Balozi wa Spain nchini, Mh. Luis Cuesta
Civis (kulia) na Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na
Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP), Alvaro
Rodriguez (katikati) wakiwasili kwenye ofisi za Halmashauri ya wilaya ya
Bagamoyo kabla ya ziara ya kuelekea katika kijiji cha Chasimba kukagua
miradi inayofadhiliwa na TASAF katika wilaya ya Bagamoyo. Kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF), Ladislaus Mwamanga.(Picha na Zainul Mzige wa modewjiblog).
Na Modewjiblog team, Bagamoyo
SERIKALI ya Hispania imetoa shilingi
bilioni 3.1 kusaidia miradi ya maendeleo ya jamii nchini ambayo mingine
inatekelezwa na Mfuko wa Maendeleo ya Jamii, TASAF.
Fedha hizo zimetolewa kupitia mfuko wa
maendeleo endelevu (SDGF) zilizotolewa kwa mashirika ya Umoja wa Mataifa
yanayofanya shughuli zake hapa nchini.
Mashirika hayo ni Shirika la Maendeleo la
Umoja wa Mataifa (UNDP) ,Shirika la Umoja wa Mataifa la watoto (UNICEF)
, Shirika la Umoja wa Mataifa la Idadi ya watu (UNFPA), na Shirika la
Kazi Duniani( ILO).
Hayo yamesemwa katika ziara ya Balozi wa
Hispania nchini, Luis Cuesta Civis na Mratibu Mkazi wa Mashirika ya
Umoja wa Mataifa nchini na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja
wa Mataifa (UNDP), Alvaro Rodriguez katika kijiji cha Chasimba kilichopo
wilayani Bagamoyo, Pwani jana.
Ziara yao ilikuwa ya kukagua miradi
inayofadhiliwa na TASAF katika wilaya ya Bagamoyo. Bagamoyo ni miongoni
mwa wilaya nane zilianza kupokea fedha za TASAF na kuonekana kuleta
mabadiliko makubwa katika jamii.
Hata hivyo moja ya shughuli wanazofanya wakazi wa Chasimba ni kilimo wakiwa na pato la sh 350,000 kwa mwaka.
Huduma za jamii zinazopatikana katika vijiji hivyo ni pamoja na shule ya msingi, barabara inayopita kijiji ni hapo na zahanati.
Wakati wa utekelezaji wa awamu ya pili ya
TASAF jamii ya Chasimba ilijenga madarasa matatu na ofisi ya walimu.
Miradi hiyo ilizinduliwa mwaka 2007 na kukamilika mwaka 2008. Katika
miradi hiyo TASAF ilichangia 30,415,471.
Aidha kijiji cha Chasimba ni miongoni mwa
vijiji 17 ambavyo vinatekeleza mradi wa CB-CCT toka mwaka 2008/2009.
Katika kipindi hicho wamepata ruzuku ya jumla ya sh 28,325,400.
Pia kijiji hicho kina kaya 197
zinazonufaika na mpango wa kunusuru kaya maskini TASAF III (PSSN) ambapo
tayari wamepewa ruzuku ya shilingi 43,227,190 katika mikupuo 9.
Akizungumza kijijini hapo Mratibu Mkazi
wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini na Mwakilishi wa shirika la
Maendeleo (UNDP), Alvaro Rodriguez aliishukuru serikali ya Tanzania na
Hispania kwa kufanikisha shughuli hiyo nzito ya kusaidia jamii
kukabiliana na umaskini.
Balozi wa Spain nchini, Mh. Luis Cuesta
Civis (kulia) na Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na
Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP), Alvaro
Rodriguez wakisaini kitabu cha wageni mara baada ya kuwasili kwenye
ofisi za Halmashauri ya wilaya ya Bagamoyo.
“ Tunashukuru serikali ya Tanzania na
Hispania kwa kushirikiana kusaidia wananchi wa Tanzania kukabiliana na
umaskini. Kwa kufanyakazi na watu wa hali ya chini kabisa miradi hii
imewezesha familia kupeleka shule watoto wao, kushiriki katika mipango
ya uwekaji wa akiba na kuongeza kipato. Jukumu letu la pamoja ni kuondoa
umaskini Tanzania” alisema Alvaro.
Naye Balozi wa Hispania Luis amesema
kwamba serikali ya Hispania inaamini katika kusaidia kupambana na
umaskini kwa kusaidia jamii kukabiliana na changamoto zinazowakabili.
Alisema wataendelea kufanya hivyo kupitia
Mashirika ya Umoja wa Mataifa ambayo yanafanyakazi kwa kushirikiana na
serikali za mikoa na mitaa ambazo ndizo ziliopo karibu na wananchi
husika.
Alisema kwamba wanaamini mradi wa kunusuru kaya maskini unafanya wajibu wake kwa kuwafikia wananchi maskini sana.
Alisema mradi huo ni moja ya miradi
inayoonesha umuhimu wa kufanyakazi pamoja kati ya Mashirika ya Umoja wa
Mataifa na nchi wahisani.
Kijiji cha Chasimba pia kinafanya kazi za
ujenzi mbalimbali kuanzia Machi 23, mwaka jana. Kazi hizo ni pamoja na
ujenzi wa barabara ya kilomita 1.1 ya Chasimba-Kiegea.
Aidha kumekuwepo na mafanikio makubwa tangu kuanza kwa mradi wa PSSN kijijini hapo.
Alisema kumekuwepo na ongezeko la
wanafunzi wanaoandikishwa na kuhudhuria shule, aidha madarasa matatu
yamejengwa na ofisi ya mwalimu.
Akizungumzia mafanikio Mkurugenzi
Mtendaji wa TASAF Ladislaus Mwamanga alisema kuna mabadiliko makubwa
katika maisha ya watu kutokana na utekelezaji wa miradi hiyo katika
kijiji.
Aidha wananchi wa Chasimba wamepata
ushawishi mkubwa wa kushiriki katika miradi ya maendeleo ndio sababu ya
mafanikio yanayoonekana.
Kwa mujibu wa taarifa zilizopo mradi wa
kunusuru kaya maskini umesaidia watoto kwenda shuleni wakiwa
wametimiziwa mahitaji yao yote.
Aidha mradi huo umeweza kufanikiwa kufanya watu wapendekwenda kiliniki na kuangalia afya za mama na watoto.
Aidha familia zilizopewa fedha sasa wamebadilisha namna ya mfumo wa kupata lishe na kuwa na uhakika na lishe.
Aidha ujira kutokana na kazi unaotarajiwa
kutolewa ni jumla ya dola za Marekani 15,991 wakati gharama za vifaa
na ufundi ni dola za Marekani 5,328.
Jumla ya kaya 197 zitashiriki katika
miradi ya ujenzi kwa kipindi cha miezi minne na utaendelea kwa miaka
miwili katika kipindi hicho hicho.
Balozi wa Spain nchini, Mh. Luis Cuesta
Civis (kulia), Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na
Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP), Alvaro
Rodriguez (kushoto) pamoja na Katibu Tawala wa Wilaya ya Bagamoyo, John
Mahali (katikati) wakielekea kwenye ukumbi wa mikutano kwa ajili ya
kupokea taarifa ya mradi wa TASAF katika wilaya ya Bagamoyo.
Katibu Tawala wa Wilaya ya Bagamoyo,
John Mahali (wa pili kushoto) akifafanua jambo kwenye mkutano wa kupokea
taarifa ya maendeleo ya miradi ya TASAF katika wilaya ya Bagamoyo kwa
wadau wa maendeleo waliotembelea wilaya hiyo kukagua miradi
inayofadhiliwa na Tasaf. Kulia ni Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja
wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa
(UNDP), Alvaro Rodriguez sambamba na Balozi wa Spain nchini, Mh. Luis
Cuesta Civis (wa pili kulia) na kushoto ni Kaimu Mkurugenzi wa wilaya ya
Bagamoyo, Hilda Gadi.
Mkurugenzi Mtendaji wa Mfuko wa
Maendeleo ya Jamii (TASAF), Ladislaus Mwamanga akizungumza kwenye
mkutano mfupi wa kupokea taarifa ya miradi inayofadhiliwa na TASAF
wilayani Bagamoyo. Wa pili kulia ni Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya
wilaya ya Bagamoyo Bi. Hilda Gadi, Katibu Tawala wa Wilaya ya Bagamoyo,
John Mahali (katikati), Balozi wa Spain nchini, Mh. Luis Cuesta Civis
(wa pili kulia) pamoja na Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa
na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP),
Alvaro Rodriguez.
Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya
wilaya ya Bagamoyo Bi. Hilda Gadi akitoa taarifa ya maendeleo ya mradi
wa TASAF wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini katika wilaya ya Bagamoyo
mbele ya wadau wa maendeleo.
Balozi wa Spain nchini, Mh. Luis Cuesta
Civis akizungumzia ufadhili wa serikali yake kusaidia miradi ya
maendeleo ya jamii nchini ambayo mingine inatekelezwa na Mfuko wa
Maendeleo ya Jamii, TASAF.
Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa
Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa
(UNDP), Alvaro Rodriguez akizungumza katika mkutano huo ambapo
aliishukuru serikali ya Tanzania na Hispania kwa kufanikisha
shughuli ya kusaidia jamii kukabiliana na umaskini ikiwa ni moja ya
utekelezaji wa Malengo ya Millenia (MDG's).
Baadhi ya wafanyakazi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa na wafanyakazi wa TASAF wakishiriki kwenye mkutano huo.
Baadhi ya waandishi wa habari waliohudhuria mkutano huo katika ofisi za halmashauri ya wilaya ya Bagamoyo.
Picha ya pamoja mara baada ya mkutano.
Balozi wa Spain nchini, Mh. Luis Cuesta
Civis (katikati) akijadiliana jambo na Mratibu Mkazi wa Mashirika ya
Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa
Mataifa (UNDP), Alvaro Rodriguez (kulia) pamoja na Katibu Tawala wa
Wilaya ya Bagamoyo, John Mahali (kushoto).
Balozi wa Spain nchini, Mh. Luis Cuesta
Civis (kulia) akiteta jambo na Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya
wilaya ya Bagamoyo Bi. Hilda Gadi. Kushoto ni Katibu Tawala wa Wilaya
ya Bagamoyo, John Mahali.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni