Mwanasheria Arthur Mbena kutoka Mamlaka ya usimamizi wa Bima Tanzania (TIRA) akiwa katika maonyesho ya 41 ya biashara Kimataifa sabasaba. sabasaba jijini Dar es salaam.Picha na Mhmoud Ahmad |
Bango la Mamlaka ya Usimamizi wa Bima nchini lenye maelezo namna ya kutambua bima kama ni halali au ni feki kama maelezo yanavyosomeka hapo |
Wa kwanza kushoto ni Mwanasheria
Arthur Mbena akiwana Paul Abdiel ambae ni Afisa Mchambuzi
(Bima)kutoka (TIRA)Makao makuu Dar es salaam wakiwa katika maonyesho
ya 41 ya biashara Kimataifa sabasaba. |
Mamlaka
ya usimamizi wa Bima nchini( TIRA)imetoa rai kwa wananchi kutumia
mfumo wa TIRA MIS ambao utamsaidia mteja kutambua bima za
vyombo vya moto zenye uhalali au feki kwa kutumia mfumo wa
kieletroniki.
Hayo
yamesemwa na mwanasheria Arthur Mbena ambapo amesema kuwa mtu yeyote
yule ambae atakamatwa na bima feki sheria itafuata mkondo wake,
ameainisha njia ambazo mtu anaweza kutambua bima yake kama ni
feki ama halali kwa kutumia simu ya mkononi( smart phone)kutumia
mtandao http/mis.tira.go.tz,google unadownlod tira
mis.
Aidha amesema kuwa kazi kubwa
ya Mamlaka ya Usimamizi wa Bima nchini ni kuwa msimamizi wa sekta ya
Bima mwenye kiwango kinachokubalika Kimataifa,kuendeleza ,kukuza
masoko ya Bima imara,shirikishi lenye kuthamini usawa na utendaji
mahiri,kwa manufaa na kulinda maslahi ya wateja.
Kwa upande
wake Afisa Mchambuzi
(Bima)kutoka (TIRA) Paul Abdiel amesema
kuwa mamlaka hiyo inafanya shughuli zake kwa weledi, kuwapa kipaumbele
wateja ,ushirikiano ,kuwajibika ,pamoja na kuaminika na
uwazi
Amewataka wateja wa Bima za vyombo
vya moto kuwa makini pale wanapokatiwa Bima hizo wazihakiki na
kuhakikisha kama ni halali ama la.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni