Mume
wa Marehemu, Ally Ibrahim Mwaiposa akitoa heshima za mwisho kwa mwili
wa mkewe Eugen Mwaiposa katika viwanja vya bunge mjini Dodoma.
Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Monduli, Edward Lowassa akitoa heshima za mwisho kwa mwili wa marehemu. |
MBUNGE
wa jimbo la Ukonga, dar es Salaam eugin Elishiringa Mwaiposa (55)
anataraji kuzikwa Jumamosi Juni 6,2015 nyumbani kwake Kipunguni B.
Taarifa
kutoka kwa mmoja wa wanafamilia waliambia Father Kidevu Blog kuwa,
Mwili wa marehemu uliwasili leo na kwenda kuhifadhiwa katika Hospitali
ya Muhimbili na mazishi yanasubiri watoto wa marehemu walioko nje ya
nchi.
Wistone Simbo amesema watoto wa marehemu wanaosubiriwa ni Mecktilda aliyeko nchini Canada na Samira aliyeko masomoni nchini Malaysia.
Aidha
Wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano leo walitoa heshima za mwisho
kwa Mwili wa Mbunge huyo katika ibada iliyoendeshwa viwanja vya Bunge
mjini Dodoma na kuhudhuriwa na mume wa marehemu Ally Ibrahim Mwaiposa, Waziri Mkuu, Katibu Mkuu Kiongozi,a Naibu Spika wa Bunge na mawaziri.
Vilio
na huzini vilitanda katika viwanja vya Bunge wakati watumishi wa Bunge,
Wabunge, Mawaziri na wanahabari wakitoa heshima za mwisho kwa mwili wa
marehemu hii leo kabla ya kusafirishwa kwenda jijini Dar es Salaam.
Akizungumzia msiba huo kwa kunukuu mtari wa Biblia
wa Ayubu 14:1 “Mwanadamu aliyezaliwa na mwanamke Siku zake za kuishi si nyingi”,
Meya wa Manispaa ya Ilala ambaye pia ni diwani wa Gongo la Mboto, Jerry Silaa
amesema ni pigo kubwa kwa jimbo la Ukonga na Halmashauri yake ya Ilala ambayo
marehemu alikuwa ni Diwani hasa kutokana na kifo hicho kuwa cha ghafla.
“Hakika Mwanadamu aliyezaliwa na mwanamke Siku
zake za kuishi si nyingi, Mwaiposa ni bora angekuwa aliumwa tukamuuguza lakini
kifo hichi ni cha ghafla sana na hatuna budi kushikamana sote bila kujali
itikadi zetu za kisiasa na tumzike ndugu yetu,” alisema Silaa.
Nae Diwani wa Kata ya Kipawa, jimbo la Segerea,
Bona Kaluwa amesema sema kifo cha Mbunge wa Ukonga, ni pigo kwake na jamii
nzima kwani alikuwa ni mtu wake wa karibu na majirani ambapo alikuwa ni mshauri
wake mkuu wa masuala mbali ya kisiasa na familia kwa ujumla.
Waombolezaji wakiwa viwanja vya Bunge mjini Dodoma.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni