Inaonyesha machapisho yaliyo na lebo kifo. Onyesha machapisho yote
Inaonyesha machapisho yaliyo na lebo kifo. Onyesha machapisho yote

MAKAMU WA RAIS MHE. SAMIA SULUHU ASHIRIKI MSIBA WA MJUKUU WA RAIS MAGUFULI

H1
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan, akisaini kwenye Kitabu cha maombolezo ya msiba wa Mjukuu wa Mhe. Rais Dkt. John Magufuli, Maryfaustna Mlyambina, aliyefariki Nov 11, 2015. Shughuli za kuagwa mwili wa marehemu zilifanyika leo Nov 13, 2015 Kimara jijini Dar es Salaam, na baadaye msiba huo kusafirishwa kuelekea Mkoani Mwanza kwa maziko. Picha na OMR
H2
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan, akitoa heshima za mwisho mbele ya jeneza lenye mwili wa Mjukuu wa Mhe Rais John Magufuli, marehemu Maryfaustna Mlyambina, wakati wa shughuli za kuaga zilizofanyika Kimara jijini Dar es Dalaam,leo Nov 13, 2015. Picha na OMR
H3
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan, akimfariji Mhe. Rais Dkt. John Magufuli, wakati wa shughuli za kuaga mwili wa marehemu Maryfaustna Mlyambina zilizofanyika Kimara jijini Dar es Dalaam,leo. Marehemu ni mjukuu wa Mhe Rais. Picha na OMR
H5
Rais Dkt. John Magufuli (wa tatu kuli) Makamu wake (wa Nne kulia) Rais Mstaafu Jakaya Kikwete, Mke wa Rais,Mama Janeth Magufuli (kulia) na Mke wa Rais Mstaafu, Mama Salma Kikwete (kushoto) wakishiriki ibada maalum ya kumuombea marehemu wakati wa shughuli za kuaga mwili zilizofanyika Kimara jijini Dar es Salaam, leo Nov 13, 2015. Picha na OMR

MBUNGE WA JIMBO LA UKONGA MAREHEMU EUGIN ELISHIRINGA MWAIPOSA KUZIKWA JUMAMOSI NYUMBANI KWAKE KIPUNGUNI B

 
 
 
 Mume wa Marehemu,  Ally Ibrahim Mwaiposa akitoa heshima za mwisho kwa mwili wa mkewe Eugen Mwaiposa katika viwanja vya bunge mjini Dodoma.
 
Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Monduli, Edward Lowassa akitoa heshima za mwisho kwa mwili wa marehemu.
 
MBUNGE wa jimbo la Ukonga, dar es Salaam eugin Elishiringa Mwaiposa  (55) anataraji kuzikwa Jumamosi Juni 6,2015 nyumbani kwake Kipunguni B.

Taarifa kutoka kwa mmoja wa wanafamilia waliambia Father Kidevu Blog kuwa, Mwili wa marehemu uliwasili leo na kwenda kuhifadhiwa katika Hospitali ya Muhimbili na mazishi yanasubiri watoto wa marehemu walioko nje ya nchi.

Wistone Simbo amesema watoto wa marehemu wanaosubiriwa ni Mecktilda aliyeko nchini Canada na Samira aliyeko masomoni nchini Malaysia. 

Aidha Wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano leo walitoa heshima za mwisho kwa Mwili wa Mbunge huyo katika ibada iliyoendeshwa viwanja vya Bunge mjini Dodoma na kuhudhuriwa na mume wa marehemu  Ally Ibrahim Mwaiposa, Waziri Mkuu, Katibu Mkuu Kiongozi,a Naibu Spika wa Bunge na mawaziri.

Vilio na huzini vilitanda katika viwanja vya Bunge wakati watumishi wa Bunge, Wabunge, Mawaziri na wanahabari wakitoa heshima za mwisho kwa mwili wa marehemu hii leo kabla ya kusafirishwa kwenda jijini Dar es Salaam.

 Akizungumzia msiba huo kwa kunukuu mtari wa Biblia wa Ayubu 14:1 “Mwanadamu aliyezaliwa na mwanamke Siku zake za kuishi si nyingi”, Meya wa Manispaa ya Ilala ambaye pia ni diwani wa Gongo la Mboto, Jerry Silaa amesema ni pigo kubwa kwa jimbo la Ukonga na Halmashauri yake ya Ilala ambayo marehemu alikuwa ni Diwani hasa kutokana na kifo hicho kuwa cha ghafla.

“Hakika Mwanadamu aliyezaliwa na mwanamke Siku zake za kuishi si nyingi, Mwaiposa ni bora angekuwa aliumwa tukamuuguza lakini kifo hichi ni cha ghafla sana na hatuna budi kushikamana sote bila kujali itikadi zetu za kisiasa na tumzike ndugu yetu,” alisema Silaa.

Nae Diwani wa Kata ya Kipawa, jimbo la Segerea, Bona Kaluwa amesema sema kifo cha Mbunge wa Ukonga, ni pigo kwake na jamii nzima kwani alikuwa ni mtu wake wa karibu na majirani ambapo alikuwa ni mshauri wake mkuu wa masuala mbali ya kisiasa na familia kwa ujumla.
 


 Waombolezaji wakiwa viwanja vya Bunge mjini Dodoma.