ya Serikali ya kuanzisha utaratibu mpya wa utoaji wa leseni za vitalu vya uwindaji wa kitalii kwa njia ya mnada. Kushoto ni Naibu Katibu Mkuu, Dk. Aloyce Nzuki.
Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii, Meja Jenerali Gaudence Milanzi (kushoto) akizungumza katika mkutano huo. Kulia ni Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla.
Mdau wa sekta ya uwindaji wa kitalii, Dk. Licky Abdallah akizungumza katika mkutano huo.
Mdau wa sekta ya uwindaji wa kitalii ambaye pia ni mmilikia wa kampuni ya uwindaji wa kitalii ya Bushman Hunting Safaris, Talal Abood akiwasilisha mapendekezo yake katika mkutano huo.
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla akisikiliza kwa makini mapendekezo ya wadau wa sekta ya uwindaji wa kitalii katika mkutano uliondaliwa na Wizara yake mjini Dodoma jana. Kushoto ni Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Meja Jenerali Gaudence Milanzi.
DK. KIGWANGALLA NA MKURUGENZI MKAZI WA UNDP KUANZISHA KIKOSI KAZI CHA KUCHUNGUZA TUHUMA ZA UJANGILI WA TEMBO KATIKA HIFADHI YA RUAHA
posted on
Na Mwandishi Wetu - Dar es Salaam
.....................................................................
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla na Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP), Bi. Natalie BOUCLY wamekubaliana kuanzisha kikosi kazi cha pamoja cha kuchunguza tuhuma zilizotolewa hivi karibuni na kituo cha habari cha ITV LONDON kuhusu ujangili wa Tembo katika Hifadhi ya Taifa ya Ruaha iliyopo Mkoani Iringa.
Dk. Kigwangalla na Mkurugenzi huyo, wamefikia makubaliano hayo leo Januari 2, 2018 wakati wa mazungumzo yaliyofanyika katika ofisi ndogo ya Wizara ya Maliasili na Utalii, Mpingo House Jijini Dar es Salaam.
Aidha, Waziri Kigwangalla amemueleza Mkurugenzi huyo kuwa Wizara yake inaandaa mikakati mbalimbali ya kuongeza idadi ya watalii nchini na mapato ikiwemo kuwashirikisha wananchi kuandaa mwezi maalum wa Urithi wa Tanzania pamoja na kuimarisha mifumo ya ukusanyaji wa mapato kwa njia za kielektroniki katika vituo mbalimbali ya Utalii.
Kwa upande wake, Mkurugenzi huyo amemuahidi Waziri Kigwangalla kuendelea kumpa ushirikiano katika nyanja mbalimbali za kuendeleza Utalii nchini na uhifadhi wa misitu na wanyamapori kwa ujumla.
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla (kulia) akizungumza naMkurugenzi Mkazi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa hapa nchini (UNDP), Bi. Natalie BOUCLY katika ofisi ndogo ya Wizara hiyo, Mpingo House Jijini Dar es Salaam leo.
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla (kulia) akimsikilizaMkurugenzi Mkazi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa hapa nchini (UNDP), Bi. Natalie BOUCLY wakati wa mazungumzo yaliyofanyika leo katika ofisi ndogo ya Wizara hiyo, Mpingo House Jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla (kulia) akiagana naMkurugenzi Mkazi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa hapa nchini (UNDP), Bi. Natalie BOUCLY baada ya mazungumzo yaliyofanyika katika ofisi ndogo ya Wizara hiyo, Mpingo House Jijini Dar es Salaam leo.
NEC YATANGAZA TAREHE YA KUFANYIKA KWA UCHAGUZI MDOGO KATIKA JIMBO LA SIHA NA KINONDONI PAMOJA NA KATA 4 ZA TANZANIA BARA
posted on
Makamu Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) Jaji Mkuu Mstaafu wa Zanzibar Hamid Mahmod Hamid
Subira Kaswaga – NEC
Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) imesema kuwa uchaguzi mdogo katika majimbo ya Siha mkoani Kilimanjaro na Kinondoni mkoani Dar es Salaam pamoja na Kata nne za Tanzania Bara utafanyika Februari 17, 2018 kufutia waliokuwa Wabunge katika majimbo hayo kujivua Uanachama na kukosa sifa za kuendelea kuwa wabunge.
Taarifa ya Makamu Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) Jaji Mkuu Mstaafu wa Zanzibar Hamid Mahmod Hamid imeeleza kuwa pamoja na Majimbo hayo,pia Kata nne za Isamilo katika Halmashauri ya Wilaya ya Nyamagana mkoani Mwanza, Manzase Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino mkoani Dodoma, Madanga Halmashauri ya Wilaya ya Pangani mkoani Tanga na Kimagai Halmashauri ya Wilaya ya Mpwapwa mkoani Dodoma zitafanya Uchaguzi mdogo
Aidha, Jaji Mkuu (Mst. Zanzibar) Hamid Mahmoud Hamid amesema kuwa, Tume inaendesha uchaguzi huo baada ya kupokea barua kutoka kwa Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano Mh. Job Ndugai kuhusu uwepo wazi wa jimbo la Kinondoni jijini Dar es Salaam na Jimbo la Siha mkoani Kilimanjaro.
Jaji Mahmoud amesema kuwa, barua hiyo ilieleza kuwa majimbo hayo yapo wazi baada Maulid Mtulia aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Kinondoni kujivua uanachama wa CUF na Dr. Godwin Mollel wa jimbo la Siha kujiuzulu uanachama wa CHADEMA na hivyo wote kukosa sifa za kuwa Wabunge.
Pia, ameeleza kuwa Tume ilipokea taarifa kutoka kwa Waziri mwenye dhamana ya Serikali za Mitaa ikiitaarifu Tume uwepo wa nafasi wazi za Udiwani katika kata nne za Tanzania Bara.
“Baada ya kupokea barua hizo Tume kwa kuzingatia vifungu vya 37(1) na 46(2) vya Sheria ya Taifa ya Uchaguzi sura ya 343 pamoja na kifungu cha 13(3) cha Sheria ya Uchaguzi wa Serikali za Mitaa sura ya 292 inatangaza kuwa majimbo mawili na kata nne zipo wazi” alisema Jaji Mahmoud.
Ameeleza kuwa, fomu za uteuzi kwa majimbo hayo mawili na kata nne itakuwa kati ya tarehe 14 – 20 Januari, 2018, uteuzi wa wagombea utafanyika tarehe 20/01/2018, na Kampeni za uchaguzi mdogo zitafanyika kuanzia tarehe 21/01 – 16/02/2018 na siku ya uchaguzi itakuwa tarehe 17/02/2017.
Vilevile, Jaji Mahmoud amevikumbusha Vyama vya Siasa na wadau wote wa uchaguzi kuzingatia sheria, kanuni, taratibu, miongozo na maelekezo yote wakati wa uchaguzi huo mdogo.
Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) imesema kuwa uchaguzi mdogo katika majimbo ya Siha mkoani Kilimanjaro na Kinondoni mkoani Dar es Salaam pamoja na Kata nne za Tanzania Bara utafanyika Februari 17, 2018 kufutia waliokuwa Wabunge katika majimbo hayo kujivua Uanachama na kukosa sifa za kuendelea kuwa wabunge.
Taarifa ya Makamu Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) Jaji Mkuu Mstaafu wa Zanzibar Hamid Mahmod Hamid imeeleza kuwa pamoja na Majimbo hayo,pia Kata nne za Isamilo katika Halmashauri ya Wilaya ya Nyamagana mkoani Mwanza, Manzase Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino mkoani Dodoma, Madanga Halmashauri ya Wilaya ya Pangani mkoani Tanga na Kimagai Halmashauri ya Wilaya ya Mpwapwa mkoani Dodoma zitafanya Uchaguzi mdogo
Aidha, Jaji Mkuu (Mst. Zanzibar) Hamid Mahmoud Hamid amesema kuwa, Tume inaendesha uchaguzi huo baada ya kupokea barua kutoka kwa Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano Mh. Job Ndugai kuhusu uwepo wazi wa jimbo la Kinondoni jijini Dar es Salaam na Jimbo la Siha mkoani Kilimanjaro.
Jaji Mahmoud amesema kuwa, barua hiyo ilieleza kuwa majimbo hayo yapo wazi baada Maulid Mtulia aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Kinondoni kujivua uanachama wa CUF na Dr. Godwin Mollel wa jimbo la Siha kujiuzulu uanachama wa CHADEMA na hivyo wote kukosa sifa za kuwa Wabunge.
Pia, ameeleza kuwa Tume ilipokea taarifa kutoka kwa Waziri mwenye dhamana ya Serikali za Mitaa ikiitaarifu Tume uwepo wa nafasi wazi za Udiwani katika kata nne za Tanzania Bara.
“Baada ya kupokea barua hizo Tume kwa kuzingatia vifungu vya 37(1) na 46(2) vya Sheria ya Taifa ya Uchaguzi sura ya 343 pamoja na kifungu cha 13(3) cha Sheria ya Uchaguzi wa Serikali za Mitaa sura ya 292 inatangaza kuwa majimbo mawili na kata nne zipo wazi” alisema Jaji Mahmoud.
Ameeleza kuwa, fomu za uteuzi kwa majimbo hayo mawili na kata nne itakuwa kati ya tarehe 14 – 20 Januari, 2018, uteuzi wa wagombea utafanyika tarehe 20/01/2018, na Kampeni za uchaguzi mdogo zitafanyika kuanzia tarehe 21/01 – 16/02/2018 na siku ya uchaguzi itakuwa tarehe 17/02/2017.
Vilevile, Jaji Mahmoud amevikumbusha Vyama vya Siasa na wadau wote wa uchaguzi kuzingatia sheria, kanuni, taratibu, miongozo na maelekezo yote wakati wa uchaguzi huo mdogo.
NAIBU MEYA JIJI LA MBEYA (CHADEMA) AAHIDI USHIRIKIANO NA WATEULE WA RAIS MAGUFULI AMSIFU MHE MWANJELWA KUSHIRIKIANA NA VYAMA VYA UPINZANI
posted on
Naibu Waziri wa Wizara ya Kilimo Mhe Mary Mwanjelwa akizungumza na wananchi waliojitokeza kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika katika Mtaa wa Kagwina Kata ya Sinde Jana Januari 2, 2018. Picha Zote Na Mathias Canal
Naibu Meya wa Jiji la Mbeya Mhe Fanuel Kyanula ambaye ni Diwani wa Kata ya Sinde akizungumza na wananchi waliojitokeza kwenye mkutano wa hadhara uliohudhuriwa na Naibu Waziri wa Wizara ya Kilimo Mhe Mary Mwanjelwa katika Mtaa wa Kagwina Kata ya Sinde Jana Januari 2, 2018
Naibu Waziri wa Wizara ya Kilimo Mhe Mary Mwanjelwa akikagua hatua zilizofikiwa katika ujenzi wa Vyumba vya madarasa Shule ya Sekondari Sinde kabla ya kuzungumza na wananchi waliojitokeza kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika katika Mtaa wa Kagwina Kata ya Sinde Jana Januari 2, 2018
Baadhi ya wananchi wakimlaki Naibu Waziri wa Wizara ya Kilimo Mhe Mary Mwanjelwa mara baada ya kuwasili kwa ajili ya Mkutano wa hadhara uliofanyika katika Mtaa wa Kagwina Kata ya Sinde Jana Januari 2, 2018.
Diwani wa Kata ya Manda Mkoani Mbeya Mhe Newton Mwakijobe akitoa salamu za wananchi wa Kata yake kwenye mkutano wa wananchi wa kata jirani ya Sinde kabla ya Naibu Waziri wa Wizara ya Kilimo Mhe Mary Mwanjelwa kuzungumza na wananchi waliohudhuria kwenye mkutano huo Jana Januari 2, 2018
Na Mathias Canal, Mbeya
IMEBAINIKA kuwa tofauti za kiitikadi baina ya madiwani katika Halmashauri nyingi nchini, zimekuwa ni kikwazo kwenye utekelezaji wa miradi ya maendeleo yenye tija kubwa kwa wananchi.
Tofauti hizo zimekuwa chanzo kikubwa katika utekelezaji wa miradi inayobuniwa na Halmashauri husika, au inayoletwa na Serikali Kuu na wafadhili. Mitazamo ya kisiasa, tofauti ya uwakilishi wa vyama na ubinafsi, ndio sababu kuu.
Katika Halmashauri ya Jiji la Mbeya inayoongozwa na Meya na Naibu Meya wanaotokana na vyama vya upinzania hali imekuwa tofauti kwani asilimia kubwa ya madiwani wanaunga mkono juhudi za serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Dkt John Pombe Magufuli tofauti kabisa na Halmashauri zingine.
Akizungumza kwenye mkutano wa hadhara uliohudhuriwa na Naibu Waziri wa Wizara ya Kilimo Mhe Mary Mwanjelwa Jana 2 Januari 2018 uliofanyika katika Mtaa wa Kagwina, Kata ya Sinde Naibu Meya wa Jiji la Mbeya Mhe Fanuel Kyanula ambaye ni Diwani wa Kata ya Sinde alisema kuwa utendaji wa Rais Magufuli ni faida ya watanzania wote hivyo kuna kila sababu ya wananchi kuunga mkono juhudi za serikali yake.
Kyanula alisema kuwa pamoja na kuwa kiongozi anayetokana na chama cha upinzani lakini serikali ni moja hivyo anaungana na wateule wote wa Rais Magufuli katika kutekeleza dhamira ya serikali ya kuwaletea wananchi maendeleo huku akimtaja Naibu Waziri wa Wizara ya Kilimo Mhe Mary Mwanjelwa kama kiongozi wa mfano katika Mkoa wa Mbeya hivyo kuahidi kushirikiana nae kwa karibu.
Naibu Meya huyo amempongeza Naibu Waziri wa Wizara ya Kilimo Mhe Mary Mwanjelwa kwa kuchangia jumla ya mifuko 40 ya saruji kwa ajili ya ujenzi wa vyumba vya madarasa katika shule ya Sekondari Iyera (Mifuko 20) na Shule ya Sekondari Sinde (Mifuko 20) zilizopo Jijini Mbeya.
Alimtaja Mhe Mwanjelwa kwamba amekuwa mwalimu mzuri wa somo la Uraia Mkoani Mbeya akifundisha kuhusu umoja na mshikamano huku akisisitiza kuwa Maendeleo ni dhana pana kwa wananchi na hayapaswi kufanywa kwa mipaka ya vyama vya siasa.
Naibu Waziri wa Kilimo Mhe Mary Mwanjelwa yupo ziarani Mkoani Mbeya ambapo amesifu Uongozi wa Wilaya ya Mbeya kwa kazi kubwa katika utendaji ikiwemo kuanza mchakato wa ujenzi wa vyumba vya madarsa ili kuikabili changamoto ya wingi wa wananfunzi waliofaulu kujiunga kidato cha kwanza Mwaka 2018.

Kaimu Mkurugenzi magonjwa yasiyo yakuambukiza Dkt. Sarah Maongezi akisisitiza jambo mbele ya Waandishi wa Habari (hawapo katika picha) katika kikao kilichofanyika mapema leo katika ukumbi wa Hospitari ya Saratani ya Ocean Road kikihusu tuzo ya Elimu kwa jamii waliopata kutoka Shirikisho la kimataifa la magonjwa yasiyo yakuambukiza mwishoni mwa mwaka katika mkutano wa kimataifa uliofanyika katika falme zakiarabu.
Kaimu Mkurugenzi magonjwa yasiyo yakuambukiza Dkt. Sarah Maongezi akipokea tuzo ya Elimu kwa jamii kutoka kwa Mwenyekiti wa TANCDA Dkt. Tatizo Waane mapema leo katika ukumbi wa Hospitari ya Saratani ya Ocean Road, Wapili kutoka kushoto ni Makamu Mwenyekiti wa TANCDA Andrew Swai.
Kaimu Mkurugenzi magonjwa yasiyo yakuambukiza Dkt. Sarah Maongezi akisisitiza jambo mbele ya Waandishi wa Habari (hawapo katika picha) katika kikao kilichofanyika mapema leo katika ukumbi wa Hospitari ya Saratani ya Ocean Road kikihusu tuzo ya Elimu kwa jamii waliopata kutoka Shirikisho la kimataifa la magonjwa yasiyo yakuambukiza mwishoni mwa mwaka katika mkutano wa kimataifa uliofanyika katika falme zakiarabu, pembeni yake ni Mwenyekiti wa TANCDA Dkt. Tatizo Waane.
………………………………………………………………….
Serikali kupitia Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto yasema kuwa magonjwa yasiyo yakuambukiza yanachangia kiasi kikubwa katika vifo vyote vinavyotokea hapa nchini.
Hayo yamebainishwa na Kaimu Mkurugenzi wa magonjwa yasiyokuwa yakuambukiza Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na watoto Dkt. Sarah Maongezi wakati akipokea tuzo kutoka kwa TANCDA waliopata mwishoni mwa mwaka huu kutoka katika Shirikisho la Kimataifa la Magonjwa yasiyo yakuambukiza.
“Muongeze juhudi katika kupambana na magonjwa hayo ambayo yanachangia asilimia27 ya vifo vyote hapa Tanzania” Alisema Dkt Maongezi.
Dkt Maongezi aliendelea kusema kwamba Serikali imedhamiria kwa nia kabisa katika kupambana na magonjwa haya kwa kuamua kushirikiana na Asasi mbali mbali nchini ili kutimiza azma hiyo ya kupambana na magonjwa haya.
“Serikali pekee yetu hatuwezi na ndio maana tukashirikiana na Asasi kama TANCDA inayojumuisha vyama vingine kama vile, Taasisi ya Saratani, Taasisi ya Magonjwa ya Moyo, Taasisi ya Mfumo wa Hewa na Taasisi ya Kisukari ambazo kwa ujumla zimejenga ushirikiano katika kupambana na magonjwa haya” Aliongeza Dkt. Maongezi.
Aidha Dkt. Maongezi amewahasa TANCDA kuongeza juhudi na kasi zaidi katika kupambana na magonjwa haya ili kuisaidia jamii kubwa ya Watanzania inayoangamia kutokana na kukosa elimu juu ya magonjwa hayo.
Dkt. Maongezi amewashukuru Waandishi wa Habari wote kwa mchango mkubwa wanaoendelea kuutoa katika kuisaidia jamii ya Tanzania hususani katika kupambana na Magonjwa yasiyo yakuambukiza kwa kuandika Makala za magazetini na vipindi vya Redioni na Tv, na kuwahasa kuendelea kufanya kazi hivyo ya kuelimisha jamii kwa juhudi.
Nae Makamu Mwenyekiti wa TANCDA Pro Andrew Swai ametoa wito kwa Asasi hizo kufanya tafiti zaidi katika maeneo mbali mbali bila kusahau vijijini, ili kuweza kufahamu idadi kamili ya watu waliohathirika na maradhi hayo na kurahisisha kufikisha ujumbe katika maeneo hayo.
“TANCDA inatakiwa kujitanua ili waweze kuwafikia watu wote, pia ule ujumbe unaopelekwa uweze kuwafanya watu ili aweze kubadilika”. Alisma Prof. Andrew Swai
Jisajili kwenye:
Machapisho (Atom)