KURASA ZA MAGAZETI YA HARDNEWS NA BURUDANI IJUMAA JULAI MOSI ,2016

IMG_20160701_045230
IMG_20160701_045248
IMG_20160701_045307
IMG_20160701_045327
IMG_20160701_045353
IMG_20160701_045417
IMG_20160701_045438
IMG_20160701_045502
IMG_20160701_045521
IMG_20160701_045541
IMG_20160701_045618
IMG_20160701_045648
IMG_20160701_045703
IMG_20160701_045810
IMG_20160701_045841
IMG_20160701_045903
IMG_20160701_045917
IMG_20160701_045937
IMG_20160701_045954
IMG_20160701_050010
IMG_20160701_050029
IMG_20160701_050107

RC MAKALA AAGIZA KUKAMATWA KWA MKANDARASI WA UJENZI WA UWANJA WA NDEGE WA SONGWE BAADA YA KUSHINDWA KULIPA MAFAO YA VIBARUA ZAIDI YA 50.

Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Amos Makalla,akitolea ufafanuzi na kujibu kero mbalimbali zilizotolewa na wananchi wa Mkoa wa Mbeya, katika kikao maalum cha kupokea kero za wananchi kilichofanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa Mkapa, ambapo kubwa zaidi katika siku hii, Makala amesema serikali itahakikisha inamkamata mkandarasi wa ujenzi wa uwanja wa ndege wa Songwe kutoka kampuni ya Kundan Sigh, baada ya kushindwa kulipa mafao ya vibarua zaidi ya 50. 
Na Emanuel Madafa, Mbeya.
Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Amos Makalla ameagiza kukamatwa kwa mmiliki wa kampuni ya Kundan Singh, ambaye alipewa tenda ya kujenga uwanja wa ndege wa Songwe, baada ya kushindwa kulipa mafao ya vibarua zaidi ya 50.


Mkuu huyo wa Mkoa wa Mbeya ametoa kauli hiyo , wakati akijibu na kutatua kero mbalimbali za wananchi ambazo hazijapatiwa ufumbuzi kwa kipindi kirefu, hali iliyochangia wananchi kuichukia serikali kwa madai ya kushindwa kuwatendea haki.

Awali, akitoa malalamiko hayo kwa Mkuu wa Mkoa, Joshua Mwasilonde kwa niaba ya vibarua wenzake, amesema wamekuwa wakidai mafao yao tangu mwaka 2012/2013 katika mfuko wa hifadhi ya jamii NSSF na kwamba kila wanapofuatilia wamekuwa wakipigwa kalenda.
Akilizungumzia hilo, Makala amesema, kwakua serikali iliingia mkataba na kampuni hiyo na kumalizana nayo bila ya kuacha deni lolote hivyo mkandarasi huyo anapaswa kuwalipa vibarua hao na kuutaka uongozi wa NSSF, kuhakikisha unavishirikisha vyombo vya dola katika kumkamata mkandarasi huyo.
Meneja NSSF Kanda ya Nyanda za Juu kusini, Robert Kadege, akilitolea ufafanuzi suala hilo, amesema suala la vibarua hao linafanyiwa kazi na kwamba tayari mahakama imetoa hukumu na kuupa ushindi mfuko huo.
Katibu tawala Mkoa wa Mbeya Mariam Mtunguja, akitolea ufafanuzi baadhi ya masuala ya kiutendaji katika kikao hicho. 
Baadhi ya wananchi waliofika kutoa kero na malalamiko katika kikao hicho.
Baadhi ya viongozi na watendaji wa serikali katika kikao maalum cha kupokea kero za wananchi kilichofanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa Mkapa June 29 mwaka huu. 
Baadhi ya wananchi wakitoa malalamiko na kero zao katika kikao maalum cha kupokea kero za wananchi kilichofanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa Mkapa June 29 -2016 ambapo MKuu wa Mkoa wa Mbeya Amos Makalla ndiye aliyepokea kero hizo sanjali na watendaji wa serikali na taasisi mbalimbali za serikali.
Kikao kikiendelea.(Picha E.Madafa).

KURASA ZA MAGAZETI YA UDAKU NA BURUDANI IJUMAA JULAI MOSI,2016

IMG_20160701_044856
IMG_20160701_044958
IMG_20160701_045014
IMG_20160701_045030
IMG_20160701_045047
IMG_20160701_045102
IMG_20160701_045121
IMG_20160701_045137
IMG_20160701_045153
IMG_20160701_045212

Dkt. Mahiga akutana na Waziri wa Mambo ya Nje wa Rwanda


Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi Dkt. Augustine Mahiga (kulia) akizungumza na Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Rwanda, Mhe.Loiuse Mushikiwabo, alipomtembelea leo katika Ofisi za Wizara Jijini Dar es Salaam. Mazungumzo yao yalijikita katika kuimarisha na kuboresha mahusiano yaliyopo baina ya nchi hizo mbili, pamoja na Ziara ya Rais wa Jamhuri ya Rwanda Mhe. Paul Kagame anayetarajiwa kuwasili nchini kesho kwa ziara ya siku mbili. 
Kaimu Mkuu wa Itifaki katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Bw. James Bwana alipokuwa akimkaribisha Mhe. Waziri Mushikiwabo mara baada ya kuwasili Wizarani. 
Kutoka kushoto ni Mkurugenzi wa Idara ya Afrika katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi Samuel Shelukindo, akiwa na Kaimu Mkuu wa Itifaki, Bw. James Bwana na Afisa Mambo ya Nje, Bw. Medard Ngaiza wakifuatilia mazungumzo.
Balozi wa Jamhuri ya Rwanda nchini, Mhe. Eugene Kayihura (kulia) pamoja na Afisa aliyeambatana na Mhe. Waziri Mushikiwabo wakifuatilia mazungumzo.
Wakati mazungumzo yakiendelea.
Wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya mazungumzo.

WAZIRI UMMY MWALIMU, MELINDA GATES WAYAPONGEZA MASHINDANO YA MAMA SHUJAA WA CHAKULA YANAYO ENDESHWA NA OXFAM TANZANIA


Mwenyekiti mwenza wa taasisi ya Bill and Melinda Gates ya Marekani Bi. Melinda Gates akiongea na wadau mbalimbali na kulipongeza shirika la Kimataifa la Oxfam Tanzania kwa kuendesha Shindano la Mama Shujaa wa Chakula ambalo lengo kubwa ni kuwawezesha wakulima wadogo wadogo wanawake kufanikiwa katika Kilimo cha chakula na umiliki wa ardhi.
Mkurugenzi Mkazi wa Oxfam Tanzania Jane Foster akitoa neno la utangulizi wakati wa sherehe hiyo.
Waziri wa Afya,Jinsia,Wazee na Watoto Mh. Ummy Mwalimu akilipongeza Shirika la Kimataifa la Oxfam Tanzania kwa kuendesha Shindano la Mama Shujaa wa Chakula ambalo linaonesha changamoto za wazalishaji wa chakula wadogo ikiwemo umiliki wa ardhi.
Dkt. Eve Marie akizungumza kwa kina ni jinsi gani Serikali na Sekta binafsi zinaweza kuwekeza katika wakulima wadogo wadogo hasa wanawake  ili kuongeza uzalishaji wa Chakula.
Muwezeshaji kutoka Forum CC Faizal Issa akielezea namna wakulima ambavyo wanaweza kukabiliana na mabadiliko ya Tabianchi ambayo kwa sasa yanaathiri kwa kiasi kikubwa katika uzalishaji katika kilimo.
Mwanamuziki maarufu wa Muziki wa kizazi kipya Bongo Fleva Mwasiti akitumbuiza wakati wa Sherehe hizo.