ESRF YAANDAA MKUTANO KUJADILI BIASHARA NA UWEKAZAJI KATI YA TANZANIA NA CHINA

 Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe Dkt. Philip Mpango akisoma hotuba kwa niaba ya Makamu wa Rais Mh. Samia Suluhu Hassan (hayupo pichani) wakati akifungua mkutano wa 6 wa mwaka wa ESRF unaozungumzia biashara na uwekezaji kati ya Tanzania na China uliofanyika jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Tafiti za Kiuchumi na Kijamii (ESRF), Dk. Tausi Kida akitoa neno la ukaribisho kwa washiriki wa mkutano wa 6 wa mwaka wa ESRF unaozungumzia biashara na uwekezaji kati ya Tanzania na China uliofanyika jijini Dar es Salaam. Mwenyekiti wa bodi ya ESRF, Philemon Luhanjo akizungumza machache kabla ya kumkaribisha mgeni rasmi kufungua mkutano wa 6 wa mwaka wa ESRF unaozungumzia biashara na uwekezaji kati ya Tanzania na China uliofanyika jijini Dar es Salaam. Mwakilishi wa Ubalozi wa China nchini Tanzania anayeshughulikia wa Masuala ya Uchumi na Biashara, Lin Zhiyong akizungumza kwa niaba ya balozi wa China wakati wa ufunguzi wa mkutano wa 6 wa mwaka wa ESRF unaozungumzia biashara na uwekezaji kati ya Tanzania na China uliofanyika jijini Dar es Salaam. Katibu Mkuu Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Profesa Adolf Mkenda akiwasilisha mada inayohusu namna watanzania wanavyoweza kunufaika na fursa za kibiashara na uwekezaji China wakati wa mkutano wa 6 wa mwaka wa ESRF unaozungumzia biashara na uwekezaji kati ya Tanzania na China uliofanyika jijini Dar es Salaam. Pichani juu na chini ni sehemu ya washiriki kutoka China na Tanzania waliohudhuria mkutano wa 6 wa mwaka wa ESRF unaozungumzia biashara na uwekezaji kati ya Tanzania na China uliofanyika jijini Dar es Salaam. Mwenyekiti ya Taasisi ya Utafiti wa Maendeleo China (CIDRN), Prof. Dr. Li Xiaoyun akitoa neno la ukaribisho kwa washiriki wa mkutano wa 6 wa mwaka wa ESRF unaozungumzia biashara na uwekezaji kati ya Tanzania na China uliofanyika jijini Dar es Salaam. Balozi wa Tanzania nchini China, Mh. Mbelwa Kairuki akizungumzia namna ambavyo watanzania wanaweza wakafaidika na fursa za biashara na uwekezaji nchini China wakati wa mkutano wa 6 wa mwaka wa ESRF unaozungumzia biashara na uwekezaji kati ya Tanzania na China uliofanyika jijini Dar es Salaam. Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Anthony Mtaka akiwasilisha mada inayohusu mahusiano ya kibiashara ya uwekezaji kati ya Tanzania na China kwa mtazamo wa Serikali za Mitaa wakati wa mkutano wa 6 wa mwaka wa ESRF unaozungumzia biashara na uwekezaji kati ya Tanzania na China uliofanyika jijini Dar es Salaam. Kutoka kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Utafiti wa Uchumi na Jamii (ESRF), Dk. Tausi Kida, Balozi wa Tanzania nchini China, Mh. Mbelwa Kairuki, Waziri Mkuu mstaafu, Dkt. Salim Ahmed Salim, Mwenyekiti wa bodi ya ESRF, Philemon Luhanjo, Mwenyekiti na Afisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni za Infotech Investment, Ali Mfuruki wakifuatilia mada mbalimbali zilizokuwa zikiwasilisha wakati wa mkutano wa 6 wa mwaka wa ESRF unaozungumzia biashara na uwekezaji kati ya Tanzania na China uliofanyika jijini Dar es Salaam. Mkutano ukiendelea. Balozi wa Tanzania nchini China, Mh. Mbelwa Kairuki pamoja na Waziri Mkuu mstaafu, Dkt. Salim Ahmed Salim wakifuatilia mada mbalimbali zilizokua zikiwasilishwa katika mkutano wa 6 wa mwaka wa ESRF unaozungumzia biashara na uwekezaji kati ya Tanzania na China uliofanyika jijini Dar es Salaam. Profesa Humphrey Moshi kutoka idara ya Uchumi katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam akiwasilisha mada inayohusu uhusiano wa China na Tanzania katika masuala ya uwekezaji na biashara wakati wa mkutano wa 6 wa mwaka wa ESRF unaozungumzia biashara na uwekezaji kati ya Tanzania na China uliofanyika jijini Dar es Salaam. Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka Maalum ya Uwekezaji (EPZA), Kanali Mstaafu Joseph Simbakalia akichangia maoni wakati wa mkutano wa 6 wa mwaka wa ESRF unaozungumzia biashara na uwekezaji kati ya Tanzania na China uliofanyika jijini Dar es Salaam. Mwanachama wa Chama cha Wanafunzi walisomea China (CAAT), Linas Kahisha akielezea uzoefu wake katika fursa za kibiashara nchini humo katika mkutano wa 6 wa mwaka wa ESRF unaozungumzia biashara na uwekezaji kati ya Tanzania na China uliofanyika jijini Dar es Salaam. Pichani juu na chini ni washiriki kutoka Tanzania na Chini waliohudhuria mkutano wa 6 wa mwaka wa ESRF unaozungumzia biashara na uwekezaji kati ya Tanzania na China uliofanyika jijini Dar es Salaam Mgeni rasmi Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe Dkt. Philip Mpango, Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Utafiti wa Uchumi na Jamii (ESRF), Dk. Tausi Kida na Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Anthony Mtaka wakiwa katika picha ya pamoja na wanafunzi watafiiti kutoka nchini China. Mkuu wa Idara ya Utafiti na Machapisho wa ESRF, Prof. Fortunata Makene (kushoto) katika picha ya kumbukumbu na Mkuu wa Idara ya Maarifa na Ubunifu wa ESRF, Bi. Margareth Nzuki (kulia) mara baada ya ufunguzi rasmi wa mkutano wa 6 wa mwaka wa ESRF unaozungumzia biashara na uwekezaji 
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Utafiti wa Uchumi na Jamii (ESRF), Dk. Tausi Kida (katikati), Mkuu wa Idara ya Maarifa na Ubunifu wa ESRF, Bi. Margareth Nzuki na Mwenyekiti ya Taasisi ya Utafiti wa Maendeleo China (CIDRN), Prof. Dr. Li Xiaoyun katika picha ya kumbukumbu. Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Anthony Mtaka (katikati) katika picha ya pamoja na washiriki kutoka TPSF na ESRF na Mshereshaji wa mkutano huo Eng. George Mulamula (kushoto). Baadhi ya washiriki kutoka China wakichukua baadhi ya makabrasha yenye taarifa mbalimbali zilizoandaliwa na ESRF wakati wa mkutano wa 6 wa mwaka wa ESRF unaozungumzia biashara na uwekezaji kati ya Tanzania na China uliofanyika jijini Dar es Salaam. Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe Dkt. Philip Mpango akisalimiana na Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Utafiti wa Uchumi na Jamii (ESRF), Dk. Tausi Kida alipowasili katika ufunguzi wa mkutano wa 6 wa mwaka wa ESRF unaozungumzia biashara na uwekezaji kati ya Tanzania na China uliofanyika jijini Dar es Salaam. Mgeni rasmi Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe Dkt. Philip Mpango (katikati) akiongozana na Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Utafiti wa Uchumi na Jamii (ESRF), Dk. Tausi Kida (kushoto) na Mwenyekiti wa bodi ya ESRF, Philemon Luhanjo baada ya kuwasili katika mkutano wa 6 wa mwaka wa ESRF unaozungumzia biashara na uwekezaji kati ya Tanzania na China. 
Mgeni rasmi Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe Dkt. Philip Mpango katika picha ya kumbukumbu na Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Utafiti wa Uchumi na Jamii (ESRF), Dk. Tausi Kida mara baada ya kufungua mkutano wa 6 wa mwaka wa ESRF unaozungumzia biashara na uwekezaji kati ya Tanzania na China uliofanyika jijini Dar es Salaam. 

WAZIRI wa Fedha na Mipango, Mhe Dkt. Philip Mpango ametaka kuwapo na uratibu wenye maslahi mapana katika biashara na uwekezaji kati ya Tanzania na China.
 

Alisema hayo wakati akifungua mkutano wa 6 wa mwaka wa ESRF unaozungumzia biashara na uwekezaji kati ya Tanzania na China. Alisema mahusiano yaliyopo kati ya Tanzania na China ambayo ni ya kihistoria yasitumike vibaya bali yanahitaji kuratibiwa kiuangalifu kwa maslahi ya pande zote mbili.
 

Aliwataka washiriki wa mkutano huo wa mwaka kujadili kwa makini namna ya kuratibu vizuri vitega uchumi na biashara kwa manufaa ya nchi zote mbili.
Alielezea kufurahishwa kuwapo na mada mbalimbali zinaozungumzia biashara na uwekezaji kati ya Tanzania na China na kusema mada hizo zitumike vyema kuweka misingi mizuri yenye manufaa kwa pande zote mbili. 


Aidha aliipongeza ESRF kwa kuona haja ya kuwapo kwa mazungumzo ya aina hiyo na kusema kupitia tafiti mbalimbali taifa hili litaenda mbele katika kujenga uchumi wa viwanda.
 

Mkutano huo unaohusisha washiriki mbalimbali wa ngazi za juu wa biashara na uwekezaji kati ya Tanzania na China umeitwa kama sehemu ya mchango wa ESRF katika ujenzi wa uchumi wa viwanda wa Tanzania. “Sisi serikalini tunaridhishwa na juhudi zinazofanywa na taasisi za kitafiti kama hii zenye lengo la kusaidia juhudi za serikali za kuhudumia watu wake na kuongeza ustawi” alisema Mpango.
 

Mkutano huo ambao unazungumzia mahusiano ya kibiashara na uwekezaji umeelezwa na Mh. Dk Mpango kuwa moja ya mikutano inayotoa fursa za kuangalia uwekezaji wenye tija unaozingatia maslahi mapana ya mataifa husika.
 

Alisema Tanzania na China zina uhusiano mzuri wa kihistoria na hadi sasa na kwamba kinachostahili ni kuoanisha uhusiano huo na kuuweka katika hali bora zaidi za kunufaisha pande zote mbili.
 

Baadhi ya miradi mikubwa ambayo Tanzania imesaidiwa na China ni pamoja na ujenzi wa Reli ya Tanzania na Zambia (TAZARA) na kiwanda cha Urafiki; kuanzishwa kwa shamba la mpunga la Mbarali; kiwanda cha sukari cha Mahonda na mgodi wa mawe wa Kiwira.
 

Kwa sasa China ni moja ya taifa lililo na uwekezaji mkubwa nchini Tanzania pia ikifanya shughuli nyingi za ujenzi zenye gharama kubwa kama daraja la Kigamboni na barabara.
 

Naye Mwenyekiti wa bodi ya ESRF, Philemon Luhanjo, akimkaribisha Mheshimiwa Waziri Mpango alisema kwamba alisema kwamba mkutano huo umeandaliwa kwa pamoja kati ya ESRF na Chuo kikuu cha Kilimo cha China. 

Alisema mkutano huo umewaleta pamoja wanazuoni wa Kichina na Kitanzania kuangalia mahusiano yaliyopo na kutengeneza mustakabli bora wa namna ya kushirikiana.
 

Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Tafiti za Kiuchumi na Kijamii (ESRF), Dk. Tausi Kida amesema kwamba mkutano huo ni sehemu ya juhudi za kusaidia serikali kwa njia ya utafiti ambapo majibu yanatumiwa kutengeneza sera au majibu ya changamoto mbalimbali. Mkutano huo ulifungwa na Waziri Mkuu mstaafu, Mh. Dkt. Salim Ahmed Salim.

BALOZI SEIF AKITAKA CHAMA CHA SKAUTI NCHINI KUWAELIMISHA VIJANA ILI WAJIKOMBOE KIUCHUMI

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi Kushoto akivishwa Skafu na Kijana Omar Amour Said wa Skauti nje ya Ukumbi wa Baraza la Wawakilishi wa zamani Kikwajuni Mjini Zanzibar kabla ya kuzungumza na Vijana wa Chama cha Sakauti Zanzibar. Kati kati yao ni Raius wa Chama cha Skauti Zanzibar ambae pia ni Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar Mh. Riziki Pembe Juma.
Balozi Seif akiambatana na Rais wa Skauti Zanzibar Mh. Riziki Pembe Juma wakielekea ndani ya Ukumbi wa Mkutano kuzungumza na Vijana wa Skautio Zanzibar wanaotarajiwa kuondoka Zanzibar kuelekea Mkoani Dodoma katika maadhimisho ya Miaka 100 ya Skauti Tanzania.
Balozi Seif akimpongeza Kijana Kassim Yussuf Msoma Mashairi ghibu baada ya kughani kwenye Mkutano wa Skauti Zanzibar uliofanyika kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Baraza la Wawakilishi wa Zamani Kikwajuni.
Baadhi ya Skauti wa Zanzibar wakifuatilia Mkutano wa Chama hicho uliohutubiwa na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi uliokuwa wa matayarisho ya mwisho wa Vijana wake kujiandaa kuelekea Dodoma katika Tamasha la Miaka 100 ya Skauti Tanzania.
Baadhi ya Makatibu wa Skauti wa Mikoa ya Unguja wakifuatilia Hotuba ya Balozi Seif ambaye hayuko pichani hapo katika Ukumbi wa zamia wa Baraza la Wawakilishi Kikwajuni Mjini Zanzibar.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif akiwahutubia VBijana wa Chama cha Skauti Zanzibar wanaojiandaa kuelekea Dodoma katika Tamasha la Miaka 100 ya Skauti Tanzania.


                                                                                                      Picha na – OMPR – ZNZ.
 

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi amesema wakati umefika kwa Chama cha Skauti Nchini kuongeza nguvu za kuwaelimisha Vijana wenzao hasa walioko Vijijini ili wajikomboe kupenda kujishughulisha na kazi au miradi ya ujasiri amali.

Alisema Vijana wengi wamekuwa na tabia ya kujihusisha na vigenge vya kihuni mitaani vinavyopelekea kujiingiza katika matumizi ya dawa za kulevya wizi pamoja na vitendo vya kudhalilisha watoto wanawake na watu wenye mahitaji Maalum.

Balozi Seif Ali Iddi alitoa Kauli hiyo wakati akizungumza na Vijana wa Chama cha Skauti Zanzibar wanaojiandaa kuelekea Mkoani Dodoma kushiriki Tamasha la Wiki Moja la Maadhimisho ya Miaka 100 ya Skauti Tanzania hapo katika Ukumbi wa zamani wa Baraza la Wawakilishi Kikwajuni Mjini Zanzibar.

Alisema zipo fursa nyingi za ajira zinazopatikana katika Sekta ya Utalii ambazo Vijana endapo wataamua kuzichangamkia zinaweza zikawapatia kipato kwa kutumia soko la bidhaa zinazotokana na kilimo cha mboga mboga na mazao ya Baharini.



Balozi alifahamisha kwamba Uskauti kwa vile hauna mafungamano ya itikadi ya Kisiasa wala Dini unalengo la kuwaunganisha Vijana katika harakati zao za kimaisha kupitia misingi ya kujenga Utaifa wao.

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar alisisitiza umuhimu wa vijana wa Skauti kufundishwa mbinu na mafunzo ya kuogelea na kuzamia kutokana na majukumu yao yaliyowazuunguka ya kuwa wao ni miongoni mwa Taasisi zinazotoa huduma wakati yanapotokea maafa au majanga.

Balozi Seif alielezea kuridhika kwake na Kanuni 10 za Skauti zinazoelekeza uzalendo unaojenga Taifa lenye Wananchi wanaopendana na kuwa na nguvu za kukabiliana na changamoto zinazowazunguuka katika misingi ya nidhamu na uwajibikaji.

Mapema Kamishna Mkuu Msaidizi wa Chama cha Skauti Zanzibar Maalim Suleiman Takadir alisema Skauti iliasisiwa Zanzibar mnamo mwaka 1912 na Mwaka 1917 ikaanzishwa upande wa Tanzania na kufifia katika miaka ya 60.

Maalim Takadir alisema Chama hicho kilianzishwa tena Mwaka 1992 chini ya Rais wa Awamu ya Tano Dr. Salmin Amour ili kufufua ari ya kuwajenga Vijana katika uzalendo.

Alisema Chama cha Skauti kimejiwekea Kanuni Kumi zinazoiongoza Taasisi hiyo ikiwa ni pamoja na kuaminika, adabu, huruma, utiifu, uchangamfu, uadilifu pamoja na usafi wa vitendo.

Akizungumzia changamoto zinazokikabili chama hicho cha Skauti Zanzibar Kamishna Mkuu Msaidizi huyo wa Skauti Zanzibar alizitaja kuwa ni pamoja na ukosefu wa Ofisi ya kufanyia kazi pamoja na uwanja wa kufanyia mazoezi kwa Vijana wake.

Maalim Takadir aliwaomba Wakuu wa Mikoa na Wilaya Nchini kufanya kazi kwa karibu na Makamishna wa Skauti wa Mikoa ili kufanikisha malezi ya vijana katika maeneo hayo.

Akitoa salamu Rais wa Chama cha Skauti Zanzibar ambae pia ni Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar Mh. Riziki Pembe Juma amemshukuru Rais Mstaafu wa Zanzibar wa Awamu ya Tano Dr. Salmin Amour kwa busara zake za kuifufua tena Skauti Zanzibar.

Waziri Riziki alisema ule ukakamavu unaoonyeshwa na Vijana Skauti katika matendo yao ya kila siku yamewawezesha kuwa na nguvu za mawazo na kiakili zinazowasababishia kufanya vizuri katika masomo na mitihani yao.

Alisema Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar ina wajibu wa kutoa Elimu na malezi kwa Watoto wote bila ya ubaguzi ambao ni wajibu wa lazima na sio wa kupendelea.

Timu ya Vijana hao walioteuliwa 40 wa Skauti Zanzibar wanaondoka Visiwani kesho kuelekea Mkoani Dodoma kushiriki Wiki ya Tamasha la kuadhimisha Miaka 100 ya Skauti Tanzania.

Othm,an Khamis Ame

Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar
19/7/2017

WAZIRI MKUU KASSIM MAJALIWA AONGOZA MAMIA YA WAOMBOLEZAJI KATIKA MAZIKO YA LINAH GEORGE MWAKYEMBE WILAYANI KYELA, MBEYA

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa na mkewe wakiwa wamebeba shada la maua tayari kuliweka katika kaburi la mke wa Waziri wa Habari, Utamaduni, sanaa na Michezo, Dkt. Harrison Mwakyembe, marehemu Linah George Mwakyembe, katika mazishi yaliyofanyika makaburi ya familia katika kijiji cha Ikolo wilayani Kyela mkoani Mbeya hii leo
Mkuu wa mkoa wa Mbeya, Mhe. Amos Makalla akiweka shada la maua katika kaburi la mke wa Waziri wa Habari, Utamaduni, sanaa na Michezo, Dkt. Harrison Mwakyembe, marehemu Linah George Mwakyembe, katika mazishi yaliyofanyika makaburi ya familia katika kijiji cha Ikolo wilayani Kyela mkoani Mbeya hii leo
Waziri wa Habari, Utamaduni, sanaa na Michezo, Dkt. Harrison Mwakyembe akiweka shada la maua katika kaburi la marehemu mkewe, Linah George Mwakyembe.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa na mkewe wakiweka shada la maua katika kaburi la mke wa Waziri wa Habari, Utamaduni, sanaa na Michezo, Dkt. Harrison Mwakyembe, marehemu Linah George Mwakyembe, katika mazishi yaliyofanyika makaburi ya familia katika kijiji cha Ikolo wilayani Kyela mkoani Mbeya hii leo
Jeneza lenye mwili wa mke wa Waziri wa Habari, Utamaduni, sanaa na Michezo, Dkt. Harrison Mwakyembe, marehemu Linah George Mwakyembe likiandaliwa kushushwa kaburini
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa ( kulia ), Mkuu wa mkoa Mbeya, Mhe. Amos Makalla na mke wa Waziri Mkuu wakifuatilia shughuli za mazishi ya mke wa Waziri wa Habari, Utamaduni, sanaa na Michezo, Dkt. Harrison Mwakyembe, marehemu Linah George Mwakyembe, katika kijiji cha Ikolo wilayani Kyela mkoani Mbeya hii leo. Picha zote na Haroub Kabwe

Ukitaka Vya Chini Sharti Uiname..!


Image may contain: one or more people, people standing, child and outdoor
Tukuyu hapa, 2015.

Neno La Leo: " Enyi Walimu Watakatifu.."


Image may contain: 2 people, people sitting
Ndugu zangu,
Nayaandika haya nikiwa pia ni mwalimu kitaaluma.

CHUNGULIA FURSA BODA TO BODA

Kituo Kikuu cha Mabasi, Dodoma
Bw. Justin Kisoka, Mtumishi wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki ambaye amebobea katika masuala ya uchumi akitoa somo namna vijana wa Kitanzania watakavyoweza kuuza bidhaa zao ndani ya soko la Afrika Mashariki lenye nchi sita na idadi ya watu wanaofikia milioni 165. 
Mfanyabiashara akielezwa namna bidhaa zake ambazo amezibeba kichwani atakavyoweza kuziuza katika nchi za Afrika Mashariki na kupata faida kubwa.

Ujumbe wa kutaka vijana na Watanzania kwa ujumla wazinduke ili wanufaike na soko la Afrika Mashariki ulifikishwa kwa njia tofauti ikiwemo sanaa ya maigizo.

Baadhi ya watu waliojitokeza kupata mbinu za kufanya biashara ndani ya Jumuiya ya Afrika Mashariki. Hapa ilikuwa Kituo Kikuu cha Mabasi mjini Dodoma.


Gandhi Hall , Mwanza 

Bw. Justin Kisoka akiwa kwenye bustani ya Gandhi Hall mjini Mwanza akitoa somo namna Wanamwanza watakavyoweza kuuza Sato, Sangara na bidhaa nyingine katika soko la Afrika Mashariki.

Wanamwanza acheni woga, vukeni mipaka ya Tanzania kuuza bidhaa zenu, ni baadhi ya maneno aliyokuwa anayatumia Mchumi huyo katika kuwashajihisha vijana wachangamke kuvuka mipaka ya Tanzania kuuza bidhaa zao.

Dada somo limemkolea anapata maelezo zaidi kutoka kwa wataalamu wa Wizara ili shughuli ya kuvuka mipaka ianze mara moja.


Viwanja vya Furahisha, Mwanza
Bw. Abel Maganya, Mtaalamu wa Masuala ya Afrika Mashariki kutoka Wizara ya Mambo ya Nje akitoa somo kwenye viwanja vya  furahisha. 

Serikali za Nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki zinatimiza majukumu yake kwa kuweka mazingira mazuri ikiwemo sheria, kanuni na miundombimu ili wanajumuiya mfanye biashara katika nchi unayopenda bila bugdha. Msijifungie ndani vukeni mipaka kupeleka bidhaa mbalimbali.

Baadhi ya Wananchi waliojitokeza katika viwanja vya furahisha.

Mzee anasema somo limengia barabara hivyo na  uzee wangu nawahimiza wajukuu zangu kufanya biashara ya kuvuka mipaka. Anafikisha ujumbe wake kwa kushiriki kusakata dance linalohimiza biashara za kuvuka boda.