KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE YA BAJETI YATEMBELEA KIWANDA CHA DANGOTE


Mtaalam kutoka Kampuni Tanzu ya Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) ya GASCO inayojihusisha na usambazaji wa gesi, Mhandisi Mwanaidi Rashid (kulia) akielezea hatua iliyofikiwa ya ujenzi wa kituo Namba I cha gesi ambapo Kiwanda cha Saruji cha Dangote kitaunganishwa na huduma hiyo kwa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Bajeti kwenye ziara hiyo.
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Dkt. Mhandisi Juliana Pallangyo ( wa tatu kutoka kulia mbele) na Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Bajeti, Hawa Ghasia ( wa nne kutoka kulia mbele) wakiwa katika picha ya pamoja na kamati hiyo wakati wa ziara hiyo.
Mkurugenzi wa Kiwanda cha Uzalishaji wa Saruji cha Dangote, Hemendra Raithatha (kulia) akimpokea Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Dkt. Mhandisi Juliana Pallangyo (kushoto) aliyeambatana na Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Bajeti mara baada ya kuwasili katika kiwanda hicho.
Mkurugenzi wa Kiwanda cha Uzalishaji wa Saruji cha Dangote, Hemendra Raithatha (kulia) akielezea mafanikio na changamoto za kiwanda hicho kwa wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Bajeti (hawapo pichani). Wengine kutoka kushoto ni Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Bajeti, Hawa Ghasia na Makamu Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC), Jaji Mstaafu Josephat Mackanja.
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Dkt. Mhandisi Juliana Pallangyo, akifuatilia maelezo yaliyokuwa yanatolewa na Mkurugenzi wa Kiwanda cha Uzalishaji wa Saruji cha Dangote, Hemendra Raithatha (hayupo pichani ) katika kikao hicho.
Mkurugenzi wa Kiwanda cha Uzalishaji wa Saruji cha Dangote, Hemendra Raithatha (mbele) akielezea jambo kwa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Bajeti katika kikao kabla ya kuanza ziara ya kutembelea kiwanda hicho.
Sehemu ya wajumbe kutoka Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Bajeti na watendaji wa kiwanda cha Dangote wakifuatilia ufafanuzi uliokuwa unatolewa na Mkurugenzi wa Kiwanda cha Uzalishaji wa Saruji cha Dangote, Hemendra Raithatha (hayupo pichani) katika kikao hicho.
Kutoka kulia mbele mtaalam kutoka Idara ya Nishati, Mhandisi Edson Ngabo, Mchumi kutoka Idara ya Sera na Mipango, Josephat Mbwambo na Kaimu Mkurugenzi kutoka Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) wakifuatilia maelekezo ya Kamati ya Kudumu ya Bunge katika kikao hicho.
Mchumi kutoka Idara ya Sera na Mipango kutoka Wizara ya Nishati na Madini, Josephat Mbwambo (kulia) akinukuu hoja mbalimbali zilizokuwa zinawasilishwa na wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Bajeti katika kikao hicho.
Makamu Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC), Jaji Mstaafu Josephat Mackanja akifafanua jambo katika kikao hicho.

UKAID NA WIZARA YA FEDHA NA MIPANGO YAZINDUA PROGRAM YA MAFUNZO KWA WATUMISHI


Wafanyakazi watano wa Wizara ya Fedha na Mipango (Walioketi) waliopatiwa udhamini wa masomo nchini katika vyuo vikuu nchini Uingereza kwa kiwango cha Shahada ya Uzamili uliotolewa na Shirika la Maendeleo la Uingereza (UKAID-DFID), wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya watumishi wa British Council-Tanzania ambao ndio waratibu wa Program hiyo ya miaka mitano, itakayogharimu Shilingi bilioni 3.6 kwa  lengo la kuongeza ujuzi na umahili wa rasilimali watu katika masuala ya uchumi, mipango, usimamizi wa fedha za Umma na Sheria za kimataifa. Kutoka kushoto Harieth Lubinga, John Kabiti, Susan Mbayuwayu, Peter Kalugwisha na Gloria Mduda.
Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) (kulia) akiongea ofisini kwake na Mkurugenzi Mkazi wa Idara ya Kimataifa ya Maendeleo kutoka Serikali ya Uingereza (UKAID-DFID), Bi. Beth Arthy, kuhusu masuala mbalimbali ukiwemo ufadhili wa miaka mitano wa Taasisi hiyo wa masomo ya juu nchini Uingereza kwa wafanyakazi wa Wizara hiyo katika ngazi ya Shahada ya Uzamili.
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Mhe. Prof. Joyce Ndalichako (Mb) (kushoto) na Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) (kushoto), wakielekea katika hafla ya uzinduzi wa mpango wa ufadhili wa miaka mitano wa masomo ya juu kwa watumishi wa Wizara ya Fedha na Mipango, uliofadhiliwa na Serikali ya Uingereza wenye thamani za shilingi bilioni 3.6.
Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) (wa pili kulia), Mkuu wa Shirika la Msaada la Uingereza (UKAID) nchini Tanzania Beth Arthy (wa pili kushoto) na Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Mhe. Prof. Joyce Ndalichako (Mb) (kushoto) wakielekea katika uzinduzi wa program ya miaka mitano ya mafunzo ya mafunzo ya juu kwa ngazi ya Shahada ya Uzalimili kwenye vyuo vikuu nchini Uingereza kuhusu masuala ya uchumi, mipango, usimamizi wa fedha umma na sheria kwa baadhi ya watumishi wa Wizara ya Fedha na Mipango uliotolewa na Serikali ya Uingereza.
Mkurugenzi Mkazi wa British Council, Bi. Angela Hennelly, akizungumza jambo wakati wa uzinduzi wa mradi wa miaka mitano wa ufadhili wa masomo ya juu katika ngazi ya Shahada ya Uzamili kwa baadhi ya watumishi wa Wizara ya Fedha na Mipango kwenye vyuo vikuu mbalimbali nchini Uingereza kupitia Shirika la Maendeleo la UKAID-DFID utakaogharimu shilingi bilioni 3.6. British Council Tanzania ni waratibu wa mpango huo.
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Mhe. Prof. Joyce Ndalichako (Mb) akizungumza katika uzinduzi wa program ya miaka mitano ya mafunzo kwa ufadhili wa Serikali ya Uingereza kupitia Shirika lake la Maendeleo la  UKAID-DFID, uliofanyika katika Ofisi za Wizara ya Fedha na Mipango, Jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) akizungumza jambo wakati wa uzinduzi wa program ya ufadhili wa masomo ya Juu katika vyuo vikuu nchini Uingereza kwa wafanyakazi wa Wizara ya Fedha na Mipango katika ngazi ya shahada ya uzamili kupitia ufadhili wa Shirika la Maendeleo la Uingereza UKAID-DFID wenye thamani ya shilingi bilioni 3.6, Jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb), na viongozi waandamizi wa UKAID-DFID, British Council-Tanzania, Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Joyce Ndalichako, na watumishi wa Wizara ya Fedha na Mipango walionufaika na ufadhili huo (kushoto) wakifurahia baada ya kuzinduliwa rasmi kwa mpango wa miaka mitano wa ufadhili wa masomo kwa ngazi ya shahada ya uzamili katika vyuo vikuu vya nchini Uingereza katika Nyanja za uchumi, mipango, usimamizi wa fedha za umma na sheria za kimataifa uliotolewa na Serikali ya Uingereza kwa Wizara hiyo.
Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) (wa tatu kulia), Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Maendeleo la Kimataifa la Uingereza (UKAID-DFID), Bi. Beth Arthy (wa tatu kushoto), Mkurugenzi Mkazi wa British Council, Bi. Angela Hennelly na Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Mhe. Prof. Joyce Ndalichako (Mb) (wa pili kulia) wakiwa katika picha ya pamoja na Maafisa wa Serikali na Watumishi wa Wizara ya Fedha na Mipango waliopata ufadhili wa Mafunzo kutoka UKAID-DFID, muda mfupi baada ya kuzindua rasmi program hiyo, Jijini Dar es Salaam. (Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Wizara ya Fedha na Mipango)​

"Nimefunga mjadala wa Rambirambi" RC Gambo

Hatimaye utata uliokuwa umeenea wa kuwepo kwa ufujaji na matumizi mabaya ya  fedha kiasi cha milioni 285.49 zilizokuwa  zimechangwa  na  wadau  pamoja  na  serikali  kwa  ajili  ya  rambi  rambi  ya  vifo  vya ajali  ya  basi  la   wanafunzi  wa  shule  ya Lucky Vicent  umekwisha  baada  ya  mkuu  wa  mkoa  wa  Arusha  Mrisho  Gambo  kukabidhi milioni  23.27 kwa  wazazi  wa  watoto  walionusurika  katika  ajali  hiyo  
Akikabidhi fedha  hizo  mbele  ya  waandishi  wa  habari  ambapo  kila  mzazi amepata Milioni  7.75, Bw.  Gambo  amesema fedha  hizo  zilikuwa  zimebaki  baada  ya  matumizi  ya shughuli  za  mazishi kwa  watoto   32 walimu  wawili  na  dereva  waliokuwa  wamekufa  katika  ajali  hiyo  na  matumizi  mengine  yakiwemo  ya  wazazi  waliokuwa  nchini  marekani  kwa  ajili  ya  kuwauguza  watoto  wao  na  kwamba  matumizi  ya  fedha hizo  watapanga wao  wenyewe.
Katika hatua  nyingine  Bw  Gambo  alisema  Serikali imekubali kutoa wataam wa saikolojia kwa ajili ya kuendelea kuwasaidia watoto walionusurika katika ajali  ya basi la wanafunzi ili kuwaweka sawa na pia kuwaandaa kufanya mtihani wa darasa la saba unaowakabili mnamo mwezi Septemba.
Aidha  Bw, Gambo amesema kazi ya kutoa tiba  ya kisaikolojia pia ilishafanyika kwa wanafunzi wa shule ya Lucky Vicent .
Wakizungumza baada ya kukabidhiwa Fedha hizo wazazi  wa watoto hao wameishukuru serikali na wafadhili kutoka marekani kwa msaada  mkubwa kwa watoto wao tangu  mwanzo hadi sasa
Aidha wazazi hao wamesema pamoja  na watoto wao kuwa nje ya shule kwa zaidi ya miezi mitatu wako tayari kufanya mtihani na kumaliza ELIMU ya msingi unaotarajiwa kufanyika mwezi  September.
Kwa mujibu  wa  Bw  Gambo  baada ya kutokea kwa AJALI hiyo MWEZI May 2017 wadau MBALIMBALI na  serikali  walijitolea na kuchanga fedha  na  kupatikana  zaidi  ya milioni 285.49 ambazo  nbaada  ya matumizi  zilibaki  milioni  23.27 ambazo  zimekabidhiwa  leo.
Na  kuhusu  ombi  la wazazi  la  kutaka  watoto  wao   wafanye  mtihani   wa  kumaliza  elimu  ya  msingi  licha ya  kuwa  nje ya  shule kwa miezi  zaidi ya mitatu  Bw Gambo  alisema  kama wazazi  wako  tayari  na  wanaona  watoto  wao  wana  uwezo  wa  kufanya mtihani  hakuna kipingamizi.
"Suala hili linawezekana ikiwa wazazi na watoto wataonyesha utayari wa kufanya mtihani huo,na hata mapema leo waziri wa elimu Mhe. Ndalichako ameshalizungumzia" alisema Gambo.
Kuhusu maelezo  yalikuwa  yameenea  katika mitandao  ya  kijamii  kuwa  Bw  Gambo  ametakiwa  kukabidhi fedha  hizo  kwenye  mfuko  wa  kuendeleza  watoto  hao  ulioanzishwa  na  shirika  la  Stemm huku  wengine  wakidai  kuwa  zipelekwe  kuboresha  Hosipitali ya  Mkoa  wa  Arusha  ya Mount meru  Gambo  alisema  suala  la  kuanzisha  mfuko  na  kuboresha  hosipitali  lina  taratibu zake  na  sio  lazima  lisubiri fedha za  chenji  ya rambirambi   
"Kama kuna mfuko wa ELIMU ni jambo jema  na unaweza kuanzishwa na kuendelea ila  hizo zilizopo wanakabidhiwa wazazi bila masharti yeyote." alisisitiza Mhe Gambo.

Kuhusu madai  kuwa  serikali iliahidi kugharamia  mazishi   na  baadaye  yakagharamiwa  na fedha  za  wadau  Bw  Gambo  alisema  fedha zilizotolewa  na taasisi  za  serikali  ni  sawa  na serikali  imetoa  na kwamba hayo  ni  masuala  ya kisisasa  ambayo  asingependa  yaingizwe  kwenye  masuala  ya msingi yanayohusiana  na maisha  ya  watu.
"Fedha zilizotolewa na taasisi mbalimbali za serikali mfano NSSF huwezi sema sio za serikali, nadhani ifike mahali tuache siasa nyepesi" alisema Mhe Gambo.
Alliongeza  kuwa  serikali  imeshatenga Bilion 1.9 kwa ajili ya Hosipitali ya mkoa wa Arusha ya Mount Meru na kamwe serikali haiwezi kutumia michango hiyo kwa suala kama hilo na kuziita taarifa zilizosambaa mitandaoni kua ni za kizushi zenye nia ya kuichafua serikali.
image1.JPG
RC Gambo akiwakabidhi wazazi wa Doreen Mshana jumla ya Shilingi Milioni 7.75 ikiwa ni bakaa ya michango ya rambirambi.
image2.JPG
RC Gambo akiwakabidhi wazazi wa Wilson Tarimo jumla ya Shilingi Milioni 7.75 ikiwa ni bakaa ya michango ya rambirambi.
image3.JPG
RC Gambo akimkabidhi mzazi wa Shadhia jumla ya Shilingi Milioni 7.75 ikiwa ni bakaa ya michango ya rambirambi
image4.JPG
Kushoto ni mtoto Shadhia na Kulia ni mtoto Wilson wakitoka nje ya jengo la ofisi ya Mkuu wa mkoa.
image5.JPG
Mhe Gambo akisalimiana na mtoto Doreen Mshana
image6.JPG
Mhe Gambo katika picha ya pamoja na manusura wa ajali ya Lucky Vincent walipotembelea ofisi yake mapema hii leo.

CCM YAHITIMISHA MAFUNZO ELEKEZI YA SIKU MBILI KWA MAKATIBU WA CCM MIKOA YA TANZANIA BARA NA VISIWANI MJINI DODOMA.


Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi, Humphrey Polepole (wa pili kushoto) akiongoza nyimbo ya hamasa mara baada ya Katibu Mkuu wa CCM ndg:Abdulrahman Kinana kuwasili kufunga mafunzo elekezi ya siku mbili kwa Makatibu wa Mikoa CCM tanzania bara na Visiwani yaliofanyika katika Ukumbi wa sekretariet katika jengo la ofisi ya makao makuu ya CCM mjini Dodoma.
Katibu wa NEC Uchumi na fedha Dkt.Frank George Haule hawassi akiwasilisha mada wakati wa mafunzo elekezi kwa Makatibu wa Mikoa CCM
tanzania bara na Visiwani yaliofanyika katika Ukumbi wa sekretariet katika jengo la ofisi ya makao makuu ya CCM mjini Dodoma.

baadhi ya washiriki wakifuatilia kwa umakini Mafunzo elekezi kwa Makatibu wa Mikoa CCM tanzania bara na Visiwani yaliofanyika katika Ukumbi wa sekretariet katika jengo la ofisi ya makao makuu ya CCM mjini Dodoma.
maofisa wa chama wakifuatilia kwa umakini Mafunzo elekezi kwa Makatibu wa Mikoa CCM tanzania bara na Visiwani yaliofanyika katika Ukumbi wa sekretariet katika jengo la ofisi ya makao makuu ya CCM mjini Dodoma.
Mafunzo yakiendelea

washiriki Makatibu wa Mikoa CCM tanzania bara na Visiwani wakiwa katika mijadala kwa makundi mbalimbali kuchambua yale walio jifunza katika mafunzo elekezi yaliofanyika katika Ukumbi wa sekretariet katika jengo la ofisi ya makao makuu ya CCM mjini Dodoma.
Katibu wa NEC Oganaizesheni ndg: pelela Ame Silima,akizungumza wakati wa kufunga mafunzo elekezi ya siku mbili kwa Makatibu wa Mikoa CCM tanzania bara na Visiwani yaliofanyika katika Ukumbi wa sekretariet katika jengo la ofisi ya makao makuu ya CCM mjini Dodoma.
Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi ndg:Humphrey Polepole akizungumza wakati wa kufunga mafunzo elekezi ya siku mbili kwa Makatibu wa Mikoa CCM tanzania bara na Visiwani yaliofanyika katika Ukumbi wa sekretariet katika jengo la ofisi ya makao makuu ya CCM mjini Dodoma.
Katibu wa NEC, Siasa na Uhusiano wa Kimataifa, Ngemela  ubinga,akizungumza wakati wa kufunga mafunzo elekezi ya siku mbili kwa
Makatibu wa Mikoa CCM tanzania bara na Visiwani yaliofanyika katika Ukumbi wa sekretariet katika jengo la ofisi ya makao makuu ya CCM mjini Dodoma.
Naibu Katibu Mkuu wa CCM-Bara Rodrick Mpogolo akizungumza wakati wa kufunga mafunzo elekezi ya siku mbili kwa Makatibu wa Mikoa CCM tanzania bara na Visiwani yaliofanyika katika Ukumbi wa sekretariet katika jengo la ofisi ya makao makuu ya CCM mjini Dodoma.
Naibu Katibu Mkuu wa CCM- Zanzibar Dkt. Abdallah Juma Mabodi, akizungumza wakati wa kufunga mafunzo elekezi ya siku mbili kwa
Makatibu wa Mikoa CCM tanzania bara na Visiwani yaliofanyika katika Ukumbi wa sekretariet katika jengo la ofisi ya makaomakuu ya CCM mjini Dodoma.
Katibu Mkuu wa CCM ndg:Abdulrahman Kinana akifunga mafunzo elekezi ya siku mbili kwa Makatibu wa Mikoa CCM tanzania bara na Visiwani (kulia) ni Naibu Katibu Mkuu wa CCM-Bara Rodrick Mpogolo(kushoto) Naibu Katibu Mkuu wa CCM- Zanzibar Dkt. Abdallah Juma Mabodi .

Katibu Mkuu wa CCM ndg:Abdulrahman Kinana akifunga mafunzo elekezi ya siku mbili kwa Makatibu wa Mikoa CCM tanzania bara na Visiwani yaliofanyika katika Ukumbi wa sekretariet katika jengo la ofisi ya makao makuu ya CCM mjini Dodoma.(PICHA ZOTE NA FAHADI SIRAJI)

WAZIRI MKUU AHITIMISHA ZIARA YAKE LEO KATIKA MKOA WA TABORA

PMO_8135
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akiongea na Viongozi pamoja na watumishi wa Mkoa wa Tabora leo August.13.2017 wakati wa majumuisho ya ziara yake Mkoa wa Tabora. Ambo ume fanyika katika Ukumbi wa Mikutano Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Tabora
PMO_8269
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akiagana katika Uwanja wa Ndege wa Tabora leo August.13.2017 . na Mwenyeji wake Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Agrey Mwandri baada ya kumaliza ziara ya siku Nne katika Mkoa wa Tabora ,katikati ni Mkuu wa Wilaya ya Tabora Queen Mwashinga
PMO_8275
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa .akiwapungia Mkono wa kwaheri Viongozi pamoja na wananchi wa Mkoa wa Tabora ambao walifika kumuaga katika Uwanja wa Ndege wa Tabora baada ya kumaliza ziara ya siku Nne ya kikazi katika Mkoa wa Tabora leo August 13,2017. Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu

WAZIRI MKUU AKIWA WILAYA YA UYUI MKOA WA TABORA KWA ZIARA YA KIKAZI

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akiwasalimia wananchi katika Uwanja wa Nsololo jimbo la Igalula Wilaya ya Uyui mara baada yakuwasili leo August 12.2017 na kufanya mkutano wa hadhara katika Wilaya ya Uyui Mkoa wa Tabora
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa na Mkewe Mama Majaliwa wakiwasalimia wananchi katika Uwanja wa Nsololo jimbo la Igalula Wilaya ya Uyui mara baada yakuwasili leo August 12.2017 na Waziri Mkuu kufanya mkutano wa hadhara katika Wilaya ya Uyui Mkoa wa Tabora
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akisalimiana na Mjumbe wa Halimashauri Kuu ya CCM Taifa na Mkuu wa Wilaya Mstaafu Bwana Jackson Masome .walipo kutana katika mkutano wa hadhara leo August 12.2017 katika Wiaya ya Uyui Tabora. Waziri yupo Mkoa wa Tabora kwa ziara ya Kikazi

                                                                   PICHA NA OFISI YA WAZIRI MKUU

MAGARI 40 YANASHIKILIWA NA JESHI LA POLISI MKOANI TABORA KUFUATIA MSAKO ULIOFANYWA NA MAMLAKA YA USIMAMIZI WA BIMA NCHINI (TIRA) KANDA YA KATI, WA KUBAINI VYOMBO VYA MOTO VYENYE BIMA FEKI.


Meneja wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bima nchini  Kanda ya Kati Bi.Stella Rutaguza akizungumza na madereva pamoja na makondakta katika stendi kuu ya mabasi mkoani Tabora ,walipokwenda kugagua bima za vyombo vya moto kama ni halali ama feki.
 
 Afisa Mwandamizi wa Bima Maneno Adam kutoka Mamlaka ya Usimamizi wa Bima( TIRA)akikagua gari ili kuangalia kama bima inayotumika kama ni halali ama ni feki
  Ukaguzi wa magari ukiendelea katika stendi kuu ya mabasi Mkoani Tabora kama inavyoonekana kwenye picha kutoka kushoto ni Meneja wa Kanda ya kati kutoka Mamlaka ya Usimamizi wa Bima nchini bi.Stella Rutaguza akiwa na askari wa kikosi cha usalama barabarani Koplo Clement 
Zoezi la ukaguzi likiendelea wakati huohuo madereva ,makondakta pamoja na abiria wakipata elimu namna ya kutambua Bima kama ni halali ama feki.

 
Wananchi ,madereva ,makondakta wa mabasi makubwa na madogo wakipewa elimu na namna ya kut5ambua bima feki kwa kutumia  simu ya mkononi au kwa njia ya mtandao mfumo wa TIRA MIS .Picha na Vero Ignatus Blog.
 

Na   Mahmoud Ahmad, Tabora

Mamlaka ya usimamizi wa Bima nchini (TIRA) imefanya zoezi la ukaguzi wa bima za vyombo vya moto katika manispaaa ya Tabora katika stendi kuu ya mabasi na kubaini magari mengi hayana bima na mengine yana bima tofauti na kile kilichoorodheshwa katika bima hizo.

Akizungumza juu ya zoezi hilo meneja ( TIRA) Kanda ya Kati Stella Rutaguza amesema kuwa katika wameweza kukagua magari zaidi ya 266 magari 27 yamebainika kuwa na bima za kughushi ,magari 13 hayakuwa na bima,magari mengine yanatumia bima za pikipiki,na baadhi ya magari madogo yanatumia bima za magari ya mizigo.

"Magari tuliyoyakagua na kuyakuta yana bima feki tumeyakamata na kuyapeleka kituoni ili kwamba watupe maelezo  kuwa hizo bima wamezipata wapi,"alisema

Amesema kwa ada za malipo ya bima kwa mujibu wa sheria kwa maana ya bima ndogo (Third party insurance) kwa jumla magari haya 40 ni shilingi Milioni  33,850,000/= ambapo magari hayo yaliyokamatwa ni mabasi ya abiria 65,Coster za abiria 26, Noa na magari madogo ya binafsi.

 Imebainika kuwa kuna wamiliki wa magari ambao walikuwa wamenunua bima kubwa (Comprehensive Insurance) ambapo kwa mabasi walikuwa wamelipia kuanzia shs.3,000,000/= na zaidi ambazo zimeingia kwenye mifuko ya matapeli wa bima.

"Tunataka hawa vishoka wa bima feki watafute kazi nyingine  halali za kufanya  kwani Mamlaka ya usimamizi wa Bima nchini haitawafumbia macho wadanyanyifu hawa

Bi Stella amesema kuwa kesi za matapeli wa bima zimekuwa zikikaa muda mrefu bila kupekekwa mahakamani na hata zikipelekwa zimekuwa zikichukua  pia muda mrefu pia.

'Tunaomba kesi za Bima ziwe zinashughulikiwa kwa haraka na mamlaka husika "alisisitiza bi Stella. 

Meneja huyo wa kanda ya kati Stella ametoa rai kwa mawakala wa bima na kusema kuwa yeyote atakayegunduliwa anauza bima feki atakamatwa na kupelekwa kwenye vyombo vya sheria na  atafutiwa leseni  maana amekiuka taratibu za kisheria .

" Hawa watu wengi wanaouza hizo feki bima siyo wakala wa bima ila ni matepeli tu wamtaani hivyo tukiwabaini tutawapeleka kwenye vyombo vya sheria hatuna utani wala mchezo katika hili".alisema.

 ********************************************************
Namna ya KUHAKIKI BIMA Kama ni  HALALI ama feki
 
Kwa njia ya simu ya mkononi  nenda kwenye uwanja wa ujumbe mfupi  andika neno STIKA weka namba ya stika tuma kwenda namba 15200
Kwa kupitia njia ya mtandaoni (internet)kwenda kwenye tovuti ya Tira mis  
htt/mis.tira.go.tz kisha ingiza namba za stika na bofya hakiki.