BODI YA ZABUNI YA WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI YAIPA WIKI TANO KAMPUNI YA UJENZI YA KOBERG KUKAMILISHA UJENZI WA NYUMBA ZA MAKAMISHNA WA UHAMIAJI, JIJINI D’SALAAM


Mwenyekiti wa Bodi ya Zabuni ya Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia ni Kamishna wa Fedha na Utawala wa Magereza, Gaston Sanga (watatu kushoto), Katibu wa Bodi hiyo ambaye pia ni Mkurugenzi wa Manunuzi wa Wizara hiyo, David Mwangosi wakimsikiliza Mkuu wa Kitengo cha Majengo wa Idara ya Uhamiaji, Hamza Shabani (kushoto), wakati wajumbe wa Bodi hiyo walipotembelea nyumba za makazi za Makamishna wa Uhamiaji, Mtoni Kijichi, jijini Dar es Salaam. Bodi hiyo ilitoa wiki tano kwa Kampuni ya Ujenzi ya Koberg kukamilisha ujenzi wa nyumba hizo. Picha zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi
Katibu wa Bodi ya Zabuni, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia Mkurugenzi wa Manunuzi wa Wizara hiyo, David Mwangosi akiwafafanulia jambo Wajumbe wa Bodi ya Zabuni ya Wizara hiyo, wakati wajumbe hao walipofanya ziara ya kukagua ujenzi wa nyumba za makazi ya makamishna wa Uhamiaji zilizopo Mtoni Kijichi, jijini Dar es Salaam. Hata hivyo, Wajumbe wa Bodi hiyo walitoa wiki tano kwa Kampuni ya Ujenzi ya Koberg kukamilisha ujenzi wa nyumba hizo. Kulia ni Mwenyekiti wa Bodi hiyo, ambaye pia ni Kamishna wa Fedha na Utawala wa Magereza, Gaston Sanga. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Mwenyekiti wa Bodi ya Zabuni, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia ni Kamishna wa Fedha na Utawala wa Magereza, Gaston Sanga (kushoto) akiangalia kabati la nguo katika moja ya chumba cha nyumba za makamishna wa Uhamiaji zilizopo Mtoni Kijichi, jijini Dar es Salaam. Wajumbe wa Bodi hiyo walizikagua nyumba hizo na kutoa wiki tano kwa Kampuni ya Ujenzi ya Koberg kukamilisha ujenzi. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Mkuu wa Kitengo cha Majengo wa Idara ya Uhamiaji, Hamza Shabani akiwaonyesha Wajumbe wa Bodi ya Zabuni ya Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, nyumba za makazi za makamishna wa Uhamiaji zilizopo Mtoni Kijichi, jijini Dar es Salaam. Wapili kushoto ni Mwenyekiti wa Bodi hiyo, ambaye pia ni Kamishna wa Fedha na Utawala wa Magereza, Gaston Sanga. Wapili kulia ni Katibu wa Bodi hiyo ambaye pia ni Mkurugenzi wa Manunuzi wa Wizara hiyo, David Mwangosi, watatu kulia ni Kamishna wa Fedha na Utawala wa Uhamiaji, Peter Chogero, na kulia ni Mhasibu Mkuu wa Wizara hiyo, Edwin Makene. Picha zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.

Mhandisi wa Kampuni ya Ujenzi ya Koberg ambayo inajenga nyumba za makazi za Makamishna wa Idara ya Uhamiaji, Leonard Leonidace, akiwafafanulia jambo Wajumbe wa Bodi ya Zabuni ya Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, walipozitembelea nyumba hizo wakikagua maendeleo ya ujenzi wa nyumba hizo, hata hivyo Wajumbe wa Bodi walitoa wiki kwa Kampuni hiyo kukamilisha ujenzi. Kulia ni Mwenyekiti wa Bodi ya Zabuni, Wizara hiyo ambaye pia ni Kamishna wa Fedha na Utawala wa Magereza, Gaston Sanga, na wanne kulia ni Katibu wa Bodi hiyo ambaye pia ni Mkurugenzi wa Manunuzi wa Wizara hiyo, David Mwangosi. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Mwenyekiti wa Bodi ya Zabuni, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia ni Kamishna wa Fedha na Utawala wa Magereza, Gaston Sanga (Katikati) na Katibu wa Bodi hiyo ambaye pia ni Mkurugenzi wa Manunuzi wa Wizara hiyo, David Mwangosi (wanne kulia), wakiwa katika picha ya pamoja na Wajumbe wa Bodi hiyo, mara baada ya wajumbe hao kumaliza ziara yao ya kukagua ujenzi wa nyumba za makazi za Makamishna wa Idara ya Uhamiaji, zilizopo Mtoni Kijichi, jijini Dar es Salaam. Hata hivyo, Wajumbe wa Bodi hiyo walitoa wiki tano kwa Kampuni hiyo kukamilisha ujenzi wa nyumba hizo. Picha zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.

IMEANDALIWA NA KITENGO CHA MAWASILIANO YA SERIKALI

WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni