MAGARI 40 YANASHIKILIWA NA JESHI LA POLISI MKOANI TABORA KUFUATIA MSAKO ULIOFANYWA NA MAMLAKA YA USIMAMIZI WA BIMA NCHINI (TIRA) KANDA YA KATI, WA KUBAINI VYOMBO VYA MOTO VYENYE BIMA FEKI.


Meneja wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bima nchini  Kanda ya Kati Bi.Stella Rutaguza akizungumza na madereva pamoja na makondakta katika stendi kuu ya mabasi mkoani Tabora ,walipokwenda kugagua bima za vyombo vya moto kama ni halali ama feki.
 
 Afisa Mwandamizi wa Bima Maneno Adam kutoka Mamlaka ya Usimamizi wa Bima( TIRA)akikagua gari ili kuangalia kama bima inayotumika kama ni halali ama ni feki
  Ukaguzi wa magari ukiendelea katika stendi kuu ya mabasi Mkoani Tabora kama inavyoonekana kwenye picha kutoka kushoto ni Meneja wa Kanda ya kati kutoka Mamlaka ya Usimamizi wa Bima nchini bi.Stella Rutaguza akiwa na askari wa kikosi cha usalama barabarani Koplo Clement 
Zoezi la ukaguzi likiendelea wakati huohuo madereva ,makondakta pamoja na abiria wakipata elimu namna ya kutambua Bima kama ni halali ama feki.

 
Wananchi ,madereva ,makondakta wa mabasi makubwa na madogo wakipewa elimu na namna ya kut5ambua bima feki kwa kutumia  simu ya mkononi au kwa njia ya mtandao mfumo wa TIRA MIS .Picha na Vero Ignatus Blog.
 

Na   Mahmoud Ahmad, Tabora

Mamlaka ya usimamizi wa Bima nchini (TIRA) imefanya zoezi la ukaguzi wa bima za vyombo vya moto katika manispaaa ya Tabora katika stendi kuu ya mabasi na kubaini magari mengi hayana bima na mengine yana bima tofauti na kile kilichoorodheshwa katika bima hizo.

Akizungumza juu ya zoezi hilo meneja ( TIRA) Kanda ya Kati Stella Rutaguza amesema kuwa katika wameweza kukagua magari zaidi ya 266 magari 27 yamebainika kuwa na bima za kughushi ,magari 13 hayakuwa na bima,magari mengine yanatumia bima za pikipiki,na baadhi ya magari madogo yanatumia bima za magari ya mizigo.

"Magari tuliyoyakagua na kuyakuta yana bima feki tumeyakamata na kuyapeleka kituoni ili kwamba watupe maelezo  kuwa hizo bima wamezipata wapi,"alisema

Amesema kwa ada za malipo ya bima kwa mujibu wa sheria kwa maana ya bima ndogo (Third party insurance) kwa jumla magari haya 40 ni shilingi Milioni  33,850,000/= ambapo magari hayo yaliyokamatwa ni mabasi ya abiria 65,Coster za abiria 26, Noa na magari madogo ya binafsi.

 Imebainika kuwa kuna wamiliki wa magari ambao walikuwa wamenunua bima kubwa (Comprehensive Insurance) ambapo kwa mabasi walikuwa wamelipia kuanzia shs.3,000,000/= na zaidi ambazo zimeingia kwenye mifuko ya matapeli wa bima.

"Tunataka hawa vishoka wa bima feki watafute kazi nyingine  halali za kufanya  kwani Mamlaka ya usimamizi wa Bima nchini haitawafumbia macho wadanyanyifu hawa

Bi Stella amesema kuwa kesi za matapeli wa bima zimekuwa zikikaa muda mrefu bila kupekekwa mahakamani na hata zikipelekwa zimekuwa zikichukua  pia muda mrefu pia.

'Tunaomba kesi za Bima ziwe zinashughulikiwa kwa haraka na mamlaka husika "alisisitiza bi Stella. 

Meneja huyo wa kanda ya kati Stella ametoa rai kwa mawakala wa bima na kusema kuwa yeyote atakayegunduliwa anauza bima feki atakamatwa na kupelekwa kwenye vyombo vya sheria na  atafutiwa leseni  maana amekiuka taratibu za kisheria .

" Hawa watu wengi wanaouza hizo feki bima siyo wakala wa bima ila ni matepeli tu wamtaani hivyo tukiwabaini tutawapeleka kwenye vyombo vya sheria hatuna utani wala mchezo katika hili".alisema.

 ********************************************************
Namna ya KUHAKIKI BIMA Kama ni  HALALI ama feki
 
Kwa njia ya simu ya mkononi  nenda kwenye uwanja wa ujumbe mfupi  andika neno STIKA weka namba ya stika tuma kwenda namba 15200
Kwa kupitia njia ya mtandaoni (internet)kwenda kwenye tovuti ya Tira mis  
htt/mis.tira.go.tz kisha ingiza namba za stika na bofya hakiki.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni