MSIWATOZE KODI YA MAJENGO WAZEE WA MIAKA 60

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amewataka maafisa wa Mamlaka ya Kodi ya Mapato nchini (TRA) wakusanye kodi za majengo kwa kuzingatia sheria na wasitoze kodi ya majengo wazee wenye umri zaidi ya miaka 60.

"TRA ijipange kukusanya kodi za majengo kuanzia Julai Mosi 2017. Katika kutekeleza jukumu hilo, zingatieni sheria. Tusisikie mnawadai kodi ya majengo wazee wenye umri zaidi ya miaka 60 kwa majengo wanayotumia kama makazi yao," amesema.

Ametoa agizo hilo leo (Alhamisi, Juni 22, 2017) wakati akizungumza na wananchi na viongozi wa wilaya ya Chato waliohudhuria uzinduzi wa jengo la TRA, wilayani humo, mkoani Geita.

Waziri Mkuu amewataka maafisa hao wakusanye kodi ya majengo kwenye maeneo ya mjini na siyo vijijini kwani kodi hiyo haiwahusu. "Msiende vijijini. Nyumba za nyasi au za tembe hazihusiki. Tembeleeni nyumba za mijini. Piteni kwenye mitaa, muainishe aina zote za nyumba zinazostahili kulipiwa kodi. Mkishafanya sensa, wekeni utaratibu wa kuwawezesha wananchi kulipia kodi hizo," amesema huku akishangiliwa.

Pia amewataka wananchi wanaonunua bidhaa wadai risiti lakini wahakikishe wanapewa risiti yenye kiwango halisi walicholipia. "Ukipewa risiti uiangalie kama ina kiwango halisi cha fedha uliyotoa. Kuna watu wachache wasio waaminifu wanaamua kukupa risiti lakini imeandikwa bei ndogo kuliko ile uliyolipia, ukitoa laki moja anakuparisiti ya sh 10,000."

Mapema, akitoa taarifa ya ujenzi wa jengo hilo la ghorofa moja, Kamishna Mkuu wa TRA, Bw. Charles Kicheere alisema ujenzi huo ulianza Julai 12, mwaka jana na ulikamilika Juni 12, mwaka huu.

"Ujenzi wa jengo hili umegharimu sh. bilioni 1.4 na ulichochewa na ongezeko kubwa la idadi ya walipakodi wa Chato kutoka watu 150 mwaka 2010/2011 hadi kufikia watu 600 mwaka 2016/2017", alisema.

Pia alisema wamejenga ofisi hizo ili kuwapunguzia umbali wafanyabiashara wa wilaya hiyo ambao walilazimika kwenda Geita mjini kupata huduma za TRA ambako ni umbali wa zaidi km.120.

Alisema hivi karibuni watakamilisha ukarabati wa ofisi za mikoa ya Mara, Iringa, ikiwemo kujenga ofisi kwenye mikoa mipya ya Simiyu, Katavi, Njombe na Manyara. "Pia tutajenga ofisi kwenye mkoa mpya wa kikodi wa Kahama," alisema.

Alizitaja wilaya ambazo ziko mbioni kupatiwa ofisi zake kuwa ni Kondoa, Longido, Bunda na Arumeru.

Alisema katika mwaka ujao wa fedha, TRA imelenga kukusanya sh. trilioni 17.106 na watahakikisha wanafikia lengo hilo.

IMETOLEWA NA:

OFISI YA WAZIRI MKUU, 
ALHAMISI, JUNI 22, 2017.

DTB BENKI KUPANUA WIGO WA HUDUMA ZAO MKOANI TANGA


 Mkuu wa Mkoa wa Tanga,Martine Shigella akizungumza wakati wa futari iliyoandaliwa na Benki ya DTB kwa ajili ya wateja wao mkoani Tanga iliyofanyika kwenye hotel ya Tanga Beach Resort,kulia ni Shehe wa Mkoa wa Tanga,Juma Luwuchu na kushoto ni Meneja wa Benki ya DTB Mkoani Tanga,Athumani Juhudi
MKUU wa wilaya ya Tanga,Thobias mwilapwa akizungumza wakati wa futari hiyo
          Shehe wa Mkoa wa Tanga,Juma Luwuchu akitoa neno kwenye futari hiyo
 Meneja wa Benki ya Diamond Trust Bank Mkoani Tanga (DTB) Athumani Juhudi akizungumza na waandishi wa habari
                                                                                                          Wageni waalikwa
Mkurugenzi wa Jiji la Tanga,Daudi Mayeji kushoto akisalimiana na Aliyekuwa Meya wa Jiji la Tanga,Alhaj Kassim Kisauji wakati wa hafla ya futari hiyo
                                                       sehemu ya wageni waalikwa wakipata futari

BENKI ya Diamond Trust(DTB) Tawi la Tanga wanakusudia kupanua wigo wa huduma zao kwa wateja kwa kukarabati na kuongeza namba ya wahudumu ikiwa ni mkakakti wa ujio wa fursa mbalimbali mkoani hapa ukiwemo mradi mkubwa wa bomba la mafuta kutoka hoima nchini Uganda hadi Bandari ya Tanga.

Hayo yalibainishwa juzi na Meneja wa Benki ya Diamond Trust Bank Mkoani Tanga (DTB) Athumani Juhudi wakati futari iliyoandaliwa na Benki hiyo kwa wateja wao wa mkoa wa Tanga iliyofanyika kwenye ukumbi wa Tanga Beach Resort mjini hapa na kuhu dhuiwa na viongozi mbalimbali wakiwemo wakuu wa wilaya za Handeni na Tanga.

Alisema wao wanakusudia kufanya hivyo ili kuweza kuendana na wigo mpana wa ukuaji wa uchumi kwa mkoa wa Tanga ambao unatarajiwa kufanyika kutokana na mradi huo mkubwa .

“Benki yetu ipo kwenye nafasi ya tano kati ya mabenki zenye amana kubwa za wateja hivyo tumeona kuwaandalia futari hiyo ni namna bora ya kuwashukuru wao kwa kuwasapoti”Alisema.

“Unajua wateja wetu wamekuwa wakitusapoti hivyo ndio maana tumeona vizuri kuwaandalia futari lakini pia niwaambie kuwa wanaweza kutuma na kusafirisha fedha kwa haraka kutoka nje ya nchi na ndani ya nchi”Alisema

Awali akizungumza katika hafla hiyo,Mkuu wa Mkoa wa Tanga,Martine Shigella aliwataka wakazi wa mkoa huu kuendelea kumuombea Rais John Magufuli aweze kuendelea kupigania haki za watanzania wanyonge ambazo zimekuwa zikipotea.

Alisema kuwa kiongozi huyo mkuu wa nchi amekuwa akifanya mambo makubwa ya kuhakikisha watanzania wanapata maendeleo haraka na kukuza uchumi ambao utatufikisha kwenye mafanikio.

“Ndugu zangu waislamu tuendelee kuombea nchi yetu na Rais wetu ili yeye na viongozi wote waendelee kutenda yaliyomema na yanayompendeza mwenyezi mungu”Alisema RC Shigella.

“Lakini pia niendelee kuwashukuru kwa kuendelea kudumisha amani na mshikamano kwa mkoa huu kwa kipindi cha tokea mwezi ulipoanza mpaka sasa hivyo muendelee kuwa na upendo kwa watu wote.

Awali akizungumza katika futari hiyo,Shehe wa Mkoa wa Tanga, Juma Luwuchu aliwataka waislamu mkoano hapa kuendelea mshikamano waliokuwa nao kwenye kipindi cha mwezi mtukufu wa ramadhani kwa kuendelea kutenda yaliyo mema.

“Tuendelee kushikamana tupendane lakini kubwa zaidi tuhakikisha tunazingati kufanya ibada mara kwa mara na sio kipindi cha mwezi huutu hata baada ya kumalizika kwake “Alisema.
 


                                      Habari kwa Hisani ya Blog ya Kijamii ya Tanga Raha

RAIS DKT. MAGUFULI AFUNGUA BARABARA YA BAGAMOYO-- MSATA KM 64 PIA AWEKA JIWE LA MSINGI KIWANDA CHA MATUNDA CHA SAYONA CHALINZE MKOANI PWANI


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akikata utepe pamoja Mama Salma Kikwete (Mb), Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu Profesa Norman Sigala, Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa, kuashiria ufunguzi wa Barabara ya Bagamoyo-Makofia Msata yenye urefu wa kilometa 64 katika eneo la Daraja la Ruvu chini, Bagamoyo mkoani Pwani. Wengine katika picha ni Mkuu wa Mkoa wa Pwani Eng. Evarist Ndikilo, Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi Eng. Joseph Nyamhanga, Mbunge wa Chalinze Ridhiwan Kikwete , Katibu wa Itikadi na Uenezi ya CCM Hamphrey Polepole pamoja na viongozi wengine wa Serikali.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa pamoja na viongozi wengine wa Kiserikali na Wabunge, akivuta kitambaa kuashiria jiwe la ufunguzi wa Barabara ya Bagamoyo-Makofia Msata yenye urefu wa kilometa 64 katika eneo la Daraja la Ruvu chini, Bagamoyo mkoani Pwani.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimpongeza Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa mara baada ya kuweka jiwe la ufunguzi wa Barabara ya Bagamoyo-Makofia Msata yenye urefu wa kilometa 64 katika eneo la Daraja la Ruvu chini, Bagamoyo mkoani Pwani.
Sehemu ya barabara ya Bagamoyo-Makofia –Msata kama inavyoonekana pichani.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha ya pamoja na Wafanyakazi wa TANROADS mkoa wa Pwani na Dar es Salaam mara baada ya kufungua barabara ya Bagamoyo-Makofia Msata yenye urefu wa kilometa 64. Wengine katika picha ni Mkuu wa Mkoa wa Pwani Eng. Evarist Ndikilo, Mama Salama Kikwete, Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu Profesa Norman Sigala, Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa Katibu wa Itikadi na Uenezi ya CCM Hamphrey Polepole pamoja na viongozi wengine wa Serikali.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza jambo na Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa kabla ya kufungua Barabara ya Bagamoyo-Makofia Msata yenye urefu wa kilometa 64 katika eneo la Daraja la Ruvu chini, Bagamoyo mkoani Pwani
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza kabla ya kufungua Barabara ya Bagamoyo-Makofia Msata yenye urefu wa kilometa 64 katika eneo la Daraja la Ruvu chini, Bagamoyo mkoani Pwani.
Mtendaji Mkuu wa TANROADS Eng. Patrick Mfugale akielezea hatua za ujenzi wa Madaraja katika barabara ya Bagamoyo-Msata huku Rais Dkt. Magufuli akimsikiliza.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akikagua kiwanda cha Viuadudu cha Kibaha mkoani Pwani.
Mbunge wa Bagamoyo Dkt. Shukuru Kawambwa akisalimia kabla ya ufunguzi wa Barabara ya Bagamoyo-Makofia Msata yenye urefu wa kilometa 64 katika eneo la Daraja la Ruvu chini, Bagamoyo mkoani Pwani
Mtendaji Mkuu wa Wakala wa TANROADS Eng. Patrick Mfugale akizungumza kabla ya ufunguzi wa Barabara ya Bagamoyo-Makofia Msata yenye urefu wa kilometa 64 katika eneo la Daraja la Ruvu chini, Bagamoyo mkoani Pwani.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Waziri wa Ujenzi Profesa Makame Mbarawa pamoja na Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu Prof. Norman Sigala wakati wimbo wa Taifa ukipigwa kabla ya ufunguzi wa barabara hiyo ya Bagamoyo-Msata.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza baada ya kufungua kiwanda cha Matunda cha Sayona Fruits kilichopo Mboga Chalinze mkoani Pwani.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akifungua kiwanda hicho cha Matunda cha Sayona Fruits kilichopo Mboga Chalinze mkoani Pwani.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na wakazi wa Kiwangwa wakati akielekea kufungua barabara ya bagamoyo-Msata mkoani Pwani. PICHA NA IKULU

FANYA YAFUATAYO KUNOGESHA SIKUKUU YA EID-AL-FITR


Ni siku chache zimebakia kabla ya waumini wa dini ya kiislamu nchini na duniani kote kumaliza mfungo wa mwezi mtukufu wa Ramadhan kwa kusherehekea sikukuu ya Eid al-Fitr. Zipo namna tofauti za kusherehekea sikukuu hii kulingana na sehemu watu walipo. 
Jumia Travel ingependa kukushirikisha mambo yafuatayo ambayo yanaweza kuifanya sikukuu hii kuwa ya tofauti na kipekee tofauti na unavyosherehekea kila mwaka. Fanya maandalizi pamoja na familia. Katika kuhakikisha kwamba kila mtu anafurahia sikukuu basi ni vema ukawashirikisha kwenye maandalizi yake. 
 
Kama baba au mama wa familia na una watoto au ndugu unaishi nao litakuwa ni jambo zuri kama mtafanya hata kikao kidogo na kujadili. Kwa mfano, shughuli zote zitakazofanyika kipindi cha sikukuu, chakula kitakachopikwa, vinywaji, zawadi, wapi kwa kusherehekea, wageni gani wa kuwaalika, kupamba nyumba nakadhalika. Hii itasaidia siku hiyo ikifika kila mtu anafurahia na sio kufanya mambo ambayo yatakufurahisha wewe tu kuwaacha baadhi ya wengine kunung’unika.
 
Sherehekea pamoja na familia na majirani. Mara nyingi sikukuu hupendeza pale zinaposherehekewa kwa pamoja na ndugu na jamaa. Haijalishi familia uliyonayo ina ukubwa gani, kujumuika kwa pamoja kunaleta furaha na muunganiko zaidi miongoni mwa watu. Pia, hata kama una familia ndogo ni vema ukawashirikisha majirani zako. Unaweza ukapika chakula cha kutosha na ukaamua kuwaalika au kuwagawia lengo ni kuifanya iwe na shamrashamra zaidi. Sherekea pamoja na watu wenye mahitaji maalum. Sio kila mtu huwa anapata fursa au kuwa na uwezo wa kusherehekea sikukuu. Na kwa sababu sikukuu ya Eid al-Fitr husherehekewa kwa siku mbili mpaka tatu (kwa sehemu zingine), unaweza ukapanga kwamba sikukuu ya moja au mbili ukasherehekea na familia yako na nyingine ukajumuika pamoja na watu wenye mahitaji maalumu kama vile watoto wa mitaani, watoto wa mitaani, wagonjwa mahospitalini, wazee, wafungwa na wengineo. 
Wasimulie watoto kuhusu maisha ya Mtume na namna waislamu wa wakati walivyokuwa wakisherehekea sikukuu ya Eid-al-Fitr. Sio siku zote watoto wakishamaliza kupata chakula cha pamoja na familia wakaenda kutembea. 

Unaweza kuitumia siku hiyo kwa muda mchache tu ukawakusanya watoto na kuwasomea hadithi za Mtume Mohammad na namna waislamu wa kipindi hiko walikuwa wanasherehekea vipi sikukuu hii. Hii itawafanya si tu kufurahia kwa kuwaongezea maarifa lakini pia kuelewa ni nini maana zaidi ya siku hii. Safiri pamoja na familia. Unaweza ukaamua kusherehekea sikukuu hii kwa kusafiri mahali tofauti na nyumbani. Mnaweza kutumia gari binafsi kama usafiri, mkawa mnapumzika kwenye vituo kadhaa kwa ajili ya chakula na kuswali mpaka mkafika mahali muendapo. 
Toa zawadi kwa ndugu, jamaa na marafiki. Kipindi cha Ramadhan mbali tu na kuwa ni kipindi cha kufanya toba na kumuomba Mwenyezi Mungu kukupunguzia dhambi zako lakini pia kutoa zawadi kunaweza kuwa ni njia mojawapo ya kukuongezea thawabu. Kutoa zawadi ni jambo jema kumfanyia mtu hususani unapolifanya kwa moyo mkunjufu. Basi kama utakuwa na uwezo unaweza kununua zawadi kadhaa na kuwapatia ndugu na majirani zako. 
Badili muonekano wa nyumba yako. Itapendeza kama siku ya sikukuu mtaisherehekea kwenye nyumba yenye muonekano tofauti. Unaweza kufanya hivi kwa kushirikiana na familia yako ili kupata mwonekano utakaovutia. Mambo yanayoweza kubadili mwonekano wa zamani ni kama vile kupaka rangi mpya, kubadili samani za ndani, kununua mapambo, kufanya usafi au hata mpangilio wa vitu ndani ya nyumba. 
Valia mavazi nadhifu. Tumezoea kwamba linapokuja suala la kuvaa nguo mpya siku za sikukuu huwa ni watoto pekee wanaopenda kufanya hivyo. Kwenye familia nyingi imekuwa ni kawaida wazazi kuweka kipaumbele kwa kuwanunulia watoto nguo mpya. 

Kutokana na desturi hiyo kuzoeleka miongoni mwa watu wengi, imewafanya watu wazima kupuuzia kuvaa nguo mpya kipindi cha sikukuu. Hiyo ni dhana na mawazo ya watu tu na wala isikufanye ujisikie vibaya kuvaa nguo mpya siku ya sikukuu. Unastahili kuutendea vema mwili wako kwa kuuvika na mavazi mapya na nadhifu siku hiyo, kama una uwezo lakini.Dhumuni la kukupatia dondoo hizi ni kuifanya sikukuu hiyo iwe na upekee tofauti na unavyosherehekea kila mwaka. Jaribu kufanya baadhi ya mambo hayo na utagundua utofauti mkubwa. Sio lazima ufanye yote yaliyoorodheshwa kwenye makala haya, machache tu yanatosha. 

Tofauti na hapo, Jumia Travel ingependa kukutakia maandalizi na mapumziko mema ya sikukuu ya Eid al-Fitr!

LIVERPOOL YAMNG'OA WINGA MOHAMED SALAH KUTOKA ROMA


Liverpool imekamilisha usajili wa paundi milioni 34 na kunasa saini ya mchezaji wa Roma aliyewahi kuichezea Chelsea winga Mohamed Salah.

Mchezaji huyo raia wa Misri mwenye umri wa miaka, 25, aliyemwaga wino kuitumikia Liverpool kwa mkataba wa miaka mitano amekuwa akiwindwa mno na kocha Jurgen Klopp.

Salah alikaribia kutua Liverpool akitokea timu ya Basle mwaka 2014 kabla ya kuamua kwenda Chelsea.
                          Mohamed Salah akionyesha jezi yake aliyokabidhiwa na Liverpool 

KIJIJI CHA SHUJAAZ CHAFUNGULIWA KATIKA MASHINDANO YA EAC 2017 MJINI MOSHI.


Afisa Masoko wa kamuni ya YARA Ltd ,Linda Byaba akitoa elimu kuhusu kilimo bora na chenye tija na jinsi ya kuongeza thamani ya mazao mbalimbali ikiwa ni pamoja na matumizi ya Mbolea kwa Mwakilishi wa taasisi ya Wel tel Story ,Alan Lucky.
Mwakilishi wa Taasisi ya Wel tel Story ,watayarishaji wa Mradi wa Shujaaz,Alan Lucky akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani ) kuhusu kufunguliwa kwa kijiji cha Shujaaz katika Mashindano ya vijana ya Afrika Mashariki maarufu kama East Africa Cup 2017 yanayofanyika katika shule ya Sekondari Moshi Ufundi .
Baadhi ya Wageni wakijiandikisha kabla ya kuingia katika kijiji hicho ambako kumekuwa kukitolewa mafunzo mbalimbali hasa ya Kilimo .
Mratibu wa Tafiti wa Mradi wa Shujaaz,Winnie Nyato akitoa tiketi kwa mmoja wa watoto waliotembelea kijiji cha Shujaaz .
Mhitimu wa Chuo Kikuu cha Dodoma ,Mohamed Kombo anayejishughulisha na Kilimo cha matunda akizungumza na vijana waliofika katika kijiji cha Shujaaz kuona namna gani wanaweza kuhamasika na kuingia katika shghuli za Kilimo.

Mjasiliamali Khalfa Muslim akitoa elimu jinsi ya kutengeneza mchanganiko wa Matunda kwa vijana waliotembelea kijiji cha Shujaaz kilichopo katka viwanja vya Shule ya sekondari Moshi Ufundi yanapofanyika mashindano ya East Africa Cup 2017.
Mjasiliamali Holo Bukombe akionesha bidhaa mbalimbali ambazo amekuwa akiziweka katika vifungashio maalumu na kuongeza thamani ya bidhaa husika.
Muonekano wa kijiji cha Shujaaz kilichopo katika Shule ya Sekondari Moshi Ufundi ambako elimu mbalimbali hususani za Kilimo pamoja na michez kwa vijana imekuwa ikitolewa.
Baadhi ya watoto wakishindana michezo mbalimbali (Games) katika kijiji cha Shujaaz.
Vijana wengine wamepaa fursa ya kucheza mchezo wa mitupo ndani ya kijiji hicho.
Vijana wengine walipata nafasi ya kuonesha vipaji vyao hasa vya kuimba na kucheza na kuambulia zawadi kutoka Shujaaz.

Na Dixon Busagaga wa Glob ya Jami ,Kanda ya
 Kaskazini.

RAIS MAGUFULI ATOA MSAADA WA VITANDA,MAGODORO NA MASHUKA KATIKA HOSPITALI YA LEVOLOSI


Mbunge wa viti maalumu ccm Mkoa wa Arusha Catherine Magige akitoa nasaha mara tu baada ya kukabidhi msaada huo wa vitanda,magodoro na mashuka yaliyotolewa na Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania
Picha ikionyesha wa kwanza kulia Mbunge wa viti maalum(CCM)Catherine Magige akikabidhi kwa niaba ya Rais John Magufuli msaada wa magodoro 25,mashuka 25 pamoja na vitanda 25 katika kituo cha afya cha Levolosi ,ambapo msaada wa vitu hivi umetolewa na Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania ikiwa ni moja wapo ya ahadi zake alizozitoa katika kipindi cha kampeni ,katikati ni Mganga mkuu wa kituo cha Afya cha Levolosi Feksi Edward ,wa kwanza kushoto ni Mganga mkuu wa Halmashauri ya jiji la Arusha Saimoni Chacha (picha na Woinde Shizza,Arusha)
Katibu wa UWT mkoa wa Arusha Fatuma Hassan akiwasalimia wananchi wakati wa hafla hiyo
Mkuu wa wilaya ya Arusha Gabriel Fabian Daqarro akiongea na wananchi wa jiji la Arusha
Baadhi ya manesi na madaktari wa jiji la Arusha wakiwa wamelibeba moja ya godoro mara baada ya kukabidhiwa hii leo
   Mkurugenzi wa Jiji la Arusha Mh: Athuman Kihamia akitoa neno la shukrani kwa niaba ya jiji mara baada ya kupokea msaada huo na kuhadi kuvitunza vifaa hivyo walivyokabidhiwa
 Mbunge wa viti maalumu Catherine Magige akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wananchi wa jiji la Arusha mara baada ya kukabidhi vifaa hivyo

Baadhi ya madaktari na manesi wakiwa wanashuhudia makabidhiano ya msaada huo wa vitanda ,mashuka na magodoro (habari picha na Woinde Shizza,Arusha)
 Na Mahmoud Ahmad,Arusha
Wananchi wametakiwa kuwapiga vita na kutokubaliana na wale wote ambao wanapinga jitiada za maendeleo ambazo zinafanywa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwani jitihada hizo zina manufaa makubwa kwa wananchi.

Aidha kumekuwa na baadhi ya watu wamekuwa wakiziponda kazi ambazo anazifanya Rasi kitu ambacho sio kizuri kwani Rais amekuwa akijitaidi kufanya kazi vizuri ya kuwaletea maendeleo wananchi kama ilani ya chama cha mapinduzi inavyosema

Hayo yamesemwa leo jijini hapa na mbunge wa viti maalumu kupitia chama cha mapinduzi mkoa wa Arusha Catherine Magige wakati akikiabidhi kwa niaba ya Raisi vitanda 25 ,mashuka 25 na magodoro 25 viliyotolewa na Rais wa jamuhuri ya muungano wa Tanzania ikiwa ni moja ya utekelezaji wa ilani ya chama cha mapinduzi

Alisema k uwa kumekuwa na baadhi ya viongozi wamekuwa wakiponda kazi za Rais na kusema kuwa afanyikitu chochote

"Rais wetu anafanyakazi mtu anaesema afanyikazi kweli ni wakupuunzwa kabisa au naweza sema ana akili angalieni jinsi alivyozuia makontena ya madini,angalieni jinsi alivyowakamata waujumu uchumi wa Escrow na sasa ivi ameunda tume ya kwenda kuchunguza Tanzanite one mbali na apo ata leo ametambua umuimu wawananchi wa mkoa wa Arusha na ameamua kutoa msaada wa magodoro ,mashuka pamoja na vitanda "alisema Magige

Aidha alitoa wito kwa wananchi kuunga mkono kazi ziazofanywa na Rais ,pia alitumia muda huho kuwasihi madaktari kutunza vifaa ambavyo vinatolewa na serikali kwani vifaa hivyo vinanunuliwa kwa kodi za wananchi ,huku akisisitiza iwapo vitatunzwa vizuri vinaweza kukaa kwa muda mrefu na kuwahudumia wananchi wengi zaidi

Akitoa shukrani kwa vifaa hivyo mkurugenzi wa jiji la Arusha Mh: Athuman Kihamia aliishukuru serikali kwa kutoa misaada hii kwa jiji la Arusha na kuhaidi kuvitunza vifaa hivyo vilivyotolewa huku akiiomba serikali iendelee kuwapa misaada ya aina mbalimbali.

Msaada huu wa magodoro 25 ,mashuka 25 pamoja na vitanda 25 uliogaiwa leo katika hospitali ya Levolosi jijini Arusha umetolewa na Rais wa Jamuhuri ya muungano wa Tanzania ikiwani moja ya utekelezaji wa ilani ya chama cha mapinduzi