MAJALIWA ATEMBELEA UWANJA WA JAMHURI MJINI DODOMA KUKAGUA MAADALIZI YA SHEREHE ZA MUUNGANO


Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizngumza baada ya kutembelea na kukagua maadalizi ya uwanja wa Jamhuri mjini Dodoma Aprili 24, 2017. Katikati ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Jenista Mhagama na kushoto ni Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu, Dkt.Hamisi Mwinyimvua. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akimsikiliza Bw.Yusto Chuma (kulia) ambaye ni mmoja wa wajumbe wa kamati ya Maandalizi ya Sherehe za Muungano wakati alipotembelea uwanja wa Jamhuri mjini Dodoma zitakapofanyika sherehe hizo ili kujionea maandalizi hayo, Aprili 24, 2017. Kushoto kwake ni Waziri wa nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Jenista Mhagama . (Picha na Ofisi ya ` Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akimsikiliza  Bw.Yusto Chuma (kulia) ambaye ni  mmoja wa  wajumbe wa kamati ya Maandalizi ya  Sherehe za Muungano wakati alipotembelea uwanja wa Jamhuri mjini Dodoma Aprili 24, 2017 zitakapofanyika sherehe hizo.  Kushoto kwake ni  Waziri wa nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Jenista Mhagama na Kulia ni Naibu Waziri wa nchi, Ofisi ya Rais TAMISEMI, Selemani Jafo. (Picha na Ofisi ya ` Waziri Mkuu)

JIMBO LA ARKANSAS LATEKELEZA ADHABU YA KIFO KWA WAFUNGWA WAWILI


Jimbo la Arkansas limewatekelezea adhabu ya kifo wafungwa wawili kwa siku moja waliohukumiwa adhabu ya kifo baada ya Mahakama ya Juu kukataa pingamizi lao la dakika za mwisho.

Wafungwa hao Jack Jones na Marcel Williams wote walihukumiwa adhabu ya kifo kwa makosa ya ubakaji na mauaji waliyoyatenda katika miaka ya 1990.

Jimbo la Arkansas limepanga kutekeleza adhabu ya kifo kwa watuhumiwa nane baada ya kubaini kuwa dawa ya sindano wanayotumia kuulia inaisha muda wake wa matumizi mwisho wa wezi huu.

Hii ni mara ya kwanza kutekelezwa kwa adhabu ya kifo kwa wafungwa wawili katika siku moja tangu kupita miaka 17 nchini Marekani.

                                         Kitanda maalum kwa ajili ya kutekelezea adhabu ya kifo

MKUU WA WILAYA YA KISHAPU AFANYA ZAIARA KATA YA MASANGA NA KUZUNGUMZA NA WANANCHI, APIGA MARUFUKU UUZAJI WA CHAKULA


Mkuu wa Wilaya Kishapu mkoani Shinyanga, Nyabaganga Taraba amepiga marufuku wananchi kuuza mazao ya chakula wanayovuna hususan mtama na badala yake waweke akiba. 

Taraba alipiga marufuku hiyo jana wakati akifanya ziara katika kata za Lagana, Mwamashele, Mwakipoya na Masanga baada ya kubaini kuwepo kwa baadhi ya wananchi kufanya biashara hiyo. 

Akizungumza kwenye mkutano wa hadhara katika kata ya Masanga alisema kuna baadhi ya watu huwahadaa na kununua mtama kwa bei ya juu hali inayowafanya wananchi wabaki bila chakula. 

“Nasikia hapa kuna baadhi watu wanapita kwenu wananchi na kununua debe moja la mtama kwa shilingi elfu ishirini na tano msidanganyie na kuuza wewkeni akiba,” alisisitiza mkuu huyo wa wilaya. 

Aidha alionya tabia ya baadhi ya watu kuuza mazao yakiwa shambani baada ya kukadiriwa kiasi cha mazao yao kabla ya kuyavuna aliwataka wananchi wakatae kufanya hivyo. 

Kwa upande mwingine aliwataka kuandaa mashamba yao mapema na kupanda mazao yanayohimili ukame yakiwemo mtama ili yaweze kustawi na kuwapa chakula. 

Taraba aliwataka wananchi hao kuwatumia wataalamu wa kilimo kwenye kata zao ili kupata ushauri wa kutumia mbegu zilizo bora ambazo zinaweza kuota na kukua kwa haraka.
Mkuu wa Wilaya ya Kishapu, Nyabaganga Taraba (katikati) akizungumza na wananchi (hawapo pichani) katika mkutano wa hadhara kata ya Masanga. kulia ni Afisa Kilimo (Ubora wa mbegu), Maduhu Masunga 
Mkuu wa Wilaya ya Kishapu, Nyabaganga Taraba (katikati) akizungumza na wananchi (hawapo pichani) katika mkutano wa hadhara kata ya Masanga. Wengine pichani kulia ni Afisa Kilimo (Ubora wa mbegu), Maduhu Masunga na Mwenyekiti wa kijiji cha Masanga, Gambishi Malele. 
Mwananchi wa kata ya Masanga akitoa kero yake kwa Mkuu wa Wilaya, Nyabaganga Taraba wakati wa mkutano wa hadhara. 
Mkuu wa Wilaya ya Kishapu, Nyabaganga Taraba akizungumza na wajumbe aliowakuta wakifanya kikao cha kujadili maendeleo ya kata, Mwamashele alipokuwa katika ziara ya kutembelea kata tatu. 
Mwananchi wa kata ya Masanga akitoa kero yake kwa Mkuu wa Wilaya, Nyabaganga Taraba wakati wa mkutano wa hadhara. 
Mkuu wa Wilaya ya Kishapu, Nyabaganga Taraba akizungumza na wananchi wa kata ya Masanga katika mkutano wa hadhara. Wengine pichani ni kuanzia kushoto ni Afisa Tawala wa Ofisi ya Mkuu wa Wilaya, Juvenalis Beyakwasho, Mtendaji Kata wa Masanga, John Zablon, na Mwenyekiti wa kijiji cha Masanga, Gambishi Malele. 
Mkuu wa Wilaya ya Kishapu, Nyabaganga Taraba akizungumza na wananchi wa kata ya Masanga katika mkutano wa hadhara. Wengine pichani ni kuanzia kushoto ni Afisa Tawala wa Ofisi ya Mkuu wa Wilaya, Juvenalis Beyakwasho, Mtendaji Kata wa Masanga, John Zablon, na Mwenyekiti wa kijiji cha Masanga, Gambishi Malele. 

RAIS DKT. MAGUFULI AWEKA JIWE LA MSINGI UJENZI WA RELI YA KISASA STANDARD GAUGE KUTOKA DAR HADI MOROGORO


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Waziri wa Ujenzi Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa pamoja na Mkewe Mama Janeth Magufuli akikata utepe kuashiria uzinduzi wa Ujenzi wa Reli ya Kisasa Standard Gauge itakayoanzia jijini Dar es Salaam hadi mkoani Morogoro na baadaye kuendelea hadi mikoa ya Kigoma na Mwanza
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Waziri wa Ujenzi Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa akiweka jiwe la msingi Ujenzi wa Reli ya Kisasa Standard Gauge itakayoanzia jijini Dar es Salaam hadi mkoani Morogoro na baadaye kuendelea hadi Kigoma na Mwanza.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiangalia majina ya baadhi ya wataalamu mbalimbali waliohusika katika mchakato wa Ujenzi huo wa Reli ya Kisasa Standard Gauge itakayoanzia jijini Dar es Salaam hadi mkoani Morogoro na baadaye kuendelea hadi Kigoma na Mwanza. Wakwanza kulia ni Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni hodhi ya Rasilimali za Reli (RAHCO) Masanja Kadogosa akiwa ameshika majina hayo
Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli akichota mchanga na kuweka kama ishara ya kushiriki katika ujenzi huo wa Reli ya Kisasa Standard Gauge itakayoanzia jijini Dar es Salaam hadi mkoani Morogoro na baadaye kuendelea hadi Kigoma na Mwanza.Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiangalia kibao cha jiwe la msingi cha Ujenzi wa Reli ya Kisasa Standard Gauge itakayoanzia jijini Dar es Salaam hadi mkoani Morogoro na baadaye kuendelea hadi Kigoma na Mwanza

BUNGE- MAJALIWA AHITIMISHA MAKADIRIO YA BAJETI YA OFISI YA WAZIRI MKUU


Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisoma hotuba ya kuhitimisha Hoja yake ya Makadirio ya Matumizi ya Ofisi ya Waziri Mkuu kwa Mwaka 2017/2018, bungeni mjini Dodoma Aprili 12, 2017. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
jal2
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Jenista Mhagama (kushoto) na Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Anthony Mavunde wakimsikiliza Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa wakati alipohitimisha Hoja yake ya Makadirio ya matumizi ya Ofisi ya Waziri Mkuu kwa Mwaka 2017/2018, bungeni mjini Dodoma Aprili 12, 2017 . (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
jal3
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisoma hotuba ya kuhitimisha Hoja yake ya Makadirio ya Matumizi ya Ofisi ya Waziri Mkuu kwa Mwaka 2017/2018, bungeni mjini Dodoma Aprili 12, 2017. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

KUMBUKUMBU YA HAYATI SOKOINE WILAYANI MONDULI


Msaidizi wa Askofu, jimbo kuu Katoliki Arusha, Prosper Lyimo akiweka shada la maua kwenye kaburi la Waziri Mkuu wa zamani, Hayati Edward Moringe Sokoine wakati wa ibada ya kumbukumbu ya kifo cha kiongozi huyo miaka 33 iliyopita, iliyofanyika nyumbani kwa Sokoine wilayani Monduli.
pam2
Waziri wa Maliasili na Utalii, Profesa Jumanne Maghembe akisaini kitabu cha wageni mara baada ya kuwasili kwenye ibada ya kuadhimisha miaka 33 ya kifo cha aliyekuwa waziri mkuu wa Tanzania, Hayati Edward Sokoine, wilayani Monduli.
pam3
Mke wa kwanza wa Sokoine Mama Napono katrika, na wa pili Mama Nekiteto kulia, wakizungumza na waziri wa maliasili na utalii Jumanne Maghembe nyumbani Wilayani Monduli
pam4
Msaidizi wa Askofu, Prosper Lyimo akihubiri wakati wa ibada ya kuadhimisha miaka 33 ya kifo cha Waziri Mkuu wa Zamani, Edward Sokoine
pam5
Binti wa Sokoine, Namelok na Kaka yake, Balozi Joseph Sokoine wakiwa na wageni wengine walioshiriki ibada ya kumbukumbu ya baba yao wilayani Monduli.
pam6
Wake za marehemu wakiwa wanaweka taji katika kaburi la Hayati Edward Sokoine, wilayani Monduli.
pam7Waziri wa Maliasili na Utalii, Profesa Jumanne Maghembe akiwa anaweka taji katika kaburi la Hayati Edward Sokoine, wilayani Monduli ya kifo cha kiongozi huyo miaka 33 iliyopita, iliyofanyika nyumbani kwa Sokoine

pam8
Mwakilishi wa mkuu wa Majeshi Tanzania, Brigadia Jenerali, Anderson Ghulila akiwa anaweka taji katika kaburi la Hayati Edward Sokoine, wilayani Monduli katika ibada ya kumbukumbu ya kifo cha kiongozi huyo miaka 33 iliyopita, iliyofanyika nyumbani kwa Sokoine
pam9
Wajukuu wa Hayati Edward Sokoine wakiwa katika ibada ya kumbukumbu ya kifo cha kiongozi huyo miaka 33 iliyopita, iliyofanyika nyumbani kwa Sokoine
pam10
Mtoto wa Hayati Sokoine, Balozi Joseph Sokoine akizungumza na wageni waalikwa katika misa maalum ya kumuenzi baba yake.
pam11
Baadhi ya wageni kutoka sehemu mbalimbali waliohudhuria misa ya kumbukumbuku ya Sokoine.
pam12
Mkuu wa Mkoa wa Njombe, Christopher Ole Sendeka akibadilishana mawazo na mwakilishi wa mkuu wa Majeshi Tanzania, Brigadia Jenerali, Anderson Ghulila pamoja aliyewahi kuwa mkuu wa mkoa wa Arusha, Balozi Daniel Ole Njoolay
pam13
Baadhi ya viongozi walioshiriki ibada ya kumbukumbu ya miaka 33 ya Sokoine, kutoka kushoto ni Askofu wa Dayosisi ya Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Mkoani Arusha, Solomon Masagwa, Mwakilishi wa Shehe Mkuu, Rajab Kiungiza, Mkuu wa Mkoa wa Njombe, Christopher Ole Sendeka na Waziri wa Maliasili na Utalii Jumanne Maghembe kwenye picha ya pamoja
pam14
Wanakwaya wakiandamana kuelekea eneo la ibada tayari kwa Misa Maalum.

BODI YA ZABUNI YA WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI YAIPA WIKI TANO KAMPUNI YA UJENZI YA KOBERG KUKAMILISHA UJENZI WA NYUMBA ZA MAKAMISHNA WA UHAMIAJI, JIJINI D’SALAAM


Mwenyekiti wa Bodi ya Zabuni ya Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia ni Kamishna wa Fedha na Utawala wa Magereza, Gaston Sanga (watatu kushoto), Katibu wa Bodi hiyo ambaye pia ni Mkurugenzi wa Manunuzi wa Wizara hiyo, David Mwangosi wakimsikiliza Mkuu wa Kitengo cha Majengo wa Idara ya Uhamiaji, Hamza Shabani (kushoto), wakati wajumbe wa Bodi hiyo walipotembelea nyumba za makazi za Makamishna wa Uhamiaji, Mtoni Kijichi, jijini Dar es Salaam. Bodi hiyo ilitoa wiki tano kwa Kampuni ya Ujenzi ya Koberg kukamilisha ujenzi wa nyumba hizo. Picha zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi
Katibu wa Bodi ya Zabuni, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia Mkurugenzi wa Manunuzi wa Wizara hiyo, David Mwangosi akiwafafanulia jambo Wajumbe wa Bodi ya Zabuni ya Wizara hiyo, wakati wajumbe hao walipofanya ziara ya kukagua ujenzi wa nyumba za makazi ya makamishna wa Uhamiaji zilizopo Mtoni Kijichi, jijini Dar es Salaam. Hata hivyo, Wajumbe wa Bodi hiyo walitoa wiki tano kwa Kampuni ya Ujenzi ya Koberg kukamilisha ujenzi wa nyumba hizo. Kulia ni Mwenyekiti wa Bodi hiyo, ambaye pia ni Kamishna wa Fedha na Utawala wa Magereza, Gaston Sanga. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Mwenyekiti wa Bodi ya Zabuni, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia ni Kamishna wa Fedha na Utawala wa Magereza, Gaston Sanga (kushoto) akiangalia kabati la nguo katika moja ya chumba cha nyumba za makamishna wa Uhamiaji zilizopo Mtoni Kijichi, jijini Dar es Salaam. Wajumbe wa Bodi hiyo walizikagua nyumba hizo na kutoa wiki tano kwa Kampuni ya Ujenzi ya Koberg kukamilisha ujenzi. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Mkuu wa Kitengo cha Majengo wa Idara ya Uhamiaji, Hamza Shabani akiwaonyesha Wajumbe wa Bodi ya Zabuni ya Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, nyumba za makazi za makamishna wa Uhamiaji zilizopo Mtoni Kijichi, jijini Dar es Salaam. Wapili kushoto ni Mwenyekiti wa Bodi hiyo, ambaye pia ni Kamishna wa Fedha na Utawala wa Magereza, Gaston Sanga. Wapili kulia ni Katibu wa Bodi hiyo ambaye pia ni Mkurugenzi wa Manunuzi wa Wizara hiyo, David Mwangosi, watatu kulia ni Kamishna wa Fedha na Utawala wa Uhamiaji, Peter Chogero, na kulia ni Mhasibu Mkuu wa Wizara hiyo, Edwin Makene. Picha zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.

Mhandisi wa Kampuni ya Ujenzi ya Koberg ambayo inajenga nyumba za makazi za Makamishna wa Idara ya Uhamiaji, Leonard Leonidace, akiwafafanulia jambo Wajumbe wa Bodi ya Zabuni ya Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, walipozitembelea nyumba hizo wakikagua maendeleo ya ujenzi wa nyumba hizo, hata hivyo Wajumbe wa Bodi walitoa wiki kwa Kampuni hiyo kukamilisha ujenzi. Kulia ni Mwenyekiti wa Bodi ya Zabuni, Wizara hiyo ambaye pia ni Kamishna wa Fedha na Utawala wa Magereza, Gaston Sanga, na wanne kulia ni Katibu wa Bodi hiyo ambaye pia ni Mkurugenzi wa Manunuzi wa Wizara hiyo, David Mwangosi. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Mwenyekiti wa Bodi ya Zabuni, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia ni Kamishna wa Fedha na Utawala wa Magereza, Gaston Sanga (Katikati) na Katibu wa Bodi hiyo ambaye pia ni Mkurugenzi wa Manunuzi wa Wizara hiyo, David Mwangosi (wanne kulia), wakiwa katika picha ya pamoja na Wajumbe wa Bodi hiyo, mara baada ya wajumbe hao kumaliza ziara yao ya kukagua ujenzi wa nyumba za makazi za Makamishna wa Idara ya Uhamiaji, zilizopo Mtoni Kijichi, jijini Dar es Salaam. Hata hivyo, Wajumbe wa Bodi hiyo walitoa wiki tano kwa Kampuni hiyo kukamilisha ujenzi wa nyumba hizo. Picha zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.

IMEANDALIWA NA KITENGO CHA MAWASILIANO YA SERIKALI

WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI