Kituo Kikuu cha Mabasi, Dodoma
|
Bw.
Justin Kisoka, Mtumishi wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa
Afrika Mashariki ambaye amebobea katika masuala ya uchumi akitoa somo
namna vijana wa Kitanzania watakavyoweza kuuza bidhaa zao ndani ya soko
la Afrika Mashariki lenye nchi sita na idadi ya watu wanaofikia milioni
165. |
|
Mfanyabiashara
akielezwa namna bidhaa zake ambazo amezibeba kichwani atakavyoweza
kuziuza katika nchi za Afrika Mashariki na kupata faida kubwa. |
|
Ujumbe
wa kutaka vijana na Watanzania kwa ujumla wazinduke ili wanufaike na
soko la Afrika Mashariki ulifikishwa kwa njia tofauti ikiwemo sanaa ya
maigizo. |
|
Baadhi
ya watu waliojitokeza kupata mbinu za kufanya biashara ndani ya Jumuiya
ya Afrika Mashariki. Hapa ilikuwa Kituo Kikuu cha Mabasi mjini Dodoma. |
Gandhi Hall , Mwanza
|
Bw.
Justin Kisoka akiwa kwenye bustani ya Gandhi Hall mjini Mwanza akitoa
somo namna Wanamwanza watakavyoweza kuuza Sato, Sangara na bidhaa
nyingine katika soko la Afrika Mashariki. |
|
Wanamwanza
acheni woga, vukeni mipaka ya Tanzania kuuza bidhaa zenu, ni baadhi ya
maneno aliyokuwa anayatumia Mchumi huyo katika kuwashajihisha vijana
wachangamke kuvuka mipaka ya Tanzania kuuza bidhaa zao. |
|
Dada somo limemkolea anapata maelezo zaidi kutoka kwa wataalamu wa Wizara ili shughuli ya kuvuka mipaka ianze mara moja. |
Viwanja vya Furahisha, Mwanza
|
Bw.
Abel Maganya, Mtaalamu wa Masuala ya Afrika Mashariki kutoka Wizara ya
Mambo ya Nje akitoa somo kwenye viwanja vya furahisha. |
|
Serikali
za Nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki zinatimiza majukumu
yake kwa kuweka mazingira mazuri ikiwemo sheria, kanuni na miundombimu
ili wanajumuiya mfanye biashara katika nchi unayopenda bila bugdha.
Msijifungie ndani vukeni mipaka kupeleka bidhaa mbalimbali. |
|
Baadhi ya Wananchi waliojitokeza katika viwanja vya furahisha. |
|
Mzee
anasema somo limengia barabara hivyo na uzee wangu nawahimiza wajukuu
zangu kufanya biashara ya kuvuka mipaka. Anafikisha ujumbe wake kwa
kushiriki kusakata dance linalohimiza biashara za kuvuka boda. |
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni