Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mrisho Gambo akizungumza na waandishi wa habarimapema leo ofisini kwake .Picha na mahmoud ahmad. |
Meneja wa TRA Mkoa wa Arusha Pili Mbaruku akifafanua jambo mbele ya waandishi wa habari mapema leo katika mkutano ulioitishwa na mkuu wa mkoa kwa waandishi wa habari.
Na.Mahmoud Ahmad .Arusha
Wananchi wametakiwa kulipa kodi ya majengo ili kuepuka usumbufu unaoweza kujitokeza baadae kutokana na Sera ya serikali inayisema kila mwananchi inayomraka takiwa kulipa kodi ya majengo.
Hayo
yamesemwa na mkuu wa mkoa wa Arusha Mrisho Gambo
alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari leo ofisini kwake na kusema
kuwa yapo makundi matatu yanayoaanishwa katika ulipwaji wakodi
hizo
Hata
hivyo amesema makundi hayo ni Pamoja na wale ambao
nyumba zao hazijapimwa wala kufanyiwa tathimini,kundi la pili in wale
ambao nyumba zao zimepimwa lakini hazijafanyiwa tathimini kundi la
mwisho no wale ambao nyumba zao zimepimwa na kufanyiwa tathimini.
Hata
hivyo amesema kundi la kwanza linatakiwa kulipa
shilingi elfu 15,000kwa mwaka,ambapo kundi la pili wanatakiwa kulipa
waendelee kulipa Kwa utaratibu waliokuwa wanautumia toka awali,kundi la
tatu gharama zao zipo juu kulingana na tathimini mpya iliyofanyika mwaka
2015-2016.
Vilevile
Gambo ametoa onyo kali Kwa wanasiasa wenye tabia
ya kupita Kwa wananchi na kuwapotosha kuhusiana na ulipaji wa kodi hiyo
amesema hatua Kali za kisheria zitachukuliwa endapo watambaini mmoja
wapo.
Nae
meneja wa TRA mkoa wa Arusha Pili Mbaruku amesema kuwa
wamejiwekea utaratibu mzuri kuhakikisha wanashirikiana na watendaji wa
mitaa ili zoezi la ukusanyaji liwe jepesi kwao badala ya kupanga foleni
TRA jambo ambalo litawqchukulia muda wananchi.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni