………………………………………………….
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
WIZARA YA HABARI VIJANA UTAMADUNI NA MICHEZO
WIZARA YA HABARI VIJANA UTAMADUNI NA MICHEZO
Taarifa kwa vyombo vya habari
Waziri wa Habari, Vijana,
Utamaduni na Michezo, Mheshimiwa Dkt. Fenella Mukangara (Mb.) ametuma
salamu za rambirambi kwa Baraza Kuu la Waislamu Nchini (BAKWATA) na
Waislamu wote nchini kufuatia kifo cha Sheikh Mkuu wa Tanzania Mufti
Shaaban Issa Bin Simba kilichotokea Jumatatu, tarehe Juni 15,2015 katika
hospitali ya TMJ Jijini Dar es Salaam alipokuwa anatibiwa.
Katika salamu hizo, Mhe. Mukangara
amesema kuwa ni jambo la kusikitisha kumpoteza kiongozi huyo ambaye
bado Taifa lilikuwa likimuhitaji hasa katika kipindi hiki cha kuelekea
uchaguzi Mkuu wa mwezi Oktoba mwaka huu.
Waziri huyo ameongeza kuwa Mufti
atakumbukwa kwa upole , unyenyekevu wake na kutopenda makuu,wakati wa
uhai wake marehemu alikuwa tayari kumsikiliza kila mtu bila kujali dini
au kabila lake.
“Nimepokea kwa huzuni nyingi taarifa ya kifo cha Sheikh Mkuu wa Tanzania Mufti Shaaban Issa Bin Simba ambaye alikuwa Kiongozi anayeshirikiana vizuri na viongozi wote wa serikali na vyama mbalimbali katika kuhakikisha Watanzania wanaendelea kuwa wamoja” amesema .

Amesema Waziri Mukangara:
“Nakutumia salamu zangu za rambirambi wewe Katibu Mkuu, BAKWATA na
waislamu wote nchini na naungana nanyi katika kuomboleza msiba huu
mkubwa katika nchi yetu.
Aidha, kupitia BAKWATA, natuma
salamu za dhati ya moyo wangu kwa familia ya marehemu kwa kumpoteza
mpendwa wao. Napenda wajue kuwa msiba wao ni msiba wangu. Pia, naungana
nao katika kumwomba Mwenyezi Mungu, Mwingi wa Rehema aiweke pema peponi
roho ya marehemu … Amina.”
Imetolewa na;
Idara ya Habari(MAELEZO)
15 Juni,2015
15 Juni,2015
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni