Waziri
wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo Mh. William Vangimembe Lukuvi akisalimia
viongozi wa NHC mara baada ya kuwasili eneo la Napupa Masasi kuzindua
nyumba za gharama nafuu zinazojengwa na NHC. Anayemuongoza Mh. Waziri ni
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa NHC Bw. Felix Maagi.
Waziri
wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo Mh. William Vangimembe Lukuvi akiongea na
hadhira iliyofurika katika sherehe za uzinduzi wa nyumba za gharama
nafuu zinazojengwa na NHC Wilayani Masasi.Alizitaka taasisi zinazotoa
huduma ya umeme na maji kutekeleza majukumu yao ili kupunguza gharama za
uuzaji wa nyumba zinazojengwa na waendelezaji wote wa makazi.
Sehemu ya umati wa wananchi waliohudhuria sherehe za uzinduzi wa nyumba za gharama nafuu zinazojengwa na NHC Wilayani Masasi.
Kaimu
Mkurugenzi Mkuu wa NHC Bw. Felix Maagi. Akitoa taarifa ya mradi wa
nyumba za gharama nafuu zinazojengwa na NHC Wilayani Masasi kwa Waziri
wa ardhi, nyumba na Maendeleo ya Makazi Mh. William Lukuvi aliyefika
katika mradi huo wenye nyumba 54 na kuuzindua.
Mkurugenzi
wa Halmashauri ya Masasi Bi Beatrice Dominic akitoa taarifa ya
usimamizi wa ardhi kwa Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo Mh. William
Vangimembe Lukuvi alipozuru Masasi na kuzindua nyumba za gharama nafuu
zinazojengwa na NHC.
Waziri
wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo Mh. William Vangimembe Lukuvi akipewa
maelezo ya mradi wa nyumba za gharama nafuu zinazojengwa na NHC Wilayani
Masasi na Kaimu Mkurugenzi wa Uendelezaji Miliki wa NHC Bw. Haikamen
Mlekio.
Waziri
wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo Mh. William Vangimembe Lukuvi akiweka
jiwe la msingi katika nyumba za gharama nafuu zinazojengwa na NHC
Wilayani Masasi ambazo ujenzi wake utakamilika mwezi Oktoba mwaka huu.
Waziri
wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo Mh. William Vangimembe Lukuvi
akisalimiana na wazee aliyowahi kufanya nao kazi Wilayani Masasi mwaka
1975 akiwa Katibu wa Vijana wa Wilaya, baada ya kukutana nao Ikulu ndogo
Mjini Masasi.
Waziri
wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo Mh. William Vangimembe Lukuvi,akionyeshwa
na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Masasi Bi. Bi Beatrice Dominic mali na
magari yaliyounguzwa na vijana wa Masasi kutokana na vurugu zilizowahi
kutokea huko nyuma na kuunguza pia jengo la Ofisi ya ardhi ikiwemo
nyaraka zote. Hadi sasa Halmashauri hiyo haina Ofisi za kutosha kufanyia
kazi na wala usafiri wa kusaidia utendaji wa kazi wenye tija.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni