TENGERU CDTI YAONGEZA UDAHILI



Na Ahemd Mahmoud

Katika juhudi za serikali za kuimarisha mazingira ya  ujifunzaji wanafunzi wa kike hapa nchini,Taasisi ya maendeleo ya jamii Tengeru iliyopo Jijini Arusha kwa  mwaka wa fedha 2022/2023 imeipatia shilingi Bilion 2.3 kwa ajili ya ujenzi wa bweni la kike ambalo litasaidia kuondoa changamoto wanazokabiliana nazo ikiwemo vitendo vya ubakaji .

Akizungumza na vyombo vya habari Jijini Dodoma wakati akiwasilisha utekelezaji na mwelekeo kwa mwaka wa fedha 2022/2023  Mkuu wa Taasisi ya maendeleo ya jamii Tengeru  Dkt. Bakari  George amesema kuwa Bweni hilo lenye uwezo wa kubeba wanafunzi 568 litakuwa mkombozi kwao na taasisi hiyo 

Amesema kuwepo kwa bweni hilo itasaidia pia  kuwafatilia kwa ukaribu ukizingatia kujua mienendo yao kwani wanapokuwa mtaani wanakumbana na changamoto nyingi ambazo upelekea wengi kushindwa kutimiza ndoto zao na ukizingatia kwa sasa vyuo vingi  kwa sasa vinachukua vijana chini ya miaka 17 ambao wamemaliza kidato cha nne ambao wanapaswa kupewa uangalizi.

Pia amesema kuwa taasisi hiyo imeanzisha utaratibu wa  kuwachangia fedha wanafunzi wanaoishi mazingira magumu huku akiwataka watanzania watakaowiwa kutoa michango yao ili wanafunzi hao waweze kutimiza malengo yao .

"Kama mnavyojua mtoto wa kike ukimjengea mazingira rafiki ya uzomaji atatimiza ndoto zake kwa hiyo sisi kama taasisi tumejipanga kuboresha miundo mbinu hivyo niwaombe watanzania wenye mapenzi mema na watoto waishio mazingira magumu watume michango yao ili tuweze kuwasaidia"amesema Dkt. Bakari. 

Vile vile amesema Kwa mwaka 2022/2023, kituo kinatarajia kushirikiana na wadau kutekeleza utolewaji wa huduma ya msaada wa kisheria kwa kuzingatia falsafa ya maendeleo ya jamii. 

Aidha ameongeza kuwa  kituo kinaandaa programu ya mafunzo kwa maafisa bajeti wa mamlaka za serikali za mitaa kuwajengea uwezo katika maandalizi ya bajeti zinazozingatia usawa wa kijinsia.

Kwa upande wake Msemaji mkuu wa Serikali Gerlison Msigwa amesema kuwa serikali kwa kutambua umuhimu wa elimu  tayari imeajiri maafsa maendeleo ya jamii 3000 huku mahitaji yakiwa ni zaidi ya elfu tano ili jamii iweze kufikiwa na wataalamu. 

WATUMISHI WALIOKUTWA NA VYETI FEKI KULIPWA BILION 20

 



Na Ahmed Mahmoud

MFUKO wa Hifadhi ya Jamii wa PSSSF umesema unatarajia kuanza kuwalipa Watumishi waliokutwa na Vyeti Feki Jumla ya Shilingi Bilioni 20 ndani ya siku 60 takribani watumishi 9000 mara baada tu yakupokea madai yao kutoka kwa waliyokuwa Waajiri wao.

Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko huo,ACP Hosea Kashimba ameyaeleza hayo Leo Jijini Dodoma  wakati akitoa taarifa kwa Waandishi wa Habari kuhusu utekelezaji wa Majukumu ya Mfuko wa PSSSF na mwelekeo kwa Mwaka wa Fedha 2022/2023.

ACP Kashimba  amebainisha kuwa hadi kufikia Mwezi Juni Mwaka2022Mfuko huo  ulikuwa na Uwekezaji wenye thamani ya Shilingi Trlioni 7.5kwaajili ya kufanya uendelevu wa Mfuko huo.

"Mafao yaliyotolewa na mifuko ya pensheni ambapo kuanzia Julai 1,mwaka huu wanachama wote wa mifuko ya pensheni wanalipwa mafao ya uzee kwa kutumia kanuni zinazofanana ambazo zinalipa mafao  bora na kuwezesha mifuko,”amesema CPA Hosea.

Pamoja na hayo CPA Kashimba ameeleza kuwa Mfuko huo unatambua Moja ya changamoto kubwa kwenye jamii ni uelewa mdogo kuhusu sekta ya hifadhi ya jamii hivyo PSSSF imejipanga kuendelea kutoa elimu kwa wanachama wake ili kuhakikisha sekta hiyo inafanikiwa .

Amesema kuwa ili jitihada za kuhakikisha lengo la kutoa huduma bora linatimia,Mfuko unaendelea kutekeleza mambo mbalimbali yanayolenga kurahisisha utoaji wa huduma ikiwa ni pamoja na mtandao wa Ofisi za Mfuko ambapo una Ofisi Kila Mkoa na baadhi ya Wilaya Kwa lengo la kuwa karibu na wanachama.

“Mfuko una kituo cha kupiga simu bure kwa ajiri ya wanachama ambapo huduma hutolewa hadi saa mbili usiku ikiwemo mfumo wa ufuatiliaji wa masuala ya yanayohusu huduma mbalimbali za uanachama,”amesema CPA Kashimba.

Akieleza matarajio ya baadae,amesema wanatarajia kuongeza vituo vya uhakiki Katika halmashauri mbalimbali na kuanzisha utaratibu wa kujihakiki kupitia simu janja na kusaidia Kila taarifa ya mwanachama iwe kwenye mfumo.

“Matarajio mengine ni kuhakikisha mifumo ya PSSSF inasomana na mifumo mingine kutoka Taasisi za Umma zinazotoa huduma,kurahisisha uandikishaji wanachama na uletaji wa madai kupitia mtandao na kutumia mifumo mipya ya Tehama kulingana na mahitaji ya Mfuko,”amesema

CPA Hosea ametaja matarajio mengine kuwa ni kubuni mifumo mipya na salama ya TEHAMA kulingana na mahitaji ya mfuko pamoja na kutumia mifumo ya TEHAMA kwa asilimia 85 huku lengo likiwa ni kutumia kwa asilimia 100 ifikapo 2023 katika shughuli za Mfuko hivyo kuboresha utoaji huduma.

Ikumbukwe kuwa mfuko wa PSSSF ulianzishwa mwaka 2018 kupitia sheria ya mfuko wa hifadhi ya jamii kwa watumishi wa Umma Namba 2 ya mwaka 2018 ambapo mfuko huo ni matokeo ya kuunganishwa kwa iliyokuwa mifuko ya hifadhi ya jamii ya GEPF (1942),LAPF (1944),PPF (1978) na PSPF(1999).

ERB YAWEKA MIPANGO YA KUZALISHA NA KUKUZA WELEDI KWA WAHANDISI NCHINI

 


Na Ahmed Mahmoud

KATIKA kuimarisha ufanisi wa utendaji kazi wa wahandisi nchini,Bodi ya wahandisi (ERB) imesema imeweka mipango ya kukuza na kuimarisha weledi wa sekta  ikiwemo kupambana na vitendo vya rushwa.


Akizungumza na waandishi wa habari  leo Novemba 10  jijini Dodoma wakati akielezea utekelezaji wa majukumu ya bodi hiyo na vipaumbele vyake kwa mwaka wa fedha 2022/2023 Msajili wa Bodi ya wahandisi Bernad Kavishe amesema Bodi itaweka maslahi ya Umma mbele ikiwemo na kuzingatia maadili.

"Wahandisi pia lazima wadhibitiwe wawe na nidhamu na maadili mema wawe na uadilifu na kwa kifupi wahandisi tunaweka maslahi ya Umma mbele na maslah yetu binafsi nyuma na ndio maana tunachukua kiapo kuapa kuweka maslahi ya Umma mbele,

" Bodi  ipo mstari wa mbele katika kupambana na rushwa manake  rushwa ni adui wa uhai siyo tu adui wa haki lakini malengo mahususi ya bodi ni kuimarisha na  kuhakikisha udhibiti wa kazi za wahandisi na taaluma ya wahandisi kwasababu uhandisi hauishii shuleni uhandisi ni tunahakikisha mpaka mtu  ana staafu" amesema Mhandisi Kavishe 

Aidha Mhandisi Kavishe ametoa wito kwa watu wenye miradi kuacha kutumia wahandisi  ambao hawajasajiliwa na bodi hiyo ili kuondokana na malalamiko pale wanapoharibiwa kazi zao.

"Kinyume cha sheria kabisa kupata huduma za kihandisi nje na watu  ambao hawajadhibitishwa na bodi  mbalimbali za kitaaluma, ile leseni tunayokabidhi ile ndio kielelezo ambacho serikali  imeipitisha kwamba huyu mtu kapata elimu sahihi hawana mashaka nae na ujuzi wake upo hai"amesema Mhandisi Kavishe.

Nae Msemaji Mkuu wa Serikali Gerson Msigwa amesema Serikali imewekeza fedha nyingi kwenye ujenzi wa miradi mbalimbali ikiwemo barabara majengo na tayari imezalisha wahandisi zaidi ya elfu 33 na endapo miradi ikiharibiwa ERB inahusika.

"Kuna kazi kubwa inafanyika na miradi mingi ndani ya nchi yetu ambayo inategemea ushauri wa wahandisi hawa  na nichukue nafasi hii kuwapongeza mpaka sasa nchi yetu imezalisha wahandisi  zaidi ya elfu 33 na 26 wapo sokoni wanafanya kazi, ikumbukwe kuwa   tulipokuwa tunapata uhuru mwaka 1961 tulikua na wahandisi wawili tuu leo tunazungumzia hawa walio kazini na vijana bado wapo vyuoni wanasoma wanaendelea kuzalishwa" amesema Msigwa

TCRA YATOA LESENI 3132 KUTOKA SEPTEMBA 2021 HADI NOVEMBA 2022


 Na Ahmed Mahmoud

Mamlaka ya mawasiliano nchini TCRA imetoa leseni 3132 katika makundi aina 6 ikiwemo leseni ndogo za ufungaji utengenezaji uagizaji usambazaji wa vifaa vya simu 2161.

Haya yamesemwa na Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya mawasiliano nchini Dkt. Jabir Bakari wakati akizungumza na waandishi wa habari kuelezea mafanikio ya kudhibiti anga ya mawasiliano nchi kuanzia septemba hadi novemba jijini Dodoma 

Aidha akibainisha Leseni hizo Dkt. Jabir amesema kwamba aina hizo ni pamoja na leseni za miundombinu ya mawasiliano 22, utumiaji wa miundombinu ya mtandao 10,matumizi ya huduma 107,huduma maudhui 741 television  61,mtandao 390 cable TV 65,Radio 218 sanjari na radio mtandao 7.

Kwa mujibu wa Dkt. Bakari ameendelea kuzitaja leseni hizo ni pamoja na Posta na usafirishaji wa vifurushi 91 tofauti na awali 120 huku akibainisha kwamba TCRA inasimamia shughuli za mawasiliano ya simu na inteneti kwa kuhakikisha zinatolewa kwa viwango vya kimataifa vilivyowekwa na EPOCA.

Aidha TCRA inahakikisha mifumo ya usimamizi wa mawasiliano ya simu intaneti kwa serikali kuanzisha mfumo uitwao TTMS ambao husimamia na kuratibu mawasiliano ya simu wenye uwezo wa kubaini takwimu mbalimbali zinazopita katika mitandao ya mawasiliano kwa watoa huduma.

Akabainisha kwamba TCRA imejikita kuhakikisha maudhui yanayorushwa na vituo vya utangazaji nchini yanazingatia weledi maadili wa uandishi wa habari pia hayakiuki sheria na kanuni zinazosimamia sekta ya utangazaji.

Hatahivyo sekta ya mawasiliano ya simu nchini imeendelea kukua hadi kufikia septemba 2022 kulikuwa na laini za simu 58.1 milioni ambazo zinajumuisha laini zinazotumiwa na watu na mashine kwa mashine huku akieleza mikoa inayoongoza ikiwa ni Dar es Salaam laini milion 9.756 Mwanza milion 3.700 Arusha milion 3.448 Mbeya milion 3.089 na Tabora milion 3.060.

Akielezea gharama za muunganisho wa simu kutoka mtandao mmoja kwenda mwingine zimekuwa zikipungua mwaka hadi mwaka 2015 zilikuwa TZS 30.58 na kwa sasa ni TZS 2.00 na kisaidia kupungua gharama za jumka za upigaji simu na kuondoa ulazima wa wateja kuwa na simu zaidi ya moja. 

Kwa muktadha huo licha ya mafanikio hayo sekta hiyo inakumbana na changamoto kadhaa ikiwemo ya uharibifu wa miundombinu ya mawasiliano, utoaji wa huduma za mawasiliano kwa wote maeneo ambayo hayajafikiwa mahitaji makubwa ya bendi za masafa usalama wa mtandao na uhalifu mtandao kudhibiti maudhui ya mtandao na ubora wa huduma za mawasiliano. 

SERIKALI YAKOPA BENKI YA DUNIA BILION 49 KWA AJILI YA MAFUNZO YA UMAHIRI WA TAALUMA YA USAFIRISHAJI




Na Ahmed Mahmoud

SERIKALI imekopa takriban Shilingi bilioni 49 kutoka Benki ya Dunia kwa ajili ya  Kituo cha Umahiri cha Mafunzo ya Taaluma za Usafiri wa Anga na Operesheni za Usafirishaji ambacho kina majukumu ya kutayarisha Wataalam wa Sekta ya Usafiri wa Anga.

Kauli hiyo imetolewa Jijini Dodoma na Mkuu wa Chuo Cha Taifa Cha usafirishaji NIT Prof. Zacharia Mganilwa alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari.

Alisema kuwa Fedha hiyo imegawanywa katika upande wa ujenzi wa  miundombinu kwa ajili ya kufundishia Wataalam na jumla ya majengo matano yatajengwa Dar es Salaam kwa gharama ya Shilingi bilioni 21 na baadae itajenga majengo mkoani Kilimanjaro kwa sababu lazima Marubani wafundishiwe ndani ya Viwanja vya Ndege.

"Fedha nyingine itatumika kununua vifaa vya mafunzo, kwa kuwa Kituo kitafundisha Marubani, Wahandisi wa Ndege, Wahudumu Ndani ya Ndege na Waajiriwa wa Viwanja vya Ndege, chuo kimenunua ndege mbili zenye injini moja za mafunzo ambazo ziko njiani kuja Tanzania kwa gharama ya Shilingi Dola za Marekani milioni 1.2,

Katika Mwaka wa Fedha, 2022/23, Chuo kinanunua tena ndege yenye injini mbili kwa ajili ya mwanafunzi kukamilisha  mafunzo yake kwa sababu  mafunzo ya Urubani yanamtaka mwanafunzi ajifunze ndege yenye injini moja na injini mbili,"alifafanua.

Pia alisema kuwa Kumfundisha Rubani mmoja nje ya nchi ni Shilingi milioni 200, hivyo Serikali inapofanya uwekezaji huo inalifanya Shirika la Ndege Nchini kuleta matumaini ya nchi katika kukuza utalii na uchumi kwa sababu Wataalam wa usafiri wa anga watafundishwa hapa hapa nchini.

"Tanzania ina zaidi ya ndege 400 zilizosajiliwa na Mamlaka ya Usafiri wa Anga ambapo asilimia 60 ya Marubani ni wageni, hivyo ndege hizi zitakapofika vijana wa kitanzania wenye sifa za kusomea Urubani watafundishwa na kupata ajira ndani ya nchi,

Kwa uwekezaji huu unaofanyika, tuna matumaini kuwa Shirika la Ndege la Tanzania litaweza kuwa Shirika bora kwa Afrika,"alieleza.

Alisema kuwa Serikali inaendelea kukuza Uchumi wa Buluu, hivyo kupitia uwekezaji wa mradi wa Benki ya Dunia wameweza kusomesha Wataalam wa kujenga meli na kusanifu meli kwa mara ya kwanza tangu kupatikana kwa Uhuru. Kuanzia mwaka 2023, kutakuwa na vijana ambao tayari wamemaliza masomo hayo.

"Kwa mara ya kwanza tangu tumepata Uhuru, chuo kinafundisha pia Diploma ya Uchomeleaji na Uungaji wa Bomba la Mafuta, hii itasaidia tusipeleke tu madereva na kina mama lishe bali tupeleke pia Wataalam watakaokuwa wanachoma bomba la mafuta,"alisema.

Alisema wana Kituo kingine cha Umahiri cha Kikanda katika usalama Barabarani ambacho kinafadhiliwa na Benki ya Maendeleo ya Afrika kwa Dola za Marekani Milioni 2.1 kwa mradi wote kikiwa na majukumu ya kufanya utafiti wa sababu za ajali na nini kifanyike pamoja na kufundisha Wakufunzi wa Madereva katika ukanda wa Jumuiya ya Afrika Mashariki,Na Kwa mwaka wa masomo wa 2022/23, tunatarajia kufikisha wanafunzi 14,000.

Kwa upande wake Msemaji Mkuu wa Serikali Gerson Msigwa alisema kuwa Serikali iliamua kuwa na Chuo cha Usafirishaji kwa sababu kuendesha vyombo vya moto ni taaluma na ujuzi na kuna miongozo inayotakiwa kuzingatiwa, kinyume cha hapo ni hatari.  

Alisema Safari inayofanywa na Serikali ya Awamu ya Sita ya kuwekeza kwenye maeneo muhimu ya uchumi itategemea sana kuwa na wataalam wetu wa ndani kwani hakutakuwa na kunufaika na thamani ya miradi  kama tunategemea wataalam kutoka nje. 

"NIT watawezesha vijana wetu kunufaika na miradi mikubwa inayoendelea nchini mathalan ndege tano zinazotarajiwa kuja nchini, ambapo kwa mwaka 2023, ndege nne zitaingia nchini,"alisema.

Chuo cha Taifa cha Usafirishaji ni chuo cha elimu ya juu kinachotoa mafunzo kwenye njia kuu zote za uchukuzi na usafirishaji ikiwemo usafiri wa barabara, reli, anga, maji na mifumo ya mabomba,Chuo hiki kinatoa mafunzo, kinafanya utafiti na kinatoa ushauri wa kitaalamu, chuo kinatoa programu za Stashahada 25, Shahada za Kwanza 15, Shahada za Uzamili 3 na Postgraduate Diploma 9.

Chuo kina wafanyakazi 360, kina Wakufunzi mahiri katika Afrika na vifaa vya kisasa. Kwa mwaka wa masomo wa 2021/22, chuo kilikuwa na wanafunzi 13,000.

WATAFITI WAOMBA USHIRIKIANO WA JARIBU NA TAASISI ZA FEDHA SERIKALI KUWASOGELEA KUSIKILIZA SHIDA


Prisca Libaga Maelezo ArushaI

Imeelezwa kwamba changamoto za ushirikiano kati ya taasisi za kifedha na serikali zinawafanya wabunifu kutofikia malengo ya kuongeza uzalishaji na kutofikiwa kwa Masoko.

Akiongea na Wanahabari watafiti na wabunifu wa kanda ya kaskazini waliopatiwa mafunzo na Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH)Mkurugenzi wa Imara Tecknoloji Alfed Changula ambao wamebuni mashine ya kupukuchulia mazao ya nafaka.

Anasema kwamba Imara Tecknoloji inajishughulisha na utengenezaji wa mashine za kilimo wamebuni kutengeneza kwaajili ya kuwauzia wakulima ambapo Imara Tech ilianza Mwaka 2019 na uzalishaji rasmi ulianza Mwaka 2020.




Taasisi hiyo imeweza kuzalisha Ajira 37,Saba za moja kwa moja na 30 vibarua hadi Sasa na mawakala 15 ambao wanauza mashine hizo maeneo mbalimbali kanda ya kaskazini Lengo likiwa ni kufikia kanda zote nchini kwa Uzalishaji wa mashine mbalimbali  ikiwemo ya kupukuchulia mazao ya nafaka na mashine nyingine.


Anaeleza kwamba Imara Tech,imekuwa na mafanikio kwa kuuza mashine 400 na kuwafikia wakulima 400 katika maeneo mbalimbali ambapo wanazalisha Ajira kadhaa kwa maeneo waliouza bidhaa hizo


Anabainisha kwamba hadi Sasa bado wanakumbana na changamoto kadha wa kadha ikiwemo ya ugumu wa kuwafikia viongozi wa serikali kuweza kujitangaza kusogeza Maarifa na uelewa sanjari na kutatua baadhi ya changamoto wanazokutana nazo.



Changula Anabainisha baadhi ya changamoto hizo ni ushirikiano mdogo kutoka serikalini na taasisi za kifedha,ruzuku kwa wakulima itakayosaidia kununua mashine ,ongezeko la mara kwa mara kwa bei za bati ambazo zinazalishia mashine hizo.

Aidha anasema kwamba wamekuwa wakikumbana na changamoto kadhaa ikiwemo ushirikiano na taasisi za kifedha kushindwa kuwasaidia wakulima mikopo pindi wanapohitaji mashine hizo.ilhali wao hawakopeshi kutokana na gharama kubwa kwa za vifaa na bidhaa ikiwemo upandaji wa bei za bati mara kwa mara.

"Utakuta wateja wanahitaji mashine hizo ambazo zimewasaidia vijana kuzalisha ajira kwa kujiajiri kwa kufunga kwenye bodaboda Sasa sisi tunaposhindwa kuwakopesha inakuwa changamoto ambapo tunapoongea na taasisi za kifedha bado hawapo teyari kuwadhamini"



Kwa mujibu wa Chengula Wanufaika wa ufadhili wa fedha za  Utafiti na Ubunifu katika Sayansi na Teknolojia wameeleza kunufaika na ufadhili huo kutoka Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH) Ilizowasaidia kuongeza ufanisi katika maeneo hayo ila wameomba ruzuku hizo kuongezwa ili kusaidia kuongeza uzalishaji.

Anasema kwamba katika fedha ya ruzuku kutoka COSTECH waneweza kununua mashine ya kukatia mabati na fedha nyingine kufanya Utafiti wa Masoko na kufanikiwa kuongeza uhitaji wa wakulima wanaotaka kununua mashine hizo.

Wanaiomba Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH) kuwasaidia kuongeza wigo mpana wa ruzuku sanjari na serikali kuwashika mkono kuweza kuzifikia ndoto zao na kuzishirikisha taasisi za kifedha kuwezesha wakulima kununua mashine hizo ambazo zimekuwa mkombozi kwa wakulima nchini.



"Teknolojia inaposambaa kwa haraka inabadilisha kilimo na kuongeza tija kwa wakulima mashine hizo zinaokoa upotevu wa mazao baada ya mavuno na kuyafanya yawe bora"

Hatahivyo Kituo cha kuhamilisha teknolojia ya zana za kilimo Vijijini, Camartec,kimekuwa ni nguzo ya kutengeneza zana za kilimo na kuziuza kwa wakulima ndani na nje ya nchi ili kurahisisha shughuli za kilimo.

Camartec,Imetoa teknolojia ya uzalishaji zana za kilimo na mashine mbalimbali kwa  taasisi ya Imara tec,iliyowezesha kutengeza mashine mbalimbali na zana za kisasa ambazo zinatumika katika kilimo na kurahisisha uvunaji,kuongeza thamani ya mazao



Kutokana na kuwa ni kisima cha teknolojia Camartec,imeiwezesha kiufundi tasisi ya Imara Tech, kubuni, kusanifu na kutengeneza mashine hizo za kisasa ambazo zinarahisisha shughuli za kilimo  na  kuongezaji thamani ya mazao

Kupitia uwezeshaji huo kutoka Camartec,taasisi ya Imara Tec,imeweza kubuni ,kusanifu na kutengeneza mashine na zana zingine za kilimo na kupata masoko makubwa ya kuuza zana hizo katika nchi za Kenya, Uganda,Rwanda na Burundi

MANDELA YAALIKA WATAFITI KUPELAKA UTAFITI WAO


Na  Mustafa   Leu,Arusha.
TAASISI ya  Chuo Kikuu cha Sayansi na Teknolojia,barani afrika Nelson  Mandela,Imefungua milango kwa baadhi ya watafiti na wagunduzi wa kisayansi ambao tafiti zao hazijafikishwa kwenye taasisi husika kutokana na sababu mbalimbalii kuwasilisha tafiti zao kwenye taasisi hiyo. 


Hii inakuwa ni taasisi ya kwanza ya Wabobezi wa Sayansi na teknolojia barani afrika kufungua milango kwa  watafiti  kuitumia taasisi hiyo kuwasilisha tafiti na gunduzi zao lengo ni kuwaendeleza kwenye tafiti zao 

 
Makamu mkuu wa taasisi hiyo Profesa Anthony Mshandete,anasema kuwa zipo changamoto mbalimbali ambazo zimechangia baadhi ya watafiti kushindwa kuwasilisha tafiti zao na hivyo matokeo ya tafiti zao kuto tambulika kutokana na changamoto hiyo taasisi imefungua milango  kwa watafiti hao .



 Akizungumza na baadhi ya  wanahabari na watafiti  kutoka Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia,(COSTECH,) ofisini kwake kuhusu hatua zinazochukuliwa na taasisi hiyo kuwaendeleza watafiti mbalimbali,Profesa Mshandete, amesema taasisi hiyo inathamini Kazi za utafiti na ugunduzi ili ziweze kuleta maendeleo ya haraka.  


Anasema hiyo ni fursa kwa watafiti nchini ambao walishafanya utafiti na kufanya ugunduzi lakini tafiti zao hawajaziwasilisha kwenye taasisi za kisayansi ili ziweze kutoa matokeo yanayosubiriwa ili zinufaishe  umma. K


Kutokana na changamoto hiyo Taasisi hiyo imeamua kufungua milango na kuwaalika  watafiti waliopo nje ya mfumo  kuwasilisha utafiti na ugunduzi zao na kuwezesha kupiga hatua kubwa ya maendeleo kwenye nyanja ya utafiti.



Amesema watafiti na. wabunifu ni muhimu  katika maisha ya sayansi  kwa kuwa sayansi inaamini katika ugunduzi,utafiti,na namba ambazo hutoa matokeo halisi. 

 Profesa Mshandete,amesema kuwa katika kuendeleza na kuhamasisha maswala ya kutafiti na ugunduzi ,tume ya taifa ya sayansi na teknolojia (COSTECH,) imefadhili taasisi hiyo ili kuendeleza na kukuza teknolojia ya sayansi na utafiti nchini



. Anasema taasisi hiyo inawaibua watafiti na wagunduzi wasiofahamika na kuwaweka mbele kutokana na. kutambua na kuthamini shughuli zao lengo ni kuongeza idadi ya  watafiti wawe wengi

BASHE KUZINDUA MAONESHO YA TANZFOOD EXPRO 2022

Na Ahmed Mahmoud Watanzania wametakiwa kuzalisha bidhaa za Kilimo zinazoendana na masoko ya kimataifa ili kuweza kujingezea kipato na kukamata masoko hayo ya kimataifa Aidha Waziri wa Kilimo Husein Bashe anatarajiwa kuwa mgeni Rasmi katika maonesho ya kimataifa ya kilimo TanzFood Expro 2022 yenye kibwagiz mbiu Ladha ya Tanzania. Akizungumza na waandishi wa habari katika makao makuu ya EAC Jijini Arusha Mkurugenzi wa sekta ya uzalishaji ndani ya Jumuiya ya Afrika masharika Jean Baptiste amesema maonyesho hayo yatafanyika kwa siku tatu kuanzia tarehe 11 hadi 13. Amesema kwa siku tatu watatumia kujenga mtandao wa kibiashara katika mazingira ya kitaalamu na kwamba sekta hii ya kilimo sio kwa ajili ya Tanzania Pekee ndio maana kama Eac na KiliFair Promotion tumeungana ili nchi wanachama wa jumuiya ya Afrika mashariki tutoke na bidhaa zilizo bora. "Bidhaa bora zinahitajika sana ili kuweza kutangaza katika maonyesho haya kutoka kote katika jumuiya itasaidia kuongeza tija ya kuzalisha bidhaa zenye ubora wa kimataifa". Awali Mkrugenzi wa Kilifair Dominic Shoo Alisema kuwa maonesho ya kilimo TanzFood pia yatazinduliwa na Balozi wa Ujerumani nchini Regine Hess na Waziri wa Kilimo Husein Bashe na kuyaleta pamoja makampuni 120 ya hapa nchini na nchi za Eac. Alisema kuwa wanayofuraha kuona waonyeshaji wa ndani na nje ya nchi kutoka masoko mengine kuja kuangalia bidhaa zetu huku akiyataka makampuni ya mbegu na Mashine za kilimo kuleta bidhaa zao katika maonyesho. Kwa Upande wake Mkurugenzi Mwenza wa Kilifair Tom Kunkler alisema kuwa maonesho hayo washiriki watapata fursa ya kupata mafunzo ya kilimo na uzalishaji wa bidhaa ili waweze kushindana katika soko la kimataifa. Alisema kuwa mafunzo hayo kwa wakulima yatawasaidia kuongeza ubora na maendeleo katika sekta ya kilimo ambapo kauli mbiu yake ni Ladha ya Tanzania.

WAZIRI DKT MABULA ATAKA UWAJIBAKI KWA MAKAMISHNA WA ARDHI KUFIKIA MALENGO YA WIZARA

Na Ahmed Mamoud Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula amewataka Makamishna Wasaidizi wa Ardhi wa mikoa nchini kuwajibika na kutumia wajibu wao katika kutekeleza mikakati ya Wizara kufikia malengo. Aidha, amewataka Makamishna hao kuwapangia majukumu kwa malengo maafisa walio chini yao na kufuatilia kazi wanazowapa mara kwa mara. Dkt Mabula amesema, hayo tarehe 25 Februari 2022 wakati akifungua kikao kazi cha Menejiment na Makamishna wa Ardhi Wasaidizi wa mikoa kilichofanyika ofisi ya Mkuu wa mkoa wa Arusha. ‘’Yapo malamiko ya lugha zisizofaa kwa wateja, hii haikubaliki fuatilieni hili na kulikemea vikali na kuzingatia misingi na kanuni za utumishi wa umma katika majukumu yenu ya kila siku ’’ alisema Dkt Mabula. Aidha, aliwataka katika utekelezaji mpango mkakati wa wizara wanazingatia vipaumbele vya serikali hususan maelekezo ya mhe. Rais Samia Suluhu Hassan na ukusanyaji wa maduhuli ya serikali kupitia kodi ya pango la ardhi. Akigeukia suala la makusanyo ya kodi ya pango la ardhi, Waziri wa Ardhi aliwataka Makamishna wa ardhi Wasaidizi wa mikoa kuwa wabunifu katika njia za kukusanya mapato. ‘’Sula la mtandao kutopataikana muda mwingi linaonekana kuwa kikwazo katika ukusanyaji maduhuli, lifanyieni kazi’’ alisema Dkt Mabula. Waziri Dkt Mabula pia alihimiza kuongezwa kwa kasi ya umilikishaji ardhi na kuwataka Makamishna hao na wakuu wa idara katika wizara kuweka malengo kwa kila ofisa mwenye taaluma ya ardhi kuandaa hati. Kwa upande wake Katibu Mkuu Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Allan Kijazi alisema baada ya kuteuliwa alifanya ziara katika baadhi ya mikoa na kukutana na baadhi ya changamoto alizozitaja kuwa ni pamoja na kutofikiwa malengo ya ukusanyaji kodi ya ardhi pamoja na baadhi ya halmashauri kutohudumia idara za ardhi kwa madai ya idara hizo kuhamishiwa wizarani. ‘’Nimeanza kuchukua hatua ili kutatua changamoto hizo ambapo tayari nimetoa maagizo mbalimbali kwenye mikoa na menejimenti ya wizara na ni matarajio kikao kazi kutaibua suluhisho la changamoto hizo’’ alisema Dkt Allan Kijazi. Kwa mujibu wa Dkt Kijazi, Wizara ya Ardhi imekuwa ikinyooshewa vidole na wananchi kwa masuala ya ukiukwaji wa haki za wananchi na kuchafua taswira ya Wizara na kutaka watendaji wa sekta ya ardhi kujitafakari na kujisahihisha kwa kutimiza wajibu ili kuondoa dhana hiyo. Aligusia pia mpango wa urasimishaji makazi holela na kueleza kuwa, ni matarajio yake kupitia kikoa hicho washirikia wataibuka na mkakati wa uelekeo wa wizara katika kupanga miji sambamba na usimamamia fedha zilizotolewa kwa ajili ya mpango wa kupanga, kupima na kumilikisha ardhi maarufu kama KKK.

MASHINDANO SED MISS VALENTINE'S 2022 KUFANYIKA KESHO

Mashindano ya Sed Miss Valentine's 2022 yatafanyika kesho februari 14 mwaka 2022 Mjini Babati Mkoani Manyara huku warembo 15 wanatarajiwa kuchuana vikali kutwaa taji hilo. Afisa Masoko wa Kiwanda cha Mati Super Brand Gwandumi Mpoma ambao ndio wadhamini wakuu wa mashindano hayo wamesema kuwa wamejipanga kuhakikisha wakazi wa Babati wanafurahia mashindano hiyo amewataka wajitokeze kwa wingi. Gwandumi amesema kuwa Mashindano hayo yanalenga kuibua vipaji vya vijana na kuwapa fursa ya kufanya kazi na kiwanda hicho kupitia bidhaa mbali mbali wanazozalisha ikiwemo Strong Gin,Sed Pinepale na Tanzanite Premium Vodka. Hamisi Saidi ni Moja kati ya waandaaji wa Mashindano ya Sed Miss Valentine amesema kuwa warembo wamejiandaa vizuri katika kambi hiyo na wanatarajia ushindani utakua mkali kutokana na maandalizi waliyoyafanya. wa Upande wao washiriki wa Mashindano hayo Jenifer Paulo Mmari na Keithwin Pallangyo wamepongeza udhamini wa kampuni ya Mati Super Brands Limited kwa kuwawezesha kukaa kambini na kujiandaa vyema hivyo wamewataka wakazi Mkoa wa Manyara na Mikoa jirani kujitokeza kwa wingi.