SEKTA BINAFSI YAJIPANGA KUKUTANA NA RAIS KWENYE MKUTANO WA BARAZA LA TAIFA LA BIASHARA - TNBC


WADAU wa Sekta binafsi nchini Jumanne wiki hii, wamefanya mkutano ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya mkutano wao na serikali chini ya jukwaa la Baraza la Taifa la Biashara (TNBC) unaotarajiwa kufanyika Mei 6 mwaka huu.

Mkutano huo wa ndani uliandaliwa na Taasisi ya Sekta binafsi nchini - TPSF ulilenga kuwekana sawa kuhusu namna bora ya kuiwakilisha sekta binafsi katika mkutano huo muhimu, ambao Mwenyekiti wake ni Rais wa Jamhuri ya Tanzania Dr. John Pombe Magufuli.

Akiwakaribisha wadau wa Sekta Binafsi katika kikao hicho cha maandalizi Mwenyekiti wa TPSF Dk. Reginald Mengi alisema Serikali na Sekta Binafsi hawakomoani, ndio maana TPSF inahimiza wafanye kazi kwa pamoja ili kulifikisha taifa kwenye uchumi wa viwanda.

Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Sekta Binafsi nchini (TPSF), Godfrey Simbeye akitoa neno la ukaribisho kwa wadau wa Sekta Binafsi kwenye mkutano wa ndani ulioambatana na chakula cha jioni kilichoandaliwa na TPSF katika hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam. Wa pili kulia ni Mwenyekiti wa Taasisi ya Sekta Binafsi nchini (TPSF), Dk. Reginald Mengi.

Dk Mengi pia alisema serikali na sekta binafsi wana malengo yanayofanana ya kutokomeza umaskini na kutengeneza ajira kwa wananchi, jambo ambalo linaweza kutekelezeka kwa urahisi iwapo kutakuwa na ushirikiano wa karibu baina ya serikali na Sekta Binafsi.

Katibu Mtendaji wa TNBC Mhandisi Raymond Mbilinyi alisema mkutano huo utakuwa ni fursa nzuri kwa serikali na sekta binafsi kubadilishana mawazo kuhusu wajibu wa kila upande katika kuboresha mazingira ya biashara na uzalishaji nchini ili kukuza uchumi wa nchi.
Mkurugenzi Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) Roberto Jarrin akijitambulisha katika mkutano huo.
Mwenyekiti wa Taasisi ya Sekta Binafsi nchini (TPSF), Dk. Reginald Mengi akizungumza na wadau wa Sekta Binafsi katika mkutano ulioambatana na hafla ya chakula cha jioni uliofanyika kwenye hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam. Wa pili kulia ni Katibu Mtendaji wa Baraza la Taifa la Biashara (TBNC), Mhandisi Raymond Mbilinyi.
Mwenyekiti wa Taasisi ya Sekta Binafsi nchini (TPSF), Dk. Reginald Mengi akiendelea na mazungumzo na wadau wa Sekta Binafsi kwenye mkutano huo ulioambatana na chakula cha jioni katika hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam.
Katibu Mtendaji wa Baraza la Taifa la Biashara (TBNC), Mhandisi Raymond Mbilinyi akifafanua jambo katika mkutano wa ndani ambao ni sehemu ya kujiandaa kukutana na serikali chini ya Baraza la Taifa la Biashara (TBNC) linalotarajiwa kufanyika mwanzoni mwa mwezi Mei jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti wa Taasisi ya Sekta Binafsi nchini (TPSF), Dk. Reginald Mengi akiteta jambo na Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Sekta Binafsi nchini (TPSF), Godfrey Simbeye wakati mkutano huo ukiendelea.
Mkutano ukiendelea.

RC GAMBO AZINDUA BARABARA ARUSHA,AKAGUA MIRADI MBALIMBALI YA MAENDELEO , SAMBAMBA NA KUZUNGUMZA NA WANANCHI KUSIKILIZA KERO ZAO

Mkuu wa mkoa wa Arusha Mrisho Gamboa akiwa ameshika mkasi ishara ya kukata utepe katika uzunduzi wa barabara ya St.James na Mahakamani leo Jijini Arusha,Kulia kwake ni mkuu wa wilaya ya Arusha mjini Gabriel Daqarro.Picha zote na Mahmoud Ahmad.

 Watoto wenye ulemavu kutoka shule ya msingi Meru wakiimba wimbo wa Taifa kama picha hapo juu inavyoonekana wakiongozwa na mwalimu Neema Lema ,na hii inayofuata hapa chini wakiongozwa na mtafsiri na mwalimu Viola Wilson .
 Mkuu wa Mkoa wa Arusha akiangalia kwa makini kile ambacho mtoto mwenye ulemavu Amina kutoka shule ya msingi Meru akitumia kompyuta katika kuhariri video aliyoichagua,aliyeshika kipazasauti ni mtaalam wa masomo ya Tehama katika kitengo cha walemavu bi.Betha Denis.
 

Na.Mahmoud Ahmad,Arusha.

Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mrisho Gambo amtembelea na kujionea mradi wa darasa la watoto wenye ulemavu  katika shule ya msingi Meru iliyopo Jijini hapa. 

Akiwa katika shule hiyo yenye jumla ya wanafunzi 68 miongoni mwao wasichana wakiwa 34 na wavulana 28 huku walimu viziwi wakiwa wawili na mtaalam mmoja wa kitengo cha I. C. T, Gambo alijionea mwenyewe jinsi wanafunzi hao wanavyofanya kazi kwa kutumia teknolojia hiyo. 

Akisoma risala mbele ya Mkuu huyo wa mkoa  mwalimu Musa Lwambano alisema shule hiyo unajumla ya walimu 42 ambapo walimu 15 ni wa kitengo na 27 wa shule ya kawaida huku idadi ya wanafunzi ikiwa ni 1,384 wavulana wakiwa ni 709 na wasichana wakiwa ni 675

Amesema shule hiyo inawafadhili kutoka nchi ya  Finland walioshirikiana na Halmashauri ya Jiji la Arusha lililotoa Sh, milioni 20 na wafadhili wakichangia zaidi ya sh, milioni 180  huku fedha hiyo ikisaidia kujenga jengo bora la ICT na kununua vifaa kama kompyuta mpakato (laptop) 184,deskitopu 5,Projekta 6,Sola 14,Scana Kamera 4,Ipad 22, Mashine ya Laminationi na printa 4.

Pia vijana viziwi wanne wamepata ajira katika kitengo hicho hukuwakimshukuru Mkurugenzi wa Jiji la Arusha, Athumani Kihamia kwa kuwawezesha kupata maendeleo hayo shuleni hapo

Gambo alimpongeza walimu na wanafunzi wa shule hiyo kwa kutoa elimu kwa wanafunzi wenye ulemavu na kuwasihi walimu kuongeza juhudi za kutoa elimu kwa wanafunzi hao ili waweze kupata ajira na kujikwamua kiuchumi 

Awali Rc Gambo alijionea jinsi wanafunzi hao viziwi wakiimba wimbo wa Taifa kwa kutumia alama zao wakiongozwa na walimu wao ambao ni Veola Wilson na Neema Lema 

Gambo anaendelea na ziara yake ya siku tano Jiji hapa kwa kuzindua miradi mbalimbali ikiwemo uzinduzi wa barabara ya Mahakama na St, James uliogharimu Sh milioni 586. pamoja na kuzungumza na wananchi ili kutatua kero zao
 Gambo amewaagiza watumishi wa  jiji la Arusha wakiwemo wataalam wa vitengo mbalimbali  kuhakikisha wanatatua kero za wananchi haraka iwezekanavyo ili kuondokana na kero zinazowakabili.
 Miradi iliyokaguliwa ni pamoja   na  Visima viwili  vya maji vilivyoko magereza vilivyogharimu milioni 372, madarasa 6 Shule ya msingi Olasity,madarasa 4 ya Shule ya msingi Burka Estate ambayo yamegaharimu jumla ya  shilingi 218 milioni .

MAJALIWA AFUNGUA KONGAMANO KUHUSU MMONYOKO WA MAADILI


Z
Kamishina Jenerali wa Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za kulevya, Nchini, Rogers Siyanga akizungumza katika Kongamano kuhusu Mmonyoko wa Maadili lililoandaliwa na Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (BAKWATA) na kufunguliwa na Waziri Mkuu, kassim Majliwa kwenye Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius, kambarage Nyerere jijini Dar es salaam Aprili 24, 2017.
Z 1
  Mufti na Sheikh Mkuu wa Tanzania, Alhaji Abubakary Zuberi akizungumza katika Kongamano kuhusu Mmonyoko wa Maadili lililoandaliwa na Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (BAKWATA) na kufunguliwa na Waziri Mkuu, kassim Majliwa kwenye Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius, kambarage Nyerere jijini Dar es salaam Aprili 24, 2017.
Z 2
Naibu Waziri wa nchi, Ofisi ya Rais TAMISEMI, Selemani Jafo akizungumza katika Kongamano kuhusu Mmonyoko wa Maadili lililoandaliwa na Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (BAKWATA) na kufunguliwa na Waziri Mkuu, kassim Majliwa kwenye Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius, kambarage Nyerere jijini Dar es salaam Aprili 24, 2017.
Z 3
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akifungua Kongamano kuhusu Mmonyoko wa Maadili lililoandaliwa na Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (BAKWATA) kwenye Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius, kambarage Nyerere jijini Dar es salaam Aprili 24, 2017. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

RAIS DR,MAGUFULI AWASILI DODOMA KWA SHEREHE ZA MUUNGANO


unnamed
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Jordan Rugimbana mara baada ya kuwasili mkoani Dodoma.
A
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Jordan Rugimbana mara baada ya kuwasili mkoani Dodoma.
A 1
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa mara baada ya kuwasili mkoani Dodoma.
A 2
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Job Ndugai mara baada ya kuwasili mkoani Dodoma.
A 3
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi ya Chama cha Mapinduzi Abdallah Bulembo mara baada ya kuwasili mkoani Dodoma.
A 4
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisaini kitabu cha Wageni mara baada ya kuwasili mkoani Dodoma. Pembeni yake ni Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Job Ndugai.
A 5
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa pamoja na Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Job Ndugai mara baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa Dodoma. PICHA NA IKULU

MAJALIWA ATEMBELEA UWANJA WA JAMHURI MJINI DODOMA KUKAGUA MAADALIZI YA SHEREHE ZA MUUNGANO


Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizngumza baada ya kutembelea na kukagua maadalizi ya uwanja wa Jamhuri mjini Dodoma Aprili 24, 2017. Katikati ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Jenista Mhagama na kushoto ni Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu, Dkt.Hamisi Mwinyimvua. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akimsikiliza Bw.Yusto Chuma (kulia) ambaye ni mmoja wa wajumbe wa kamati ya Maandalizi ya Sherehe za Muungano wakati alipotembelea uwanja wa Jamhuri mjini Dodoma zitakapofanyika sherehe hizo ili kujionea maandalizi hayo, Aprili 24, 2017. Kushoto kwake ni Waziri wa nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Jenista Mhagama . (Picha na Ofisi ya ` Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akimsikiliza  Bw.Yusto Chuma (kulia) ambaye ni  mmoja wa  wajumbe wa kamati ya Maandalizi ya  Sherehe za Muungano wakati alipotembelea uwanja wa Jamhuri mjini Dodoma Aprili 24, 2017 zitakapofanyika sherehe hizo.  Kushoto kwake ni  Waziri wa nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Jenista Mhagama na Kulia ni Naibu Waziri wa nchi, Ofisi ya Rais TAMISEMI, Selemani Jafo. (Picha na Ofisi ya ` Waziri Mkuu)

JIMBO LA ARKANSAS LATEKELEZA ADHABU YA KIFO KWA WAFUNGWA WAWILI


Jimbo la Arkansas limewatekelezea adhabu ya kifo wafungwa wawili kwa siku moja waliohukumiwa adhabu ya kifo baada ya Mahakama ya Juu kukataa pingamizi lao la dakika za mwisho.

Wafungwa hao Jack Jones na Marcel Williams wote walihukumiwa adhabu ya kifo kwa makosa ya ubakaji na mauaji waliyoyatenda katika miaka ya 1990.

Jimbo la Arkansas limepanga kutekeleza adhabu ya kifo kwa watuhumiwa nane baada ya kubaini kuwa dawa ya sindano wanayotumia kuulia inaisha muda wake wa matumizi mwisho wa wezi huu.

Hii ni mara ya kwanza kutekelezwa kwa adhabu ya kifo kwa wafungwa wawili katika siku moja tangu kupita miaka 17 nchini Marekani.

                                         Kitanda maalum kwa ajili ya kutekelezea adhabu ya kifo

MKUU WA WILAYA YA KISHAPU AFANYA ZAIARA KATA YA MASANGA NA KUZUNGUMZA NA WANANCHI, APIGA MARUFUKU UUZAJI WA CHAKULA


Mkuu wa Wilaya Kishapu mkoani Shinyanga, Nyabaganga Taraba amepiga marufuku wananchi kuuza mazao ya chakula wanayovuna hususan mtama na badala yake waweke akiba. 

Taraba alipiga marufuku hiyo jana wakati akifanya ziara katika kata za Lagana, Mwamashele, Mwakipoya na Masanga baada ya kubaini kuwepo kwa baadhi ya wananchi kufanya biashara hiyo. 

Akizungumza kwenye mkutano wa hadhara katika kata ya Masanga alisema kuna baadhi ya watu huwahadaa na kununua mtama kwa bei ya juu hali inayowafanya wananchi wabaki bila chakula. 

“Nasikia hapa kuna baadhi watu wanapita kwenu wananchi na kununua debe moja la mtama kwa shilingi elfu ishirini na tano msidanganyie na kuuza wewkeni akiba,” alisisitiza mkuu huyo wa wilaya. 

Aidha alionya tabia ya baadhi ya watu kuuza mazao yakiwa shambani baada ya kukadiriwa kiasi cha mazao yao kabla ya kuyavuna aliwataka wananchi wakatae kufanya hivyo. 

Kwa upande mwingine aliwataka kuandaa mashamba yao mapema na kupanda mazao yanayohimili ukame yakiwemo mtama ili yaweze kustawi na kuwapa chakula. 

Taraba aliwataka wananchi hao kuwatumia wataalamu wa kilimo kwenye kata zao ili kupata ushauri wa kutumia mbegu zilizo bora ambazo zinaweza kuota na kukua kwa haraka.
Mkuu wa Wilaya ya Kishapu, Nyabaganga Taraba (katikati) akizungumza na wananchi (hawapo pichani) katika mkutano wa hadhara kata ya Masanga. kulia ni Afisa Kilimo (Ubora wa mbegu), Maduhu Masunga 
Mkuu wa Wilaya ya Kishapu, Nyabaganga Taraba (katikati) akizungumza na wananchi (hawapo pichani) katika mkutano wa hadhara kata ya Masanga. Wengine pichani kulia ni Afisa Kilimo (Ubora wa mbegu), Maduhu Masunga na Mwenyekiti wa kijiji cha Masanga, Gambishi Malele. 
Mwananchi wa kata ya Masanga akitoa kero yake kwa Mkuu wa Wilaya, Nyabaganga Taraba wakati wa mkutano wa hadhara. 
Mkuu wa Wilaya ya Kishapu, Nyabaganga Taraba akizungumza na wajumbe aliowakuta wakifanya kikao cha kujadili maendeleo ya kata, Mwamashele alipokuwa katika ziara ya kutembelea kata tatu. 
Mwananchi wa kata ya Masanga akitoa kero yake kwa Mkuu wa Wilaya, Nyabaganga Taraba wakati wa mkutano wa hadhara. 
Mkuu wa Wilaya ya Kishapu, Nyabaganga Taraba akizungumza na wananchi wa kata ya Masanga katika mkutano wa hadhara. Wengine pichani ni kuanzia kushoto ni Afisa Tawala wa Ofisi ya Mkuu wa Wilaya, Juvenalis Beyakwasho, Mtendaji Kata wa Masanga, John Zablon, na Mwenyekiti wa kijiji cha Masanga, Gambishi Malele. 
Mkuu wa Wilaya ya Kishapu, Nyabaganga Taraba akizungumza na wananchi wa kata ya Masanga katika mkutano wa hadhara. Wengine pichani ni kuanzia kushoto ni Afisa Tawala wa Ofisi ya Mkuu wa Wilaya, Juvenalis Beyakwasho, Mtendaji Kata wa Masanga, John Zablon, na Mwenyekiti wa kijiji cha Masanga, Gambishi Malele.