"Nimefunga mjadala wa Rambirambi" RC Gambo

Hatimaye utata uliokuwa umeenea wa kuwepo kwa ufujaji na matumizi mabaya ya  fedha kiasi cha milioni 285.49 zilizokuwa  zimechangwa  na  wadau  pamoja  na  serikali  kwa  ajili  ya  rambi  rambi  ya  vifo  vya ajali  ya  basi  la   wanafunzi  wa  shule  ya Lucky Vicent  umekwisha  baada  ya  mkuu  wa  mkoa  wa  Arusha  Mrisho  Gambo  kukabidhi milioni  23.27 kwa  wazazi  wa  watoto  walionusurika  katika  ajali  hiyo  
Akikabidhi fedha  hizo  mbele  ya  waandishi  wa  habari  ambapo  kila  mzazi amepata Milioni  7.75, Bw.  Gambo  amesema fedha  hizo  zilikuwa  zimebaki  baada  ya  matumizi  ya shughuli  za  mazishi kwa  watoto   32 walimu  wawili  na  dereva  waliokuwa  wamekufa  katika  ajali  hiyo  na  matumizi  mengine  yakiwemo  ya  wazazi  waliokuwa  nchini  marekani  kwa  ajili  ya  kuwauguza  watoto  wao  na  kwamba  matumizi  ya  fedha hizo  watapanga wao  wenyewe.
Katika hatua  nyingine  Bw  Gambo  alisema  Serikali imekubali kutoa wataam wa saikolojia kwa ajili ya kuendelea kuwasaidia watoto walionusurika katika ajali  ya basi la wanafunzi ili kuwaweka sawa na pia kuwaandaa kufanya mtihani wa darasa la saba unaowakabili mnamo mwezi Septemba.
Aidha  Bw, Gambo amesema kazi ya kutoa tiba  ya kisaikolojia pia ilishafanyika kwa wanafunzi wa shule ya Lucky Vicent .
Wakizungumza baada ya kukabidhiwa Fedha hizo wazazi  wa watoto hao wameishukuru serikali na wafadhili kutoka marekani kwa msaada  mkubwa kwa watoto wao tangu  mwanzo hadi sasa
Aidha wazazi hao wamesema pamoja  na watoto wao kuwa nje ya shule kwa zaidi ya miezi mitatu wako tayari kufanya mtihani na kumaliza ELIMU ya msingi unaotarajiwa kufanyika mwezi  September.
Kwa mujibu  wa  Bw  Gambo  baada ya kutokea kwa AJALI hiyo MWEZI May 2017 wadau MBALIMBALI na  serikali  walijitolea na kuchanga fedha  na  kupatikana  zaidi  ya milioni 285.49 ambazo  nbaada  ya matumizi  zilibaki  milioni  23.27 ambazo  zimekabidhiwa  leo.
Na  kuhusu  ombi  la wazazi  la  kutaka  watoto  wao   wafanye  mtihani   wa  kumaliza  elimu  ya  msingi  licha ya  kuwa  nje ya  shule kwa miezi  zaidi ya mitatu  Bw Gambo  alisema  kama wazazi  wako  tayari  na  wanaona  watoto  wao  wana  uwezo  wa  kufanya mtihani  hakuna kipingamizi.
"Suala hili linawezekana ikiwa wazazi na watoto wataonyesha utayari wa kufanya mtihani huo,na hata mapema leo waziri wa elimu Mhe. Ndalichako ameshalizungumzia" alisema Gambo.
Kuhusu maelezo  yalikuwa  yameenea  katika mitandao  ya  kijamii  kuwa  Bw  Gambo  ametakiwa  kukabidhi fedha  hizo  kwenye  mfuko  wa  kuendeleza  watoto  hao  ulioanzishwa  na  shirika  la  Stemm huku  wengine  wakidai  kuwa  zipelekwe  kuboresha  Hosipitali ya  Mkoa  wa  Arusha  ya Mount meru  Gambo  alisema  suala  la  kuanzisha  mfuko  na  kuboresha  hosipitali  lina  taratibu zake  na  sio  lazima  lisubiri fedha za  chenji  ya rambirambi   
"Kama kuna mfuko wa ELIMU ni jambo jema  na unaweza kuanzishwa na kuendelea ila  hizo zilizopo wanakabidhiwa wazazi bila masharti yeyote." alisisitiza Mhe Gambo.

Kuhusu madai  kuwa  serikali iliahidi kugharamia  mazishi   na  baadaye  yakagharamiwa  na fedha  za  wadau  Bw  Gambo  alisema  fedha zilizotolewa  na taasisi  za  serikali  ni  sawa  na serikali  imetoa  na kwamba hayo  ni  masuala  ya kisisasa  ambayo  asingependa  yaingizwe  kwenye  masuala  ya msingi yanayohusiana  na maisha  ya  watu.
"Fedha zilizotolewa na taasisi mbalimbali za serikali mfano NSSF huwezi sema sio za serikali, nadhani ifike mahali tuache siasa nyepesi" alisema Mhe Gambo.
Alliongeza  kuwa  serikali  imeshatenga Bilion 1.9 kwa ajili ya Hosipitali ya mkoa wa Arusha ya Mount Meru na kamwe serikali haiwezi kutumia michango hiyo kwa suala kama hilo na kuziita taarifa zilizosambaa mitandaoni kua ni za kizushi zenye nia ya kuichafua serikali.
image1.JPG
RC Gambo akiwakabidhi wazazi wa Doreen Mshana jumla ya Shilingi Milioni 7.75 ikiwa ni bakaa ya michango ya rambirambi.
image2.JPG
RC Gambo akiwakabidhi wazazi wa Wilson Tarimo jumla ya Shilingi Milioni 7.75 ikiwa ni bakaa ya michango ya rambirambi.
image3.JPG
RC Gambo akimkabidhi mzazi wa Shadhia jumla ya Shilingi Milioni 7.75 ikiwa ni bakaa ya michango ya rambirambi
image4.JPG
Kushoto ni mtoto Shadhia na Kulia ni mtoto Wilson wakitoka nje ya jengo la ofisi ya Mkuu wa mkoa.
image5.JPG
Mhe Gambo akisalimiana na mtoto Doreen Mshana
image6.JPG
Mhe Gambo katika picha ya pamoja na manusura wa ajali ya Lucky Vincent walipotembelea ofisi yake mapema hii leo.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni