Na Mahmoud Ahmad-Arusha
Mahakama za Tanzania bado
zinakabiliwa na changamoto ya kuzikabili kesi za kimataifa ikiwemo kesi
za uhalifu wa kimtandao,biashara ya binadamu kwani imeonekana zimekuwa
zikiisha bila ya kuwatia hatiani wakosaji wa makosa hayo na kuangalia
kama vyombo husika na mashtaka vinauwezo kiasi gani katika kuzikabili
kesi hizo.
Kauli hiyo imetolewa kwenye
Kongamano lililowakutanisha majaji kutoka sehemu mbali mbali za bara
hili na nje na kaimu jaji mkuu wa Tanzania Ibrahim Juma wakati
alipotakiwa kuelezea suala la makosa mbali mbali ya kimataifa na
kuandaliwa na Taasisi ya Wayamo na kufanyika jijini hapa.
Jaji Juma alisema kuwa wamekutana
kuangalia ni namna gani wanaweza kuyakabili makosa ya namna hiyo na
kupeana njia ya kuweza kuyashughulikia kikamilifu na kutoa haki yenye
tija kwa makosa hayo pindi yanapofika mahakamani ambapo miongoni mwa
makosa hayo yanayofika kwenye mahakama ni ujangili wa kimataifa,wizi wa
njia ya mtandao,na kesi za chaguzi.
“Tumefika mahali sasa kuangalia
makosa hayo na njia ya kuyatatua ilikuweza kuipeleka mahakama kuweza
kuyashughulikia makosa kwa weledi na kutoa haki inayostahili kwa makosa
hayo”alisema kaimu jaji mkuu.
Nae Jaji mkuu wa Zanzibar Othman
Makungu alisema kuwa Ongezeko la makosa ya Chaguzi limeonekana kukuwa
kwa kasi kwenye mataifa yetu kila pembe hivyo kongamano hilo litakuja na
jibu la kuweza kuyatatua kwa ukaribu na kuweza kuyashughulikia kwa
uweledi.
Ametolea mfano wa makosa ya
ujangili ambapo mshtakiwa analetwa mahakamani halafu anaachiwa huru au
kesi inachelewa kuamlizika kwa wakati hapa je ni
umaskini,kutokujali,rushwa, au uzoefu mdogo ndio maana tunakutana
kuyajadili ilituweze kuyapatia majibu masuala hayo.
Jaji Makungu amesema kuwa njia
pekee ya kuweza kufikia malengo ya makosa hayo ya kimataifa ikiwemo
biashara ya binadamu,Makosa ya uhalifu wa mtandao,inasababisha watu
kuweza kuendelea kuteseka hapa njia ni kuanza kuyazuia yasitokee.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni