BILA SHERIA HAKUNA KOSA,

 
PHOTO: Jaji wa mahakama ya kimataifa
ya makosa ya jinai ICC Bertram Schmitt

Warsha ya mafunzo ya kimataifa juu ya sheria na makosa inawakutanisha wadau mbalimbali kutoka nchi kadhaa duniani ikiwa ni katika kupambana na uhalifu wa kwenye nyanja za kimataifa na wakimataifa katika mradi wa Afrika mashariki ukiwa chini ya usimamizi wa wizara ya mambo ya nje ya Ujerumani.


PHOTO: Jaji wa mahakama ya kimataifa ya makosa ya jinai ICC
Bertram Schmitt, aliyesimama akiwasilisha mada kuhusu uwezeshaji
Katika mahakama pamoja na mapungufu kwa upande wa fedha (bajeti)

 PHOTO JUU NA CHINI: Wahudhuliaji kutoka taasisi mbalimbali za kimahakama kama wanasheria, majaji na mawakili wakifuatilia mada.

  Mahmoud AhmadARUSHA                                                                         
Katika warsha hiyo ya wataalam maarufu na wataalam wa kuongoza mradi  wa Wayamo iliyojumuisha nchi nyingi za Afrika wakiwemo mawakili, majaji kutoka nchi za Afrika mashariki ikiwemo Tanzania imeanza leo jijini Arusha.

Jaji wa mahakama kuu nchini Jaji Othuman Chande amesema mkutano huo wenye lengo la kuzungumzia uhuru wa mahakama, utawala wa kisheria, utendaji wa mahakama za kimataifa na uhusiano wake na makosa ya jinai ambayo yanayofanyika nje ya mipaka ya nchi ambako makosa yanafanyika kimataifa.

Ameongeza kuwa “usafirishaji binadamu, kuua  wanyamapori, ni moja kati ya makosa yanayofanyika kimataifa na vita yake siyo ifanyike hapa Tanzania lakini pia hata nje ya mipaka” hivyo ametoa wito kwa vyombo vya dola kutoa ushirikiano katika nchi zinazo athirika na janga hilo.


Aitha warsha hiyo imewakutanisha majaji maarufu kutoka mahakama ya kuu ya makosa ya Jinai The Hague mstaafu Navil Pillay, Jaji wa mahakama ya juu ya nchini Marekani Jaji Sonia Sotomayor na Rais wa zamani wa mahakama ya Rwanda Jaji Muyoboke Karimuda na majaji wa Afrika Mashariki hata wanasheria wakujitegemea akiwemo Nelson Ndeki kutoka Tanzania.





Hakuna maoni:

Chapisha Maoni