BASHE KUZINDUA MAONESHO YA TANZFOOD EXPRO 2022

Na Ahmed Mahmoud Watanzania wametakiwa kuzalisha bidhaa za Kilimo zinazoendana na masoko ya kimataifa ili kuweza kujingezea kipato na kukamata masoko hayo ya kimataifa Aidha Waziri wa Kilimo Husein Bashe anatarajiwa kuwa mgeni Rasmi katika maonesho ya kimataifa ya kilimo TanzFood Expro 2022 yenye kibwagiz mbiu Ladha ya Tanzania. Akizungumza na waandishi wa habari katika makao makuu ya EAC Jijini Arusha Mkurugenzi wa sekta ya uzalishaji ndani ya Jumuiya ya Afrika masharika Jean Baptiste amesema maonyesho hayo yatafanyika kwa siku tatu kuanzia tarehe 11 hadi 13. Amesema kwa siku tatu watatumia kujenga mtandao wa kibiashara katika mazingira ya kitaalamu na kwamba sekta hii ya kilimo sio kwa ajili ya Tanzania Pekee ndio maana kama Eac na KiliFair Promotion tumeungana ili nchi wanachama wa jumuiya ya Afrika mashariki tutoke na bidhaa zilizo bora. "Bidhaa bora zinahitajika sana ili kuweza kutangaza katika maonyesho haya kutoka kote katika jumuiya itasaidia kuongeza tija ya kuzalisha bidhaa zenye ubora wa kimataifa". Awali Mkrugenzi wa Kilifair Dominic Shoo Alisema kuwa maonesho ya kilimo TanzFood pia yatazinduliwa na Balozi wa Ujerumani nchini Regine Hess na Waziri wa Kilimo Husein Bashe na kuyaleta pamoja makampuni 120 ya hapa nchini na nchi za Eac. Alisema kuwa wanayofuraha kuona waonyeshaji wa ndani na nje ya nchi kutoka masoko mengine kuja kuangalia bidhaa zetu huku akiyataka makampuni ya mbegu na Mashine za kilimo kuleta bidhaa zao katika maonyesho. Kwa Upande wake Mkurugenzi Mwenza wa Kilifair Tom Kunkler alisema kuwa maonesho hayo washiriki watapata fursa ya kupata mafunzo ya kilimo na uzalishaji wa bidhaa ili waweze kushindana katika soko la kimataifa. Alisema kuwa mafunzo hayo kwa wakulima yatawasaidia kuongeza ubora na maendeleo katika sekta ya kilimo ambapo kauli mbiu yake ni Ladha ya Tanzania.

WAZIRI DKT MABULA ATAKA UWAJIBAKI KWA MAKAMISHNA WA ARDHI KUFIKIA MALENGO YA WIZARA

Na Ahmed Mamoud Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula amewataka Makamishna Wasaidizi wa Ardhi wa mikoa nchini kuwajibika na kutumia wajibu wao katika kutekeleza mikakati ya Wizara kufikia malengo. Aidha, amewataka Makamishna hao kuwapangia majukumu kwa malengo maafisa walio chini yao na kufuatilia kazi wanazowapa mara kwa mara. Dkt Mabula amesema, hayo tarehe 25 Februari 2022 wakati akifungua kikao kazi cha Menejiment na Makamishna wa Ardhi Wasaidizi wa mikoa kilichofanyika ofisi ya Mkuu wa mkoa wa Arusha. ‘’Yapo malamiko ya lugha zisizofaa kwa wateja, hii haikubaliki fuatilieni hili na kulikemea vikali na kuzingatia misingi na kanuni za utumishi wa umma katika majukumu yenu ya kila siku ’’ alisema Dkt Mabula. Aidha, aliwataka katika utekelezaji mpango mkakati wa wizara wanazingatia vipaumbele vya serikali hususan maelekezo ya mhe. Rais Samia Suluhu Hassan na ukusanyaji wa maduhuli ya serikali kupitia kodi ya pango la ardhi. Akigeukia suala la makusanyo ya kodi ya pango la ardhi, Waziri wa Ardhi aliwataka Makamishna wa ardhi Wasaidizi wa mikoa kuwa wabunifu katika njia za kukusanya mapato. ‘’Sula la mtandao kutopataikana muda mwingi linaonekana kuwa kikwazo katika ukusanyaji maduhuli, lifanyieni kazi’’ alisema Dkt Mabula. Waziri Dkt Mabula pia alihimiza kuongezwa kwa kasi ya umilikishaji ardhi na kuwataka Makamishna hao na wakuu wa idara katika wizara kuweka malengo kwa kila ofisa mwenye taaluma ya ardhi kuandaa hati. Kwa upande wake Katibu Mkuu Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Allan Kijazi alisema baada ya kuteuliwa alifanya ziara katika baadhi ya mikoa na kukutana na baadhi ya changamoto alizozitaja kuwa ni pamoja na kutofikiwa malengo ya ukusanyaji kodi ya ardhi pamoja na baadhi ya halmashauri kutohudumia idara za ardhi kwa madai ya idara hizo kuhamishiwa wizarani. ‘’Nimeanza kuchukua hatua ili kutatua changamoto hizo ambapo tayari nimetoa maagizo mbalimbali kwenye mikoa na menejimenti ya wizara na ni matarajio kikao kazi kutaibua suluhisho la changamoto hizo’’ alisema Dkt Allan Kijazi. Kwa mujibu wa Dkt Kijazi, Wizara ya Ardhi imekuwa ikinyooshewa vidole na wananchi kwa masuala ya ukiukwaji wa haki za wananchi na kuchafua taswira ya Wizara na kutaka watendaji wa sekta ya ardhi kujitafakari na kujisahihisha kwa kutimiza wajibu ili kuondoa dhana hiyo. Aligusia pia mpango wa urasimishaji makazi holela na kueleza kuwa, ni matarajio yake kupitia kikoa hicho washirikia wataibuka na mkakati wa uelekeo wa wizara katika kupanga miji sambamba na usimamamia fedha zilizotolewa kwa ajili ya mpango wa kupanga, kupima na kumilikisha ardhi maarufu kama KKK.

MASHINDANO SED MISS VALENTINE'S 2022 KUFANYIKA KESHO

Mashindano ya Sed Miss Valentine's 2022 yatafanyika kesho februari 14 mwaka 2022 Mjini Babati Mkoani Manyara huku warembo 15 wanatarajiwa kuchuana vikali kutwaa taji hilo. Afisa Masoko wa Kiwanda cha Mati Super Brand Gwandumi Mpoma ambao ndio wadhamini wakuu wa mashindano hayo wamesema kuwa wamejipanga kuhakikisha wakazi wa Babati wanafurahia mashindano hiyo amewataka wajitokeze kwa wingi. Gwandumi amesema kuwa Mashindano hayo yanalenga kuibua vipaji vya vijana na kuwapa fursa ya kufanya kazi na kiwanda hicho kupitia bidhaa mbali mbali wanazozalisha ikiwemo Strong Gin,Sed Pinepale na Tanzanite Premium Vodka. Hamisi Saidi ni Moja kati ya waandaaji wa Mashindano ya Sed Miss Valentine amesema kuwa warembo wamejiandaa vizuri katika kambi hiyo na wanatarajia ushindani utakua mkali kutokana na maandalizi waliyoyafanya. wa Upande wao washiriki wa Mashindano hayo Jenifer Paulo Mmari na Keithwin Pallangyo wamepongeza udhamini wa kampuni ya Mati Super Brands Limited kwa kuwawezesha kukaa kambini na kujiandaa vyema hivyo wamewataka wakazi Mkoa wa Manyara na Mikoa jirani kujitokeza kwa wingi.

SERIKALI YARIDHISHWA NA UWEKEZAJI KWENYE VIWANJA VYA NDEGE TBA

Na Ahmed Mahmoud Arusha SERIKALI imeridhishwa na utekekezaji wa miradi miwili ya maendeleo ya ujenzi wa Jengo la ghorofa kumi la nyumba za kuishii watumushi wa serikali lililopo mkabala na jengo la Uhamiaji mkoa pamoja na uboreshaji wa uwanja wa ndege wa Arusha.. Naibu waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Mwita Waitara, ameyasema hayo ilipohitimisha ziara yake ya siku moja ya kutembelea miradi hiyo,iliyotanguliwa na Waziri huyo kufanya kikao na watumishi wa serikali kwenye ukumbi wa benki kuu. Kwenye mradi wa ujenzi wa Jengo la ghorofa kumi linalomilikiwa na linalijengwa na wakala wa majengo nchini TBA,Waitara,ameipongeza wakala huyo na kuagiza kuwa kipaumbele cha watu watakao ishi ndani ya jengo hilo iwe ni watumishi wa serikali. Alisema kukamilika kwa ujenzi wa Jengo hilo kutaongeza mapato ya serikali na uhitaji wa majengo ya kuishi watumushi ni mkubwa mno hivyo Jengo hilo litaiwezesha TBA,kujiendesha kibiashara . Alisema wizara imeshaagiza wastaafu ikiwemo wabunge waliomaliza muda wao kuondoka kwenye nyumbaza serikali zilizopo Dodoma ili kuwezesha watumishi wengine kupata nyumba za kuishi. Akiwa kwenye uwanja wa ndege wa Arusha,Waziri Waitara,ameridhishwa na hatua za uboreshaji wa uwanja huo uliofanywa na mamlaka ya viwanja vya ndege nchini,na kusema kuwa serikali Imetoa fedha nyingi kwa ajilj ya miradi hiyo. Alisema kukamilika kwa ukarabati huo unahusisha kuongeza Urefu wa uwanja eneo la kurukia ndege kutaongeza ndege nyingi kutua uwanjani hapo na mapato nayo yataongezeka.kwani uwanja huo ni rafiki kwa watalii na wananchi wa mkoa wa Arusha Alisema jumla ya viwanja kumi na moja nchini vitafanyiwa marekebisho na uboreshaji katika bajeti ya mwaka huu na serikali sasa inafungua njia za uchumi kwa kuimarisha miundo mbinu ya barabara,reli,ndege na Mali kwa wizara hiyo ni wezeshi kufikia malengo ya kiuchumi. Kwa upande wake meneja wa uwanja wa ndege wa Arusha,Mhandisi Eliud Tesha,alisema mradi wa ukarabati na maboresho ya uwanja huo yanahusisha eneo la maegesho ya ndege na kuruka ,maegesho ya magari,eneo la kurukia ndege na miradi hiyo iliyotekelezwa ambayo imekamilika mwaka jana. Ameongeza kwamba mamlaka ya viwanja vya ndege nchini ina mpango wa kujenga jengo lingine la kisasa uwanjani hapo.la kufikia wageni kwa lengo la kuendelea kuongeza wigo mpana kwa abiria wanaofika kusafiri ndani ya uwanja huo.

DC DAQARRO ATAKA WADAU WA ELIMU KUHAKIKISHA MPANGO WA LANES UNAENEA ARUSHA NA KULETA MATOKEO CHANYA

Mkuu wa wilaya Arusha mjini Gabriel Daqarro akifungua wiki ya usomaji iliyofanyika kwenye maktaba ya mkoa Arusha pembeni ni mkutubi mkuu wa maktaba hiyo Bi Rafiki Mvamba na kushoto ni Afisa elimu Vielelezo Godfrey Augustino wakifuatilia hotuba ya mgeni rasmi mkuu huyo wa wilaya picha zote na mahmoud ahmad arusha 

Afisa elimu Vielelezo Godfrey Augustino akitoa hotuba kwenye ufunguzi wa wiki ya usomaji Lanes kabla ya kumkaribusha mgeni rasmi mkuu wa wilaya ya Arusha Gabriel Daqarro picha na mahmoud ahmad arusha

Meza kuu wakiwa wanajadiliana mkuu wa wilaya na mkutubi mkuu wa maktaba bi Rafiki Mvamba ambapo afisa elimu akiendelea kutoa hotuba yake kabla ya kumkaribisha mgeni rasmi

Pichani juu na chini ni sehemu ya wanafunzi wa shule sita za wilaya ya Arusha walioshiriki mashindano mbali mbali ya kusoma kuandika na kuhesabu wanaoonekana pichani ni wanafunzi wa shule ya msingi Mwangaza na sombetini  wakifuatilia kwa makini matukio mbali mbali yalioendelea kwenye hafla hiyo


MAONYESHO YA VITABU MBALI MBALI NAYO YALIKUWEPO KWENYE WIKI YA USOMAJI KATIKA JIJI LA ARUSHA ILIYOADHIMISHWA KWENYE MAKTABA KUU YA MKOA WA ARUSHA

Mwanafunzi wa shule ya Msingi Uhuru Jaquline Abrogast akisoma kitabu mbele ya mkuu wa wilaya kwenye maadhimisho ya siku ya Usomaji iliyoadhimishwa kimkoa kwenye maktaba ya mkoa jijini Arusha


Picha juu ni igizo la wanafunzi wa shule ya msingi Naura wakionyesha masuala mbali mbali ya safari ya kusoma kwenye maonyesho ya wiki ya usomaji mbele ya mgeni rasmi mkuu wa wilaya ya Arusha

Wanafunzi wa shule ya msingi Arusha School wakiimba wimbo mbele ya mgeni rasmi mkuu wa wilaya ya Arusha

Mkutubi mkuu wa maktaba ya mkoa akiwa na majaji wenzake wakifuatilia mashindano ya kusoma kwa wanafunzi wa shule sita za Naura,Sombetini,Meru,Mwangaza,Uhuru na Arusha School

Baadhi ya wanafunzi wakioshiriki mashindano ya kusoma vitabu wa darasa la kwanza wa shule hizo sita zilizoshiriki maadhimisho hayo ya wiki ya Usomaji
Na Ahmed Mahmoud Arusha
Mkuu wa wilaya ya Arusha Gabriel Daqarro amewataka waalimu na Afisa elimu kuhakikisha mpango wa KKK (LANES) unatiliwa mkazo sanjari na kuhakikisha wanafunzi wanajua kusoma kuandika na kuhesabu ili kuleta matokeo chanya na kufikia malengo ya serikali ya wananchi wote kujua kusoma.
Akiongea wakati akifungua wiki ya kusoma na stadi za kukuza kusoma kuandika na kuhesabu (LANES) iliyofanyika katika Maktaba ya mkoa Dc Daqarro amesema kuwa wajibu huo ni wetu sote kuanzia nyumbani hadi mashuleni kuhakikisha kila moja wetu anatimiza wajibu wake.
Amesema kuwa wiki kama hiyo ni ya kujitathmini tumefika wapi na tunaelekea wapi kama taifa kwa ajili ya kukuza uelewa wa vijana wetu kujua kuhesabu kusoma na kuandika ili kuwa na taifa linalopiga hatua kwa wananchi wake kujua kusoma.
“Taifa limejipanga kuondoa  wananchi wasio jua kusoma na kuandika ndio maana ilikaja na mkakati wa kkk hivyo kila mmoja wetu anawajibu kuhakikisha tunafikia malengo ya mkakati huu”alisema Daqarro
Kwa Upande wake Afisa elimu vielelezo Godfrey Augustino amesema kuwa wajibu wa wazazi ni kufuatilia maendeleo ya watoto wao na wao kama waalimu watahakikisha kila kijana anayepata nafasi anajua kusoma kuandika na kuhesabu lengo ni kuondoa vijana wanaomaliza elimu wakiwa hawajui kusoma na kuandika.
Amesema kuwa hatavumilia kuona wilaya hiyo ikiwa ina vijana ambao hawajui kusoma wala kuandika na amejipanga kuhakikisha wanafikia malengo yalioanza kuonekana kwenye ufaulu kwa wilaya kushika nafasi ya kwanza kitaifa katika ufaulu wa Darasa la saba mwaka huu.
Awali mkutubi mkuu wa maktaba ya mkoa Rafiki Mvamba amesema kuwa analishukuru shirika Kwa kufadhili wiki hiyo na kuwataka watanzania kupenda kujisomea na kufuatilia watoto wao ili kujua kusoma na kuandika itakayopelekea taifa kuwa na wananchi wenye elimu ya kuweza kufikia malengo endelevu
Amesema kuwa mpango huo LANES wa wiki ya kusoma ni kujitathmini na kuwafikia wanafunzi kujua uelewa wao katika kukuza stadi za kusoma kuandika na kuhesabu kuanzia watoto wa awali hadi vyuo vikuu kupenda kujisomea kwani elimu haina mwisho.
“sisi kama maktaba tumejipanga kuhakikisha wanafunzi wote wanaofika hapa wanapata vitabu vyote wanavyohitaji sanjari na kuwapa nafasi na kuwaongoza pale wanapohitaji ili lengo ya kuwa na taifa lenye watu wanaojua kusoma na kuandika linafikiwa”alisema Mvamba
Mwisho………………


TCCIA LONGIDO SACCOS WAITAKA SERIKALI KUSIMAMIA SUALA LA ELIMU KWA VYAMA VYA USHIRIKA NCHINI

Afisa ushirika wilaya ya Longido Japhet Mambo akisisitiza jambo wakati akiongea na wanachama wa TCCIA Longido Saccos Ltd ambapo kushoto ni Mwenyekiti wa TCCIA wilaya hiyo Abduraman Konje akifuatalia mkutano huo na kulia ni Mshauri kutoka Shirika la Trias Julius Mlambo akifuattilia picha zote na mahmoud ahmad wa globu ya jamii Longido

Juu na chini ni sehemu ya wanachama wa saccos ya TCCIA wilayani Longido wakiwa katika mkutano wao wa mwaka wakifuatilia vipengele vya Agenda za mkutano huo picha na mahmoud ahamad longido


Meza kuu wakifuatilia mkutano huo kushoto ni makaumu wa mwenyekiti wa saccos hiyo akifuatiwa na mtendaji wa kata ya Namanga akifuatiwa na mwenyekiti wa Longido Saccos Abdulrahman Konje na Afisa Ushirika na mwisho kabisa ni mshauri wa vikundi kutoka shirika la TRIAS Julius Mambo

Vijana nao walikuwemo kama sehemu ya mkakati wa serikali kuweza kutengeneza uchumi wa kati wa viwanda vijana ndio nguvu kazi ya taifa lolote kufikia malengo kaama walivyokutwa na kamera ya matukio

Wanachama wakisoma taarifa za kikao hicho hatua kwa hatua katika mkutano huo

Mwenyekiti wa mkutano huo David Wiliam na makamu wake Adela Magani wakisikiliza taarifa ya mapato na matumizi ikisomwa

Wanachama hawakuwa nyuma kufuatilia hatua kwa hatua taarifa ya mapato ya chama chao


Wananchama juu na chini wakifuatilia kikao hicho ambapo waliibua mambo mengi ya kuweza kusaidia kukuza chama chao


Na Ahmed Mahmoud Longido
Vyama vya Ushirika nchini vimetakiwa Kutenga muda wa kutoa elimu kwa wananchama wao lengo likiwa kujua faida za vyama hivyo pamoja na kuweka akiba na kukopa ili kuweza kuwafikia wanachama wengi zaidi hapa nchini kukuza vipato vyao sanjari na kujiwekea akiba na hisa.
Akifungua mkutano mkuu wa mwaka na wa pili wa TCCIA Longido Saccos Mwenyekiti wa Tccia wilaya ya Longido Abrahaman Konje ameitaka serikali kutambua suala la elimu ya uwekaji akiba na uwekaji wa amana kwa watanzania suala ambalo wengi wao bado hawana elimu hiyo.
Amesema kuwa Tatizo hilo ndio maana vyama vingi vya ushirika vimekuwa vinaende kwa kusuasua jambo ambalo sio zuri na linaleta ukakasi kwa wanachama katika juhudi zao za kufikia kuwa na vyama vikubwa hapa nchini vitakavyosaidia maendeleo ya nchi na kuongeza vipato.
“Tatizo hapa nchini wanachama wengi hawana uelewa mkubwa wa masuala ya kujiwekea akiba na Amana(HISA) hivyo kujikuta wanashindwa kutofautisha vicoba na saccos kwa kushindwa kujiletea faida na kuendesha familia kwa kujiwekea amana ili kuweza kuweka na kuwasaidia kusomesha watoto wao na kujiendesha maisha”alisisitiza Konje.
Aidha Kwa Upande wake Afisa ushirika wilaya ya Longido Japhet Mambo amewataka wataalamu wenzake kuhakikisha wanatenga muda mwingi kuvifikia vikundi kwa ajili ya kutoa elimu ya vyama vya ushirikia kwani amegundua vyama vingi wanachama vijijini hawana uelewa hivyo sasa ni ndio muafaka sanjari na kuifafanua sheria namba sita ya mwaka 2013 ya vyama vya ushirika.
Amesema kuwa wengi wa wanachama wa vyama vya ushirika wamekuwa wanashindwa kutofautisha vicoba na saccos na faida zake kwa jamii hususani kuweka akiba na amana jambo hilo limechangia kuwepo mapungufu mengi katika vyama vya ushirika hapa nchini.
Awali akisoma taarifa kabla ya kumkaribisha  mgeni rasmi Mwenyekiti wa TCCIA Longido Saccos Ltd Flora Swai amesema kuwa chama hicho kina jumla ya wanachama 147 ambapo kina mtaji wa kiasi cha tsh.14 milion na kuwataka  wanachama wenzake kuhakikisha wanajiwekea hisa ili kuweza kufikia malengo ya chama chao.
Amesema kuwa kuanzia mwakani wataweka utaratibu wa kuwapongeza wanachama watakaofanya vizuri na kuitaka serikali kuwafikia vyama vya ushirika hapa nchini kuweza kutoa elimu ya uwelewa kwa wanachama wa saccos mbali mbali ili ziwe na tija na kuongeza pato la mwananchi na taifa kwa ujumla.
“Nawasihii wanachama wenzangu kujiwekea amana na kupenda kuuliza ili kuweza kujiletea maendeleo ambapo wengi  wamekuwa pindi kunapotolewa wito wavikao wanashindwa kufikia viwe vya serikali ama vya ushirika nawaomba muwe na moyo wa kuitikia wito pindi unaposikia na sio kupuuzia wito”alisisistiza Swai
Mwisho…………………………………………………………..





Mwili Mwingine Waonekana Ukielea Ajali Mv Nyerere tanzia



Mwili mmoja wa mtoto umepatikana saa nne asubuhi hii, wakati wazamiaji wakiweka sehemu ya chini Maputo (boya) yanayojazwa upepo ili kukiinua kivuko cha MV Nyerere, eneo la Bwisya kisiwani Ukara, jijini Mwanza.
Kazi ya kukinyanyua kivuko hicho  kilichozama Alhamisi iliyopita na kusababisha vifo vya watu  225 ilianza jana  Jumamosi Septemba 23.
Kazi hiyo inafanywa na kampuni ya Songoro Marine chini ya usimamizi wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ).
Akizungumza mbele ya Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa katika Kijiji cha Bwisya Kisiwa cha Ukara kilipozama kivuko hicho, mtaalamu kutoka kampuni hiyo, Meja Songoro alisema hatua ya kwanza itakuwa kuingiza hewa ndani ya kivuko ili kuyatawanya maji na kuanza kukivuta.
“Kivuko kinaendelea kuelea kwa sababu kuna hewa ndani yake. Wakati kinageuka (kupinduka) kilichota maji, tutaanza kuingiza hewa kutoa maji na kuanza kukivuta. Tutakapoanza kuyatawanya maji hayo, pia tutapeleka boya na hii itafanya chombo kizidi kuja juu. Baada ya hapo tutakisogeza taratibu hadi kwenye maji mafupi.”
 
Usisahau Kuinstall  Andoid Applicatuion yetu ili kupata habari zetu kwa haraka zaidi. Ingia Playstore, search Manyara leo blog